Kulikuwa na sababu gani za msingi, au kuna faida gani kwa wasaidizi wa Rais Magufuli kumpuuza Makamu wa Rais Samia Suluhu?

Wasaidizi wa rais wanamdanganya kwa maslahi yao wenyewe. Kulikuwa hakuna haja ya kusema Magufuli ataudhuria.

Wasaidizi wanawadanganya ‘wadanganyika’ wa TZ kwa maelekezo ya mkuu wao ili kujaribu kujenga taswira chanya.

Viongozi Wanapaswa kumcha Mungu sana, na kuiogopa teknologia!
 
Hii ishu mbona mnaishupalia sana,?,hakuna aliepuuzwa,,jpm alikuepo,akapata udhuru akatoka,na hata makamu ndivyo aluvyosema,,
Sioni sababu ya watu kuvalia njuga wiki nzima ishu ambayo haipo.
Kama sababu ni iyo basi naweza sema siasa imetumika hapa....
 
Kwani Makamu wa Rais anapokuwa anamuwakilisha Rais huko nje ( hasa Ulaya ) au hata katika nchi zingine hapa hapa Barani Afrika Kiitifaki huwa inatambulikaje?

Tuacheni Nongwa na tupunguze Kumsakama Rais au Taasisi yake ya Urais kwa Chuki zetu kila Uchao tu. Kiitifaki sijaona tatizo lolote lile ikisemwa ( ikitangazwa ) kuwa Rais ameshiriki Kikao hata kama aliyekihudhuria ni Makamu wake.

Hilo la Waziri Mwigulu Nchemba Kumtishia huyo Dada Maria kama ni kweli basi nadhani PhD yake haitumii vyema katika Kufikiri ( Kufikiria ) hivyo airejeshe tu huko Chuoni na aendelee kubakia na Upumbavu pamoja na Ushamba wake.

Alichotakiwa Kufanya Waziri Nchemba si Kumtishia Dada Maria ( kama ni kweli ) bali ni Kumuelekeza tu kwa Mtazamo wa Kiitifaki na Kidiplomasia juu ya hilo na wala hili Jambo lisingekuwa Kubwa hivi na la Kimjadala. Makamu wa Rais anafanya Kazi za Rais, ni Msaidizi wake na Muwakilishi wake Mkuu katika Matukio yote ya Kiitifaki hivyo akihudhuria Yeye ( Makamu ) na ikatangazwa Rais amehudhuria wala hakuna Kosa ( tatizo ) lolote hapo.
 
Taarifa ya Ikulu kwamba Rais Magufuli kashiriki hicho kikao iko wapi?
 
Uwekewe na nani, wasiliana na Msigwa maana yeye na ww ni wapambe wa jiwe atakuambua alichofanya juzi.
Kwanini mnashadadia hata taarifa zinawekwa humu na wahuni?

Mimi naomba unipe taarifa rasmi ya Ikulu inayosema Magu ndio alishiriki hicho kikao.
 
Makamu wa Rais anafanya Kazi za Rais, ni Msaidizi wake na Muwakilishi wake Mkuu katika Matukio yote ya Kiitifaki hivyo akihudhuria Yeye ( Makamu ) na ikatangazwa Rais amehudhuria wala hakuna Kosa ( tatizo ) lolote hapo.
Hizi akili ni za wapi jamani! Ikiwa hivo hatuwezi kusema rais amehudhuria. Sahihi tunasema makamu amehudhuria/amehudhuria kwa niaba/amemuwakilisha etc. Nitoe mfano, ambao sio mzuri samahani: Mh. makamu angepatwa na tatizo la kiafya, eg akafariki akiwa kwny kikao, je tungesema rais amefariki? Jibu ni a bg NO.
 
Hizi akili ni za wapi jamani! Ikiwa hivo hatuwezi kusema rais amehudhuria. Sahihi tunasema makamu amehudhuria/amehudhuria kwa niaba/amemuwakilisha etc. Nitoe mfano, ambao sio mzuri samahani: Mh. makamu angepatwa na tatizo la kiafya, eg akafariki akiwa kwny kikao, je tungesema rais amefariki? Jibu ni a bg NO.
Una tatizo Kubwa la kutokujua Itifaki.
 
Back
Top Bottom