Kulikuwa na sababu gani za msingi, au kuna faida gani kwa wasaidizi wa Rais Magufuli kumpuuza Makamu wa Rais Samia Suluhu?

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,925
2,000
IMG_4239.jpg


Inapotokea kikao cha Jumuia ya Afrika Mashariki kikahudhuriwa na Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu, halafu ikulu ikatoa taarifa kuwa ni Rais Magufuli ndiye alyeshiriki kikao hicho, Je, Hii si ishara ya kumpuuza makamu wa Rais?

Mwanaharakati Maria Sarungi-Tsehai amefichua uongo huo wa Ikulu uliotangazwa na mkurugenzi wa habari wa ikulu Bw. Gerson Msigwa aliyetoa taarifa ya Mh. Rais kushiriki kikao cha jumuia ya Afrika Mashariki.

Maria ameweka picha, video na taarifa za maandishi zikimuonesha Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu akikaribishwa na Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta huku Rais wa Rwanda, Paul Kagame akiongoza kikao hicho kilichofanyika kwa njia ya mtandao.

Wakati huohuo Waziri wa Sheria na Katiba Bw. Mwigulu Nchemba amempiga mkwara mzito Maria Sarungi baada ya kufichua uongo huo.

Kulikuwa na sababu gani za msingi, au kuna faida gani kwa taifa kumpuuza Makamu wa Rais?

Hawa wasaidizi wa Rais wana mpango gani na Rais hadi kuweka uongo wa kitoto namna hii?

Mwigulu naye anatoa vitisho kwa faida ya nani?

IMG_4240.jpg

Dr cyrilo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom