Kulikuwa na haja ya wabunge 83 kwenda Misri kuangalia AFCON ?Hapa tatizo la uwekezaji kwenye michezo si fedha bali ubinafsi na utashi uliojaa upumbavu

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Wabunge wote walioenda nlisikia ni 83, achilia mbali maafisa wengine wa serikali almost 110, the kwa haraka haraka tickets + accomodation + foods etc ya kipindi chote si chini ya dola 10,000 kwa mmoja, zidisha kwa 110 unapata dola 1,100,000 zidisha kwa exchange rate ya 2300 unapata Tzs 2,300,000,000(bilioni mbili na milioni 300) kwa siku hizi chache tu.
Mkuu wakati unapiga hesabu hizo nnaomba nikujuze kuwa hao ni wachache, maana utaratibu ni kwamba wanakwenda kwa makundi, kila mechi moja linakwenda kundi la wabunge, yaani mechi ijayo wanakwenda wengine na ile mechi ya Kenya as well, na hao Wabunge ni wa CCM plus wa Upinzani, nnachojua hakuna mwanasiasa mwenye uchungu na mambo yetu, wote wanapambania maisha yao, shubaamit zao wote

Najiuliza maswali sisi ambao tunashinda kuilaumu Taifa stars kwenye mitandao kwa kufanya vibaya tunashindwa kujua kuwa pale timu zote za kundi letu ispokuwa Kenya wana wachezaji wengi wa kulipwa barani Ulaya, jana wale wa Senegal wana mpaka mchezaji anayecheza Barcelona na Liverpool Timu ambazo zina ubora wa juu kabisa, pale hata kama ni uwezo wa mtu binafsi ndo unamfikisha huko lakin tumeshuhudia nchi nyingi zikiwaandaa vijana kwa kuwaweka kwenye academies, na inakuwa strategy ya serikali na taasisi husika juu ya masuala ya mpira,

Leo hii sisi ambao hatuna hata wachezaji watano professional tunaanza kuwaza kujilinganisha na wenzetu kwa kudhani kwamba kuna muujiza utajitokeza bila kujishughulisha na kuwekeza, hata umtegemee Mungu , pia na washindani wako wanamtegemea Mungu , hapo ndo Mungu anacha Law of nature to decide, yaan aliyejiandaa ndo awe mshindi, najiuliza hivi hizo bilion tungeandaa academy ngapi? au tungewezesha kiasi gani kutengeneza mazingira ya uwekezaji katika mpira?
Tukumbuke wao taifa stars kama wachezaji hawana cha kupoteza maana wakitolewa tiyari wamesha tour vya kutosha na kupiga picha na mapiramid tuliyosimuliwa kuhusu ujenzi wake hahaha,

Hapa unajua wazi tatizo la uwekezaji kwenye michezo sio fedha bali ubinafsi na utashi uliojaa upumbavu na ujinga wa hali ya juu sana!

Britanicca,
 
Hayo yapo mpaka kwenye chama, unakuta mtu badala ya kuandaa mikakati mizuri ya kushawishi wananchi ili apendwe yeye na chama chake unasikia hakuna nyutro, nione unatangaza mpinzani kashinda aisee tanzania bado sana

Kama wamejilipia kwa pesa zao sio hoja.. Hoja Ni kwamba hiyo pesa awawez kuitoa sadaka au kusaidia watoto yatima.. au kutoa kwa maendeleo ya majimbo yao..
 
Kila Mbunge amejilipia Kwa gharama zake kama mashabiki waliojitolea Kwa niaba ya watanzania.
Sio hela ya serikali ni hela zao za mfukoni. Acheni uchonganishi na kujifanya mnajua kila kitu.
Hata wewe ukiwa na uwezo unaombwa kwenda kushangilia. Kuna kampuni inasafirisha mtu mmoja Kwa Dola 1800 Kwa gharama zote ambapo ni pamoja na mapazi nauli na chakula. Ambapo ni Sawa na sh 3,600,000#
 
Tupe mfano wa aliyeenda kwa gharama hiyo, acha assumption kijana,
Fare ya Cairo to DSm flight return ticket unaijua?
Gharama za kula na malazi per day unazijua?
Gharama ya tikect kuangalia mechi AFCON unaijua?
 
Unachokisema ni Tatizo la kila mahala Tanzania, lakini Watanzania tunashindwa kujua mzizi wa tatizo mpaka leo kiasi ya kila siku kushuhudia tatizo na shida mpya..

Mkuu amini usiamini Matatizo nchi hii yataisha siku CCM ikiondoka na kufa kabisa, na kuanzia watanzania tuwe na uwezo wa kubadili Serikali wakati wowote tukitaka. tofauti na hapo tutaendelea kuona vituko kila siku.. Taifa la watu zaidi ya 50mil na km za mraba zaidi ya laki tisa kila siku eti ni watu wakushindwa kwenye vitu kama hivi..
 
Kila Mbunge amejilipia Kwa gharama zake kama mashabiki waliojitolea Kwa niaba ya watanzania.
Sio hela ya serikali ni hela zao za mfukoni. Acheni uchonganishi na kujifanya mnajua kila kitu.
Hata wewe ukiwa na uwezo unaombwa kwenda kushangilia. Kuna kampuni inasafirisha mtu mmoja Kwa Dola 1800 Kwa gharama zote ambapo ni pamoja na mapazi nauli na chakula. Ambapo ni Sawa na sh 3,600,000#
Thibitisha mkuu
 
Kwanini hizo hela wasingelipia TBC1 hiyo michuano ikaonyeshwa wananchi wengi tuweze kuona? Huo ni ubinafsi usio na msingi. Kuna mjinga mmoja jana anasema eti hata Mch. Msigwa yuko, akidhani akitutajia mbunge wa upinzani ndio tutaona sawa. Hao wabunge wote walioenda huko pamoja na spika wao ni wauza sura kama wauza sura wengine.
 
Me binafsi sijaona umuhim wa viongozi wetu kwa idadi hiyo kwenda uko Misri ,,labda Kama wameenda kutalii au kushaangaa magorofa ..tusijifanye wazalendo kwa stail hii ..ata Kama ela ni za kwao ..ila kwa waelewa wa mpira ..Tumeenda kushiriki..
 
Hizi pesa si zilikuwa zinatosha kutulipa watumishi madai na malimbikizo ya mishahara

Back
Top Bottom