Kulikuwa na haja ya kumtimua Kafulila NCCR? Mh. Moses Machali Live on Star TV

Hata mimi nimeshangaa uelewa wa hawa jamaa wa NCCR Mageuzi kuhusu hii order ya mahakama. Sheria imewatupa mkono hawa.
NCCR wana best lawyers kama akina Mvungi..nafikiri wana uelewa zaidi wa sheria kuliko unavyowashutumu
 
Kuongea mambo ya chama nje ya chama hilo ni kosa kwa kuwa yeye sio kiongozi, ila kumwambia mwenyekiti ni ccm ndio nashangaa hilo ni tusi? kweli nccr wamekwishini
 
Kaka Yahya, asalaam,

Ni aibu kwa VIJANA kama Machali na mwenzake kutetea ubakaji wa democrasia na kuhusu suala ya kufukuzwa mbunge mwenzao KIJANA, kisa kulinda maslahi ya mwenyekiti, naona aibu kuwa KIJANA wa kitanzania mpenda democrasia ya kweli asubuhi ya leo.
Vipi juu ya wale watakaojivua ubunge baada ya kuchoshwa na siasa uchwara??
Je wazee nao wamtetee mzee mwenzo akivuliwa ubunge kwa utovu wa nidhamu just because ni mzee mwenzao?
 
Hii ni tuhuma nzito TUNAOMBA MTUPE USHAHIDI WA MAANDISHI JUU YA TUHUMA MLIZOMTUPIA KAFULILA KUWA YEYE NDO ALIMSHAWISHI MBATIA AMFUNGULIE MDEE KESI.
Kafulila anabebeshwa kila zigo la taka lililopo NCCR Mageuzi.

Kama kweli mbatia hakuwa na nia ya kupinga ushindi wa Mdee hadi aliposhauriwa na Kafulila basi naye ni kichwa cha nazi. Atafunguaje kesi bila sababu za msingi?
 
Hata mimi nimeshangaa uelewa wa hawa jamaa wa NCCR Mageuzi kuhusu hii order ya mahakama. Sheria imewatupa mkono hawa.
Of course NCCR haija-take any further action baada ya order kutolewa. Order ilikuja actions kadhaa zilishachukuliwa. Further actions zilizopo/zilizozuiliwa ni pamoja na kumvua ubunge kafulila (hilo si wajibu wa NCCR), action nyingine ni Mkutano Mkuu wa NCCR kupitia maamuzi ya Halmashauri kuu (hilo sasa NCCR haiwezi kufanya maana kuna zuio la mahakama). Kwa maana hiyo order inazuia rufaa ya Kafulila kusikilizwa ndani ya chama
 
Tunafanya taratibu kumpata Ndg.Kafulila wiki ijayo katika sehemu ya pili ya mjadala huu. Tunategemea ushiriki wenu wanaJF
Yahya,
Tutakuwa pamoja panapo majaliwa. Naomba ujitahidi kupata mwanasheria mzuri anayeweza kutoa tafsiri sahihi ya order ya mahakama kuu. Machali na NCCR yake wanajikanyaga tu, hawaeleweki.
 
Mh Mh...

This' serious now.

Hebu kwenda deep kidogo.
Mkuu Invisible, deep yenyewe ndio hiyo, haya mambo ni mazito kuliko tunayoyaona juu juu. CCM mara nyingi kama sio zote ndio mainjinia wa migogoro ya vyama vya upinzani. Mbana Hassan, Mshirika wa Kafulila ni mzee asiyekuwa na kipato cha kumwezesha kuzunguka nchi nzima, ghafla alipata uwezo huo kwa mijihela ya Mkono. Hela ndio shina la dhambi hii ndugu yangu
 
Yahya,
Tutakuwa pamoja panapo majaliwa. Naomba ujitahidi kupata mwanasheria mzuri anayeweza kutoa tafsiri sahihi ya order ya mahakama kuu. Machali na NCCR yake wanajikanyaga tu, hawaeleweki.
Atafutwe Dr. Mvungi, wawekwe studio moja na Mhe.Kafulila ili tujue mbivu na mbichi waziwazi
 
Of course NCCR haija-take any further action baada ya order kutolewa. Order ilikuja actions kadhaa zilishachukuliwa. Further actions zilizopo/zilizozuiliwa ni pamoja na kumvua ubunge kafulila (hilo si wajibu wa NCCR), action nyingine ni Mkutano Mkuu wa NCCR kupitia maamuzi ya Halmashauri kuu (hilo sasa NCCR haiwezi kufanya maana kuna zuio la mahakama). Kwa maana hiyo order inazuia rufaa ya Kafulila kusikilizwa ndani ya chama

Waridi,
Nashukuru kwa ufafanuzi lakini sidhani kama ndivyo ilivyo. Kama ni kuzuia further actions pekee ndiyo order ya mahakama imezuia basi Kafulila si mwanachama wa NCCR na hivyo si mbunge!

Hiyo order ya mahakama ikipatikana hapa itatusaidia kujiridhisha kama hiyo ndiyo tafsiri yake.
 
Ni mjadala mzuri lakini ninaomba Kafulila na yeye angekuwepo ili kuweka uwiano kwasababu Mh. Machali anapomshambulia alafu yeye hayupo kujieleza ili tuweze kuelewa ukweli uliodhahiri nadhani tutakuwa hatumtendei haki Mh. Kafulila.

Jumapili ijayo Kafulila atakuwapo
 
Mkuu Invisible, deep yenyewe ndio hiyo, haya mambo ni mazito kuliko tunayoyaona juu juu. CCM mara nyingi kama sio zote ndio mainjinia wa migogoro ya vyama vya upinzani. Mbana Hassan, Mshirika wa Kafulila ni mzee asiyekuwa na kipato cha kumwezesha kuzunguka nchi nzima, ghafla alipata uwezo huo kwa mijihela ya Mkono. Hela ndio shina la dhambi hii ndugu yangu

Hapa ndipo kazi pevu ilipo.

Mbatia katuhumiwa kutumiwa na CCM lakini hachukuliwi hatua.

Kafulila katuhumiwa kutumiwa na CCM, amechukuliwa hatua mara moja.

Maalim Seif ametuhumiwa kutumiwa na CCM lakini hajachukuliwa hatua.

Hamadi Rashid katuhumiwa kutumiwa na CCM, amechukuliwa hatua mara moja.
 
jee kuna haki ya mtu anayevuruga nchi au chama au taasisi yeyote ile kachiliwa tuu kuendelea?

watanzania wanaona ni kitu kipya kwao eti mbunge kufukuzwa coz hatuna desturi hiyo tumezoea tuuu kuwakumbatiaaa
 
Tusubiri iyo jpili tujue na ukweli wa kafulila ila kinachoonekana apa ni Kama vile viongozi wa vyama hawapendi kukosolewa. Pia tahadhari kwa magazeti yanatugomanisha nahisi yanatumiwa na ccm
 
Vipi juu ya wale watakaojivua ubunge baada ya kuchoshwa na siasa uchwara??
Je wazee nao wamtetee mzee mwenzo akivuliwa ubunge kwa utovu wa nidhamu just because ni mzee mwenzao?

Tatizo ni kwamba viongozi wengi wa vyama ni wazee na hawako tayari kuona nafasi zao zinahatarishwa na vijana, kwahiyo hutaona mzee akifukuzwa ndani ya chama zaidi ya kushauriwa ajipime mwenyewe!

Umemsikia bila shaka Machali akisema James Mbatia ni taasisi, aking'olewa katika nafasi ya uenyekiti chama kitasambaratika! Kwahiyo utaona ni kwanini Mbatia analindwa kwa nguvu zote na kwa gharama yoyote.
 
hakukuwa na njia mbadala kwa kafurila kuwekwa sawa kwa mujibu wa taratibu za NCCR tofauti na kutimuliwa? na kwa nini vijana walio ndani ya chama kama nyie wote hamuwezi kuwa kitu kimoja kwa maslahi ya taifa inapobidi mbona bado muda wa kufanya migogoro?
 
NCCR wana best lawyers kama akina Mvungi..nafikiri wana uelewa zaidi wa sheria kuliko unavyowashutumu

Sijawashutumu bali nimeeleza masikitiko yangu juu namna wanavyojikanganya katika kuitafsiri order ya mahakama.

Btw, best lawyers Tanzania na lundo la mikataba feki!!

Hii inanikumbusha wakati nasoma elimu ya juu wenzetu wakafukuzwa chuo. Wakaenda mahakama kuu na kupata order ya ''ku-maintain status quo''. Ilikuwa shughuli pevu kwa wanasheria wa chuo kuielewa na kuitafsiri sahihi order hiyo!
 
Tutaendelea wiki ijayo Wadau Asante kwa michango yenu wanaJF Maswali haya nimeyahifadhi mpaka wiki ijayo

mnaweza kuweka hiyo order ya mahakama hapa jamvini ili tuidadavue? naona kila mtu anainterpret kivyake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom