Kulikuwa na haja ya kumtimua Kafulila NCCR? Mh. Moses Machali Live on Star TV

Kwa nini NCCR Mageuzi (na vyama vingi vya upinzani) mnashindwa kushikilia kanuni za party institutionalization na badala yake mnafuata kanuni za uendeshaji chama kwa kuzingatia utashi wa mtu mmoja (big man philosophy)?
 
kama kafulila anasema ana hofu chama kitaitwa CCM B mbona yeye mwenyewe tulimsikia TBC akisema NCCR ni photocopy ya CCM?
 
Kwa hizi tuhuma nadhani Kafulila alikuwa anastahili kufukuzwa. Lakini hii mada ingenoga zaidi kama Kafulila mwenyewe angekuwepo
 
Rest In Peace Regia!

Kunatuhuma kuwa Mkutano uliomuondoa Kafulila ulikuwa na Mamluki (wasio wajumbe halali), Aidha upigaji kura ulikuwa wa kura za wazi ilikuua haki ya maamuzi ya wajumbe
 
Further actions to IMPLEMENT THE DECISIONS. Sidhani kama inahitaji phd ya sheria kuielewa. Anyway mimi sina a b c za sheria, i stand to be educated
 
Hii ni tuhuma nzito TUNAOMBA MTUPE USHAHIDI WA MAANDISHI JUU YA TUHUMA MLIZOMTUPIA KAFULILA KUWA YEYE NDO ALIMSHAWISHI MBATIA AMFUNGULIE MDEE KESI.
 
Mahakama imezuia NCCR kuchukua uamuzi zaidi ili iweze kuhoji ufukuzwaji wa Kafulila na kama mbunge anatakiwa awe mwanachama kwa mujibu wa katiba basi by implication Kafulila bado ni mwanachama mpaka mahakama itakapoamua vinginevyo.
 
Kafulia alimwambia mwana Kigoma mwenzake, kwamba anataka NCCR iwe mali ya Kigoma kama CHADEMA ilivyo mali ya Kilimanjaro, kikosi chake cha kufanya hivyo ilikuwa kiwe yeye, Mzee Rungwe na Zitto. Alipomshirikisha dili hilo Machali na Msabaha (wote wa Kigoma) ndipo alipoingia chaka
 
Baadaye iligundulika kwamba Kafulila yuko financed na watu mbalimbali, inasemekana hadi Nimrod Mkono anahusika katika kutoa mijihela ya kuimaliza NCCR
 
Inasikitisha, inamaana ni marufuku kukosoana? nionavyo mimi Mtu mwenye damu ya upinzani harufu ya kwanza kuisikia ni ya ccmafisadi, kafulila alisikia harufu ya kiccm,ccm ktk chama chao na inaonyesha kweli harufu ile ipo. mungu ibariki tanzania.....inaonyesha hawa nccr wana zile sera za zidumu fikra za mwenyekiti hawa.
 
Kaka Yahya, asalaam,

Ni aibu kwa VIJANA kama Machali na mwenzake kutetea ubakaji wa democrasia na kuhusu suala ya kufukuzwa mbunge mwenzao KIJANA, kisa kulinda maslahi ya mwenyekiti, naona aibu kuwa KIJANA wa kitanzania mpenda democrasia ya kweli asubuhi ya leo.
 
Kumbe Machali ndiye kamuuza Kafulila. Amekiri wazi kwamba walipanga njama za kumng'oa Mbatia kwenye nafasi ya uenyekiti wakiwa nyumbani kwa Kafulila Mbezi beach.

Hawa watoto wa Kigoma wanamalizana wenyewe kwa wenyewe. Machali anafurahia kuchukua mikoba ya Kafulila (Katibu Mwenezi). Huyu Machali hawezi kuaminika tena kwa unafiki wake!
 
yote kwa yote lazima tuwe na taifa la watu wenye nidhamu, na tuheshimu vyombo husika vinapofanya maamuzi
 
Further actions to IMPLEMENT THE DECISIONS. Sidhani kama inahitaji phd ya sheria kuielewa. Anyway mimi sina a b c za sheria, i stand to be educated


Hata mimi nimeshangaa uelewa wa hawa jamaa wa NCCR Mageuzi kuhusu hii order ya mahakama. Sheria imewatupa mkono hawa.
 
Star TV, ninyi makosa aliyohukumiwa nayo Kafulila mnayafahamu, mmefuatilia kutoka katika nyaraka za NCCR kujua ni yapi hasa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom