Kulikuwa na faida gani ya baadhi ya waafrika wenzetu kupigania uhuru wakati kila kitu tunapata wazungu?

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
INAWEZEKANA labda mimi upeo wangu ni mdogo ila nilikuwa nataka kufahamu ivi kulikuwa kuna faida gani ya baadhi ya waafrica wenzetu kupigania uhuru wakati kila kitu tulikuwa tunapata toka kwa wazungu.

kama elimu ilikuwa ni bure, hospitali watu walikuwa wanatibiwa bure lakini pia bila kusahau wazungu walitujengea shule za msingi na secondari ambazo wamesoma viongozi wengi,wamejenga reli, ofisi za serikali zilizopo hivi sasa nyingi zilijegwa na wao .........

lakini twende mbele turudi nyuma kama haya yote walikiwa wanatufanyia wazungu ivi kulikuwa na haja waafrica wengi kupigania uhuru na huu uhuru walikuwa wanaupigania kwa maslahi ya nani kama kila kitu tulikuwa tunakipata na maendeleo yalikuwa yanapatikanaaa
 
uhuru ukizidi sana unakuwa utumwa.
tuchukulie mfano mdogo tu kwenye familia yako mletabuzi.
itokee jemba nyingine inakuamria kila kitu kwenye gamiliam yako ikiwemo kutimiza mahitaji ya mkeo na watoto wako. bado utajiita ni baba wa familia.
 
jamaa sithani kama alisoma title
 
INAWEZEKANA labda mimi upeo wangu ni mdogo ila nilikuwa nataka kufahamu ivi kulikuwa kuna faida gani ya baadhi ya waafrica wenzetu kupigania uhuru wakati kila kitu tulikuwa tunapata toka kwa wazungu.

kama elimu ilikuwa ni bure, hospitali watu walikuwa wanatibiwa bure lakini pia bila kusahau wazungu walitujengea shule za msingi na secondari ambazo wamesoma viongozi wengi,wamejenga reli, ofisi za serikali zilizopo hivi sasa nyingi zilijegwa na wao .........

lakini twende mbele turudi nyuma kama haya yote walikiwa wanatufanyia wazungu ivi kulikuwa na haja waafrica wengi kupigania uhuru na huu uhuru walikuwa wanaupigania kwa maslahi ya nani kama kila kitu tulikuwa tunakipata na maendeleo yalikuwa yanapatikanaaa
Ha ha ha!Tulikosea sana kuwaondoa wakoloni kama Walibya walivyokosea kwa Col. Gaddafi.
 
Duh! Hivi bado kuna watu wanautamani ukoloni? Inasikitisha Sana, ila sababu ni serikali za nchi huru hasa Africa kushindwa kuendeleza raia wao na nchi zao baada ya ukoloni kuondoka ila bado si sababu ya kuudharau uhuru uliopiganiwa kwa jasho na damu na kuuthamini ukoloni ambao hata wengi wetu tumeufahamu kupitia vitabu na hadithi tu.
 
Wapo wanao utaman ukolon coz ukiangalia mambo yanayofanywa na viongoz Wa kiafrika ni afadhali mkolon angeendelea kututawala uchu Wa madaraka vimetawala miongon mwao hakuna wanachofanya zaidi ya kujinufaisha Wao na kunenepeana matumbo
 
Waliamua tu kuondoka maana mkiambiwa piteni kushoto mnapita kulia
Mna macho hamuoni na mna masikio lakini hamsikii
Eti ukombozi
Sema waliamua kuondoka tu na waliobaki kama South Africa ni wafanyabiashara tu
Ingawa wengi wamekimbia pia

Hii picha ni Tanga 1917
tapatalk_1555832426655.jpg
 
waliopigania uhuru...walikuwa wanatuzuga....tu kwa kifupi wakoloni wenyewe walitutengenezea mapinduzi...baadhi ya mababu waliokuwa na ushawishi wakapewa mbinu....na wakoloni wenyewe ili ionekane wamepambana kuwaondoa...lakini ni kama wakoloni walijiteka wenyewe...sasa kuna ukoloni mambo leo ambao ni wa hatari kuliko ukoloni wenyewe unaojulikana...tunatawaliwa, wanatupangia....na wakoloni wapo hadi leo
 
INAWEZEKANA labda mimi upeo wangu ni mdogo ila nilikuwa nataka kufahamu ivi kulikuwa kuna faida gani ya baadhi ya waafrica wenzetu kupigania uhuru wakati kila kitu tulikuwa tunapata toka kwa wazungu.

kama elimu ilikuwa ni bure, hospitali watu walikuwa wanatibiwa bure lakini pia bila kusahau wazungu walitujengea shule za msingi na secondari ambazo wamesoma viongozi wengi,wamejenga reli, ofisi za serikali zilizopo hivi sasa nyingi zilijegwa na wao .........

lakini twende mbele turudi nyuma kama haya yote walikiwa wanatufanyia wazungu ivi kulikuwa na haja waafrica wengi kupigania uhuru na huu uhuru walikuwa wanaupigania kwa maslahi ya nani kama kila kitu tulikuwa tunakipata na maendeleo yalikuwa yanapatikanaaa
Ilo swali hata Mimi najiuliza Sana
 
Ndo maana kuna kisiwa cha Mayotte wao walikataa huo uhuru wa Waafrica. Bali wakaamua kuendelea kua chini ya Mfaransa, na ni kisiwa pekee Comoro chenye maendeleo makubwa kabisa kama ufaransa
Yes ni kweli mkuu, cha ajabu wanaume wa comorro wanakwenda Mayotte ili kuoa wanawake wapate uraia wa Mayotte na kuwa raia WA ufaransa , hata re union wao bado ni sehemu ya france
 
Back
Top Bottom