Kulikua Na Ulazima Makame awe Kama Kivuitu???

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,191
:thinking: Kulikua na Ulazima Gani Makame Vyatu vya Kivuitu??

Nilivyodhania ni kwamba mtu yeyote katika ngazi ya Ujaji, hata kama kastaafu, ni rafiki mkubwa dhahabu inayoitwa HAKI. Na kwamba pindi anapofuzu katika hilo ndipo anapopewa cheo stahiki cha kuitwa RAFIKI WA MAHAKAMA. Na kwamba yale yote yaliokinyume na hapo pia ni ukweli mtupu.

Wizi wowote ule una madhara makubwa ya kumpokonya mwenye haki ama mali yake au uhai wake na wakati mwingine zote kwa pamoja. Sasa, tukichukua sura halisi ya mambo yalivyotokea kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2010, ni kama vile Watanzania wote TUMEFIWA NA MWANA WA PEKEE 'DEMOKRASIA' aliondolewa haki ya kuishi katika meza ya kikundi kidogo cha 'Watu wenye Ustahili zaidi na Taifa letu', mtu ukitulia ndani mwako wakati mwingine ukiyakumbuka UNAJIHISI WENZETU HAWA WALITUONA SOTE NI MARUHANI tu - mambo yatatokea tu kama miaka mingine na kupita salama hivi hivi. Lakini, walisahau kwamba siku zote ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu!!!

Mtu pindi unapoanza kutekeleza au kusaidia kutekelezwa kwa WIZI wa KURA ni sharti usiishie tu katika kutazama ASALI zitakazotokana na zoezi lako hilo. Muhimu zaidi, na hasa katika uchaguzi wenye mgombea wa upinzani anayependwa, inakua ni busara kuangalia kwanza MADHARA yanayoweza kutokea baada ya yote kwa taifa lako kuliko kukirimu yule asiependeka kupata mabawa asiyoyastahili kuwahi TAJI na NISHANI ya mwenzake. Katika hali kama hii kuna mawili; ama WANAICHI KUANZA KUDAI KILICHO CHA HAKI na mwenye kukimbilia kiti kupitia mlango wa nyuma, kwa udhaifu asilia ya binadamu yeyote yule, atajibu kwa kuwafundisha somo kupitia NGUVU ya DOLA. Na hapo ndipo MLANGO WA JEHANAAM unapofunguliwa bila aibu kwa kila upande kutetea kinachonekana kwa na tafsiri yao kuwa ndio HAKI halisi. Matokeo yake ni mauaji ya kutisha hasa kwa akina mama na wato na mali kibao kuteketezwa kati chumi dhaifu kama hizi za kwetu. Ni MACHAFUKO MTINDO MMOJA hata katika taifa lisilofahamu DAMU kama Tanzania. Hili, mwanasheria yeyote mahiri haitaji kuwa shahada ya chuo kikuu kulitambu, maslahi madogo madogo yakiwekwa pembeni.

Kila ninapofikiria Uchaguzi Mkuu 2010 nywele hunisimama na damu kuwasha, Mungu saidi!!! Mpaka hapa, kwenye mjadala mzito kati ya akili yangu, roho na mwili; na kwa upole zaidi najiuliza: Je, kulikua na ulazima wowote Kwa Jaji Mstaafu MAKAME kumranda KIVUITU wa wa Kenya 2007??? Kama jibu ni ndio, je huenda alikumbana na hali kama zile zile alizokuja kuzikiri baadaye huyo fanania yake - kulazimishwa kutangaza alichopew??? Na kama jibu ni hapa, je kuna uwezekano wowote JF ikatuanikia taarifa za mwenendo ya Akaunti za Fedha za Makamishna wote wa Uchaguzi katika kipindi cha miaka mitano tangu uchaguzi wa 2005 umalizike??

Mbali na hapo, kwa mtaji huu wa MAKAME kudhihirishia ulimwengu kwama licha ya kuwahi kuwa mwanasheria mwenye ngazi ya Ujaji vile vile anaweza kabisa kubadilika akili na KULIPIGA KABALI 'HAKI YA UMMA' kwa sentensi moja tu kwenye vyombo vya habari, nadha pia ingekua VEMA zaidi kwetu kutilia shaka MAAMUZI alizowahi kutoa mahakamani. Lengo ni kupata TAARIFA MUHIMU itakayoelekeza fikra za taaluma ya wanasheria kunapojitokeza mazingira kama haya tulionayo leo hii. Tume ilipewa haki ya kusikilizwa na vyombo vya habari mbele ya jamii na wakakiri (japo kwa sauti nyembamba) hayo tunayoyafahamu kuhusu uchaguzi wetu. Waangalizi wa kimataifa kutoka EU (Taasisi ya kuaminika) ndio ikamalizia kabisa MISUMARI YA MOTO ambayo Jumuiya ya Kimataifa itaanza kuyafanyia kazi kwa nguvu ya ajabu sio kipindi kirefu.

Je, kwa msiba huu mkubwa ulioghubika taifa letu kwa kuondokewa na mpendwa wao DEMOKRASIA, ambaye amesumbuliwa sana na maradhi mengi tangu mtunzaji mwaminifu Mwalimu Nyerere kutangulia mbele ya haki (Roho yake ipumzike Kwa Amani na Apate Pumziko ya Milele), wahusika walifikiri kwa kwa kutumia Uwezo wa Akili au Maelekezo ya Mitumbo yao????????????????????????????

Nadha THREAD hii haitopatwa kifo cha ghafla chini ya umri wa siku tatu kama ilivyoonekana kwa threads nyinginezo za hapo awali.
 
Back
Top Bottom