Kulikonj Msafara wa Kampeni ya JK kuandamana na Ambulance!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kulikonj Msafara wa Kampeni ya JK kuandamana na Ambulance!!!!!!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Bill, Aug 25, 2010.

 1. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,163
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Katika kile kinachoonekana ni kujipanga dhidi ya uwezekano wowote wa kuugua ghafla au kupata ajali kwa viongozi au makada wake, msafara wa kampeni za mgombea huyo umekuwa ukiongozana na magari maalum ya kubebea wagonjwa mahututi (ambulance).

  Mbali na kuanguka jukwaani jijini Dar es Salaam, baadhi ya watu waliohudhuria mkutano wake wa kampeni katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na waliofuatilia mkutano huo kupitia kituo cha televisheni cha ‘Star Tv', walisema bado Rais Kikwete alionekana mdhoofu na aliyepoteza uchangamfu wake wa kawaida licha ya kujitahidi kuhutubia bila kufikwa na msukosuko mwingine wa kiafya.

  Kumbukumbu zinaonyesha kuwa msukosuko wa kiafya wa Jumamosi ni wa nne kumfika hadharani Rais Kikwete.

  Akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Kikwete aliwahi kuzidiwa ghafla mwaka 1997 katika uwanja wa ndege wa Brussels nchini Ubelgiji akiwa njiani kuelekea nchini Cuba hali iliyosababisha alazwe kwa saa kadhaa kabla ya kuruhusiwa kuendelea na safari.

  Mwaka 2005 siku moja kabla ya uchaguzi mkuu, alizidiwa ghafla na kuanguka jukwaani katika viwanja hivyo hivyo vya Jangwani.

  Baada ya kupata matibabu ya awali, alizungumza na vyombo vya habari nyumbani kwake na kuwaeleza kuwa kilichomfanya aanguke ni uchovu wa kampeni na hasa kwa kuwa siku hiyo alikuwa amefunga.

  Akihutubia umati wa waumini wa Kanisa la Africa Inland (AIC) jijini Mwanza Oktoba 4 mwaka jana, Rais Kikwete aliishiwa nguvu hali iliyomlazimu daktari wake, Peter Mfisi, kutoa ufafanuzi kwa vyombo vya habari kwa kusema Rais Kikwete alikuwa hana tatizo lolote la kiafya ila aliishiwa nguvu kwa uchovu.

  ".......uchaguzi ule alidondoka kwa sababu ya uchovu sasa kuanguka hivi jamani kunashtusha maana safari hii ndio alikuwa anazindua hizo kampeni kwa hiyo suala la uchovu hapo halipo. Kuna kitu wanatuficha......wanajua wenyewe, ndio mambo ya wakubwa hayo lakini tutakuja kujua tu, dunia haina siri bwana, lakini namtakia afya njema", alisema mwanaharakati mmoja kwa sharti la kutotajwa jina lake.

  Hata hivyo, alipoulizwa na mhariri wa chombo kimoja cha habari kuwa chama hicho kimejipangaaje kumpunguzia uchovu Rais Kikwete katika kampeni za mwaka huu, Kinana alisema watatumia usafiri wa helikopta kumnadi mgombea huyo ili kumpunguzia umbali mrefu wa kusafiri kwa njia ya barabara.
  Mbali ya kupunguziwa umbali wa kusafiri kwa njia ya barabara, Kikwete atapata muda wa kupumzika wa siku 16 katika kipindi chote cha siku 68 za kampeni na hivyo kumfanya kuwa katika mchakato huo kwa siku 52.

  Uamuzi huo utamwezesha mgombea huyo wa urais wa CCM kupunguza umbali wa kusafiri kwa njia ya barabara kwa urefu wa kilomita 58,000 ikilinganishwa na ilivyokuwa mwaka 2005. Kumbukumbu zinaonyesha kuwa wakati wa kampeni za mwaka 2005 Kikwete alisafiri kwa njia ya barabara umbali wa kilomota 96,000. Alisema katika kampeni za mwaka huu mgombea huyo atasafiri kwa njia ya barabara kwa umbali wa kilomita 38,000 tu.

  Ili kuhakikisha Rais Kikwete anapata muda mrefu wa kumpumzika na kumpunguzia uchovu, CCM imepunguza muda wa kuzungumza kwa mgombea huyo katika mikutano yake ya kampeni. Hali hiyo imeonekana mjini Mwanza na maeneo mengine alikopita ambako alitumia muda usiozidi dakika 30 kuomba kura kwa wananchi.
  [​IMG]Ambulance ya Hospitali ya Rufaa Bugando ikiwa kwenye msafara wa mgombea wa CCM, Rais Jakaya Kikwete. Sina uhakika kama imelipiwa na chama au itakuwa inasaidia misafara ya wagombea wa vyama vyote.Picha na Katulanda


  SOURCE: Tanzania Daima - 25/08/2010

  Mytake: JK kapunguziwa uchovu kwa kupewa usafiri wa anga na kupunguziwa muda wa kuhutubia, mbona ambulance tena? Si JK kaacha kufunga ambalo ndio ilikuwa kiini cha kuishiwa nguvu/sukari! Mbona ambulance tena na kupunguziwa muda wa kuhutubia???? Yangu masikio na Macho.....
   
 2. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,731
  Trophy Points: 280
  Mungu ameingilia kati kuwasaidia watanzania kufikiri sawasawa. Haihitaji tena Dr. Slaa awaambie kuwa JK ni mgonjwa hivyo hastahili kupewa nafasi ya kuwa rais.Kila kitu kiko wazi, na dunia itawashangaa watanzania kuacha mtu mzima na kwenda kuchagua mgonjwa kuwa rais, itaonekana Tanzania ni taifa la wagonjwa, ASANTE MUNGU MUUMBA WA MBINGU NA NCHI KWA MAFUNUO HAYA.
   
 3. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,163
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Nadhani si kuambatana na Madaktari tu, pia hata kupata tiba ya uhakika nje ya nchi kwa hela zetu walipa kodi japo siyo lazima kujua anachoumwa Mheshimiwa.
   
 4. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kwa mtaji huu wa kuwanguka anguka ghafla itabidi wabuni njia nyingine ya kuhutubia mkutano achukue mfano wa kakobe akiwa safarini video zake zinatumika, ushauri wa bure kwa CCM tumieni mikanda ya video ili kunusuru mgombea wenu asianguke tena jukwaani kuepusha minongono ya wananchi:eyeroll2:
   
 5. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mkuu wamesema haumwi bali ni uchovu wa kufunga sasa kwanini atumie pesa zetu kwenda nje ya nchi kuchekiwa, Muhimbili,Regency,Lugalo, Aga Khan na kwingineko wale madaktari bingwa hawawezi kumcheki hali yake ya uchovu hadi nje!!!!
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Aug 25, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kwanini kuna na ambulance na waganga wa jadi wakiwa ndani ya magwanda ya CCM?
   
 7. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Binadamu kazi kwelikweli!
   
 8. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #8
  Aug 25, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,163
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Mkuu Born Town umenena...., uchovu na ambulance wapi na wapi?? Yangu macho mwaka huu.
   
 9. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #9
  Aug 25, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,528
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. J. M Kikwete akiwa amejiegamiza ktk jukwaa(kushoto) huku akimsikiliza mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM Jasson Rweikiza(Jimbo la Bukoba Vijijini).
   
 10. Bourgeoisie

  Bourgeoisie JF-Expert Member

  #10
  Aug 25, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 611
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Mh! Makubwa mwaka huu! Uchovu pia unalindwa na ambulance.
   
 11. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #11
  Aug 25, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli Mkuu hizi ambulance ni muhimu sana kwa Rais Jk na mkewe kwa ajili ya matatizo yao ya kuzimia-zimia
   
 12. A

  ALIBAALIO Member

  #12
  Aug 25, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nami sioni ubaya wa ambulance kuwa stand by kwenye sehemu ya adhara kama hiyo.kumbuka hata kwenye shughuli za michezo ambulance zinakuwepo.tatizo hapa hatujazoea vitu kama hivi lakini ni utaratibu unaokubalika kama unavyoona magari ya fire yanapaki stand by kama mlimani city
   
 13. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #13
  Aug 26, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Nilazima kuwe na ambulance well equiped with aid kit, rais wa china alipokuja tz alikuja nazn 2,moja ilikuwa for vip. Sisi hatukuwa na utaratibu huo kwa kuwa kabla ya msafara tunamualika sheikh yahya na mch lwakatare:changanya na zako.
   
Loading...