Kulikoni ?????


Boramaisha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Messages
820
Likes
2
Points
0

Boramaisha

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2009
820 2 0
Ukitafakari kidogo juu ya matokeo ya kura hasa Tanzania Bara ambako kuna mchanganyiko wa karibu nusu kwa nusu wa dini mbili kubwa, utagundua matokeo hayo kwa wagombea urais kwa tiketi ya CCM na CUF hasa Tanzania Bara yana ka-element ka udini. Mgombea wa CUF amepata kura nyingi ukanda wa mwambao wa Pwani ya Tanzania kwa sababu wananchi wengi wa maeneo hayo ni wa dini anayotoka mgombea huyo. Huko mikoani pia sehemu ambazo zina idadi kubwa ya wapiga kura wa dini hiyo idadi ya kura za mgombea huyo zilikuwa juu. Kwa maana hiyo basi, shutuma za 'udini' uliokuwa umevaliwa njuga viongozi wa juu kwa kulenga dini ambayo viongozi wake wanavaa 'majoho' hazikuwa na mantiki yoyote. Isitoshe, baadhi ya viongozi wa dini wasiovaa 'majoho' bali kanzu ndio waliokuwa wakitawatamkia wazi waumini wao kwa kutaja jina wachague kiongozi wa dini yao kwa kuwa ni mwenzao! Wavaa majoho hawakuwahi kutaja jina la mgombea yeyote bali kutaja sifa zinazopaswa kuangaliwa ili kuweza kupata kiongozi bora. Kama waumini wa wavaa majoho wangelikuwa na udini na kuuonyesha kwenye sanduku la kura isingeliwezekana Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM kupata kura nyingi alizopata. Kura alizopata ni mchanganyiko wa kura za waumini wa wavaa majoho pamoja na wale wa wavaa kanzu!
 

Forum statistics

Threads 1,204,898
Members 457,584
Posts 28,175,030