Kulikoni waziri chiza na ufukuzwaji kiholela wa wafanyakazi bodi ya kahawa raisi wetu tusaidie

John Kisii

Member
Nov 27, 2013
7
0
Kulikoni waziri chiza na ufukuzwaji kiholela wa wafanyakazi bodi ya kahawa raisi wetu tusaidie

Leo wametimia wafanya kazi kama sikosei ni sita wamefukuzwa kazi na mkurugenzi mkuu Bw Adolph Kumburu
Taarifa tulizozipata hivi punde ni kwamba kwa kipindi cha wiki mbili wafanyakazi 2 wa bodi hii wamefukuzwa kazi kwa kile kijulikanacho kuwa chuki binafsi za mkuu huyo

Mfanyakazi mmoja ambae alipewa barua ya onyo wiki mbili zilizopita na hapohapo kufunguliwa mashitaka mapya yakiwa ni yaleyale aliyoundiwa na kupewa onyo kali leo amefukuzwa nayo kazi.

Taarifa za ndani zinasema mkurugenzi huyo amesikika akitamba kuwa waziri Chiza ndie akiyempa ruhusa ya kuwafukuza kazi kienyeji wafanyakazi wa bodi hiyo bila kujali misingi na taratibu za sheria ya kazi na mahusiano kazini.

Bw Kumburu akiwa ameshamaliza mkataba wake tokea September 30 mwaka huu bado anaendelea na kazi huku mkataba wake ukiwa haujulikani uko vipi

Jumla ya kesi zilizoko mahakamani tangu alipoiingia kuendesha shirika hilo ni nyingi achilia mbali zile za wafanyakazi ikiwa ni pamoja na zile za wafanyabiashara wa kahawa na wasafirishaji EXPORTERS pamoja na wakulima wa zao hilo
Mara kwa mara huwa anasikika akisema hata kama waliokimbilia mahakamani wakishinda kesi yeye atakuwa ameshaondoka
Hawa ndio aina ya viongozi tuliona Tanzania kwa hivi sasa.

Huku waziri mwenye dhamana akiwa kafunga macho kinachojionyesha ni jinsi gani waziri huyo anavyoachia serikali kuja kupata hasara kubwa kwa kuwalipa wale watakaoshinda kesi zao mahakamani ambazo ni kiasilimia ni kuwa bodi hiyo lazima ishindwe.

Mkurugenzi huyo Bw Kumburu haijaeleweka vizuri amepewa kibali na nani cha kuharck email za watu na pia kusikiliza na kurekodi simu za watu.

Hivi karibu nitaweka hapa jamvini barua na sababu za kufukuzwa kwa wafanyakazi hao wote kwa wale wanaojua sheria watusaidie zaidi kuona nchi yetu inakoelekea.
Taarifa za ndani zinasema kuwa hivi kuanzia wiki ijayo kuna wafanyakazi wawili ambao ndio anaanzana nao ambao ni Mwanasheria wa bodi hiyo kwa kueleza ukweli na Afisa mwajiri na utawala wa shirika hilo

Raisi wetu mpendwa tunakuomba kuingilia kati hili swala la uonevu unaondelea kwenye bodi hii na pia usisikilize upande mmoja tunakuomba usikilize pande zote mbili kwa kuwa upande mmoja yaani waziri Mwenyekiti na mkurugenzi mkuu ni waongo sana hawatakueleza ukweli.
 

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,111
2,000
Na wewe usipoangalia utafukuzwa, ni lazime mjifunze kuheshimu Authorities, kama mna hoja kinzani, ni lazime mtumie busara zilizomo kwenye policies za bord katika kuwasilisha hoja zenu, Authorities zote zimewekwa na Mungu.

Majuzi alikuja hapa mwenzako na tuhuma lukuki dhidi ya viongozi wa hiyo bodi, likely na yeye kawa terminated, na kama hawajamterminate watakuwa wanamatatizo makubwa sana.

kwa sasa, hao waliofukuzwa waende kupata msaada wa kisheria mahakamani, meanwhile, bodi sasa sasa itaweza kufanya kazi zake kwa amani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom