Kulikoni wasanii wa Tz!

Spear_

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
1,603
486
Habari Wana Jf,

Hivi wasanii wa Tz wanajua kuwa muziki au uigizaji ni kazi kama nyinge na inatakiwa kuheshimiwa? mbona wanajishusha bei kiasi hicho? mfano ni msanii Diamond ambaye alikuwa aje Arusha kufanya shoo kwa malipo ya sh.2.5 mil, baada ya kuingia mitini wakurugenzi wanasema wamepata hasara kwani mashabiki takribani 2000 walianza kuleta fujo wakitaka kurudishiwa fedha zao za kiingilio ambapo kila mtu aliingia kwa 10,000!! ukiangalia hapa waandaaji walipata 20,000,000 lakini msanii walikubaliana kumlipa 2.5mil maana yake ni nini??? hivi wasanii wa tz wanaangalia mbele?? wanajua thamani yao??? imenuma sana japo jamaa aliingia mitini na 1.5mil!! kitu ambacho pia sio kizuri ila kwa leo sizungumzii hilo!!

wakuu hebu tujadili, hivi hawa wasanii wanajua thamani yao?

source: Issa Michuzi
 
Sioni kwa nini wasanii walaumiwe kwa hili. Tuangalie ukweli ulivyo...........Mtayarishaji amesema amepata 20,000,000. Diamond kapewa 2.5milioni, kiasi cha 10%, unasema msanii kaibiwa , je unazijua gharama za matayarishaji? Unajua makubaliano yalikuwa yepi? nani aligharamia, malazi, usafiri, chakula, kukodi ukumbi, kukodi vyombo, matangazo ............biashara hii ndivyo inavyofanyika duniani kote. Hivi katika ajira uliyonayo mwenyewe unagawana kwa pasenti ngapi na mwajiri wako?
 
Hapo kwenye RED sijaelewa nini hoja yako, maana unaonesha
kuwatetea wasanii lakini baadaye unawaponda!! Mimi nadhaani
tatizo ni shule kwa kuwa wengi hawajui hata athari ya mikataba
wanayoingia, wanaposaini huangalia kiasi cha pesa tu bila kusoma
vifungu kwenye mikataba yao, wanapokuja kugundua (baada ya
kushtuliwa) ukweli ndo wanaanza kulalamika kuibiwa...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom