Kulikoni vifurushi vya TTCL kumalizika kabla ya muda?

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,681
1,698
Wakuu tarehe 12/03 nilijiunga na kifurushi cha sh 5,000/= kama kawaida yangu takriban miaka mitatu au minne hivi.

Na kila nikijiunga hupata ujumbe huu "Ndugu mteja, Umefanikiwa kuunganisha huduma yako ya Watumishi Pack Plus 2GB-100min-AllNetworks-100sms Monthly. Piga *148*30# kwa huduma zaidi".

Tarehe 19/03 nikapokea ujumbe huu "Ndugu mteja, umeshatumia asilimia 75 ya dakika zako za mwezi. Piga *148*30# kwa huduma zaidi." Ujumbe huu haukunisitua kwani ni mara nyingi huupokea na kuendelea na matumizi mpaka mwezi unaisha.

Jana asubuhi, tarehe 22/03 nikataka kupiga cm nikaambiwa salio limeisha bila hata kutumiwa ujumbe. Kawaida hupokea ujumbe wa kunijulisha muda wa kifurushi kuisha.

Nikawasiliana nao na kuambiwa 2GB ya dakika 100 nimeimaliza. Nikamwambia mbona si kawaida yangu au pana mabadiko gharama ya vifurushi hapo?

Sijajibiwa mpaka sasa.
 
Umejibiwa umemaliza unaonekana uliandaa majibu yako maana yake ulitaka wakujibu kama wewe ulivyokuwa unafikiri kichwani kwako.
 
Panda tukupandishe, acha kulialia vitu vidogo namna hii…. 2GB wiki nzima unashangaa nini zikiisha?
 
Panda tukupandishe, acha kulialia vitu vidogo namna hii…. 2GB wiki nzima unashangaa nini zikiisha?
Sikatai kuisha ila sina kawaida ya kuzungumza kwa zaidi ya dakika mbili kwa wakati mmoja kwa siku, sembuse dakika 10 kwa siku kwa hizo siku 10!
 
Back
Top Bottom