Kulikoni utitiri wa shule za Chekechea Arusha mjini zisizokidhi vigezo? Mamlaka zitazame hili haraka sana

Emaoi

JF-Expert Member
Mar 9, 2013
285
250
Wakuu naombeni msaada kuhusu hii wizara ya elimu. Kuna mambo naona hayaendi sawasawa kuhusu hizi shule za chekechea/nursery.

Mimi sio mwenyeji sana nimehamia Arusha majuzi tu nikabahatika kupita maeneo ya Sanawari kuanzia Sanawari ya chini mpaka ya juu nimekuta shule za chekechea ni nyingi mno kila kona kwenye nyumba za kupanga mitaani wengine wameweka matangazo na wengine wameandika tuition na ukiangalia ni watoto wadogo ambao hawajaanza hata shule ndio wanapelekwa kwenye maeneo hayo.

Cha kusikitisha ni kwamba kipindi hiki kigumu cha Corona unakuta watoto wamerundikana kwenye chumba kimoja hakuna choo cha watoto, hakuna Maji ya kunawa mikono kwenye ndoo , hakuna ulinzi kwa watoto wanazagaa mitaani wakipita uchochoroni wazazi hawajui hata kama kuna tatizo la watoto kubakwa au kuibiwa.

Na ukifika kabisa Sanawari ya juu ndio balaa kila kona ni chekechea ukiangalia mazingira hayafai kabisa sio mazingira Rafiki kwa watoto.

Tunaomba uongozi wa Arusha DC watupe muongozo kwamba hizi chekechea na Tuition mitaani na kwenye nyumba za kupanga zimesajiliwa na nani? Au nani Muhusika aliyeruhusu hizi huduma mbovu mitaani?

Watoto wanapata shida mno wengine wakiachiwa tu wanabaki kuzurura barabarani huku wakicheza mipira kwenye maeneo hatarishi

Arusha DC upande wa Elimu tunaomba kujua ni vigezo gani mnatumia kuruhusu hizi chekechea Bubu na tuition mitaani?

Wizara ya elimu na nyie tupeni ufafanuzi kuhusu hizi shule za awali mitaani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom