Kulikoni utawala wa JK; Msafara Kupigwa Mawe, Mei Mosi Kutoalikwa, Hotuba Kususiwa?

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,856
398
Wandugu,
Nimekuwa nikitafakari vimbwanga vilivyotokea hapa nchini vilivyoweka rekodi ya aina yake tangu nchi yetu ipate uhuru. Najua vipo vingi, lakini nitachokoza kwa kuanza na hivi vitatu.

1. Wananchi kupopolea mawe msafara wa jk wakati wa ziara yake mkoani mbeya. Hili lilikuwa ni tukio la kihistoria tangu tupate uhuru.

2. Wakati wa sherehe za Mei Mosi 2010 kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu muungano wa vyama vya wafanyakazi haukualika serikali kushiriki kwenye sherehe, tofauti na ilivyozoeleka tangu tupate uhuru na sherehe zilihitimishwa bila hotuba za viongozi wa serikali akiwemo jk mwenyewe.

3. Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu wabunge wasiopungua 40 wanatoka nje ya ukumbi wa bunge ikiwa ni ishara ya kususia hotuba yake.

4. .......


Wenye matukio mengine ya kihistoria tafadhali waendeleze orodha hiyo.

NINACHOJIULIZA
ccm inayayaona hayo kuwa ni ya kawaida?
 

Mahesabu

JF-Expert Member
Jan 27, 2008
5,515
1,762
kwa mara ya kwanza duniani nchi pekee ambayo ndani ya miaka 15.... chaguzi 3 kuu chama cha mapinduzi kinaongoza matokeo ya urais na ubunge
 

Henge

JF-Expert Member
May 14, 2009
6,933
1,509
kwa mara ya kwanza duniani nchi pekee ambayo ndani ya miaka 15.... chaguzi 3 kuu chama cha mapinduzi kinaongoza matokeo ya urais na ubunge
na kudhiiilisha upeo wetu ulivyomdogo! Elimu watu hawana!
 

seniorita

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
674
53
Kwa mara ya kwanza tumekaribia kuwa the poorest country in the world, we are number 148/169. while our country is rich in resources. Think about it, and how it will be in 2015, I am sure tutaweka guiness record of being the poorest in the whole world!!! And of course, one of the top corrupt countries, inawezekana tukawatangulia Nigeria!!!!!
 

Liz Senior

JF-Expert Member
Apr 19, 2007
483
52
na sasa msafara wake unajumuisha Ambulance ya Knight Support! Kwani kuna nini? Jana alipita mida ya saa moja hivi msafara mrefu sana na Ambulance imo! Au ndio kule kuanguka?
 

jcb

JF-Expert Member
Jul 6, 2010
280
66
Mara ya kwanza kwa matokeo ya Raisi wa Jamhuri ya Tanzania kukataliwa
 

blackpepper

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
381
14
kukimbia mdahalo na mgombea mwenzake wa urais...na kuwakataza wagombea wa chama chake (yeyekama Mwenyekiti)kushiriki midahalo
 

Leornado

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,533
191
Askari wa kike kuuwawa kwa risasi kwa kuupoteza msafara wa raisi Tarime???, RIP PC .....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom