Tumeaminishwa na Serikali kuwa mgonjwa anatakiwa kwenda hospitali za umma na atapata matibabu bure. Leo nimeenda Kituo cha Afya ya Buzuruga kumwona mgonjwa wangu sikuamini macho yangu nilipoambiwa kanunue gloves, kanunue pamba, kanununue dawa ya kusafisha jeraha nk.
Hivi Mtanzania wa kawaida ataweza gharama hizi? Mawaziri kwenye bajeti wanapokuwa na mbwembwe eti mwaka huu bajeti ya Afya ni billioni 250 kutoka billioni 35 ya mwaka 2015. kumbe wanatudanganya.
Afadhali hata wakati wa Kikwete tulikuwa tunapata dawa bure hata kwa taabu hivyo. Pili, kwa kweli watumishi hawajitumi. Mganga anawaacha wagonjwa wamekaa anaenda kutembea kwa muda wa dakika 45 ndipo anarudi?
Hospitali za Tanzania bado sana. Mawaziri acheni mbwembwe zisizo na maana.