Kulikoni Steve Nyerere, Wema Sepetu na Mama Wema?

H M HAY

Member
May 18, 2015
32
19
Naanza kwa kusema Nguvu ya siasa inaweza kubadili maisha na mitazamo ya watu katika taifa lolote lile ulimwenguni. Kwa hapa kwetu Tanzania siasa imekuwa ikichukuliwa kama mchezo wa kuigiza (SANAA) na hivyo kuipunguzia hadhi na heshima yake inayostahili!!

Ndiyo,hivyo ndivyo ilivyo kwa sababu hakuna chama chochote cha siasa katika Tanzania ambacho kinatambua heshima na thamani ya SIASA katika nchi. Na ndiyo maana kuna wachambuzi wa mambo ya siasa waliwahi kusema kuwa siasa za Tanzania ni siasa za maji taka! Sitaki kuzungumzia ushindani hewa uliopo kati CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) na vyama vinavyounda UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI (UKAWA) ikiongozwa na CHADEMA kwa kile ninachokiamini kuwa ni kama mchezo wa kuigiza tu. Ukitaka kuliamini hili angalia sababu zinazomfanya mtu kuhama kutoka chama kimoja cha siasa kwenda kingine,si sababu za kisiasa hata kidogo bali ni sababu ambazo unaweza ukaziita ni za kiushabiki zisizokuwa na tija wala mashiko ama kwa chama anachohamia au kwa mtu husika (mwanachama). Hapa unaweza kusema ni afadhali hata yule anayeishabikia simba au yanga bila ya hata kujua jina la hata mchezaji mmoja katika timu anayoishabikia!!! Usicheke,ndivyo ilivyo

Sikatai ushabiki ila ni vema ukashabikia jambo ambalo unalielewa vizuri ili ushabiki wako uwe na maana zaidi. Pia ifike wakati kuwe na tofauti kati ya ushabiki wa Simba na Yanga na ushabiki wa kisiasa. Kulielewa jambo vizuri ni pamoja na kutafakari kabla ya kuchuka hatua kuhusiana na kile unachofikiria kukifanya. Kwa upande mwingine siasa za Tanzania na wanasiasa wake ni zile zinazoazimia zaidi kupendezesha kurasa za mbele za magazeti kwa lengo hasa la kujitafutia umaarufu na masilahi binafsi na si kwa masilahi ya Taifa na wake wake. Naam,siku chache sana zilizopita tumeshuhudia SINEMA ya kisiasa katika nchi yetu. Kumbuka kuwa neno Sinema bado linalenga neno SANAA kama nilivyobainisha hapo juu,kati ya CCM na CHADEMA. Kwa bahati nzuri sana ni kwamba SINEMA hiyo imehusisha wasanii wakubwa,wenye heshima,wenye followers wengi sana na wenye kuaminika kuwa wao ni kioo cha jamii. Hapa nataka upate picha juu ya nini uzuri au ubaya wa SINEMA hiyo kutegemeana na fikra zako na jinsi unavyowafahamu wasanii hao ambao hasa nawalenga STEVE NYERERE na WEMA SEPETU. Hakuna asiyejua ukaribu kama siyo udugu kati ya familia ya Akiana wema na Steve Nyerere,lakini leo hii wanatumia vyombo vya habari tena kwa kufanya PRESS CONFERENCE kuzungumzia mambo ambayo hayana miguu wala kichwa kwa masilahi ya Tanzania na watanzania. Inasikitisha zaidi kuona eti mtu kwa vile amehusishwa/kuhusika katika vita fulani inayoendelea sasa nchini mwetu,iwe ndiyo sababu ya mtu huyo kuhama chama kwa kile anachoamini ni mwarobaini wa tatizo alilo nalo au linalomkabili. Sina hakika mtu kama huyu anastahili kuaminiwa na watu makini ambao wana lengo la kupigania haki na kuleta ukombozi katika taifa hili tegemezi kama wenyewe wanavyojinadi!!!! Cha kushangaza mtu huyu na chama chake alichohamia cha sasa kupitia viongozi wake eti wanazunguka huku na kule kwa imani kuwa mwanachama amepata chama bora cha kukitumikmia na chama kwa upande wake kimepata mwananchama ambaye kinaamini ni mtaji katika kukiimirisha chama hasa kwa ajili ya chaguzi zijazo.

Usiamini usilolijua, nasema hivi kwa sababu inaaminika kuwa WEMA SEPETU ana followers wanaokadiriwa kufikia milioni mbili hivi ambao kwa imani ya Wema na chama chake kipya ni kwamba labda na hao WEMA'S FOLLOWERS watamfuata kipenzi chao,la hasha!!!!!! Kwa mtazamo huu ni ukweli usiopingika kuwa CHADEMA hawajui wala kukumbuka walipotoka,walipo na wanapokwenda. Kama hivi ndivyo,ni dhahiri kuwa hakuna upinzani wa kweli wa kisisasa katika nchi yetu bali kuna upinzani wa namna ya kutafuta unafuu wa maisha kwa mtu mmoja mmoja. Haya yanathibitishwa siyo tu malumbano yaliyopo sasa kati ya Steve Nyerere na Wema Sepetu lakini pia namna watu wanaoaminika katika jamii kufanya maamuzi ya kukurupuka. Ni jukumu la wewe unayesoma makala haya kuamua cha kuamini,kufanya na kuchukua hatua baada ya kutafakari kwa kina. Kwa kumalizia ni kwamba Steve Nyerere na Wema Sepetu ni binadamu kama walivyo binadamu wengine na kwamba si kila wanayoyafanya yanaweza kuwa sahihi na mfano katika jamii yetu. Pamoja na ukweli huu,nao wana nafasi ya kutafakari kwa kina hasa kuhusiana na mambo yao ya kimahusiano na si tofauti zao za kisiasa. Kwa mazingira haya sina sababu tena ya kumzungumzia mama yake Wema Sepetu kwa kile ninachokiamini kuwa nilichokiandaa nimeshawafikishia na yeye kama mama atatumika kwa kiasi kikubwa kujenga au kubomoa katika kile kinachoendelea hivi sasa. Asanteni
 
....
....wewe ni Mhanga...
 
Jamani,kwanini tunakataa kuamini kuwa kila mtu ana uhuru wakuamini anachokitaka/anachokipenda?Wema kuondoka ccm watu wameumia kiac kwamba hata kuhifadhi maumivu yao inashindikana.ss km chama chenu kina mcingizia mwanacha jambo kubwa km hilo na yy anaamini kaonewa kwann akae humo kuvumilia uonevu ? Ss mahakama ndo itasema kutokana na ushahidi.km kakosa au lah.ila ikiamuliwa kiccm mtamkomoa kwakua kawaaibisheni.unapodai wapenzi/wafuac wa Wema hatamfuata,wamekwambia hivyo hao wafuac ? Manake unaongea km we ndo Wema unayejua wafuac wako walivyo.iwe au icwe ww imekuhusu vp mpaka uongee aliyotakiwa kuongea Wema au wafuac wenyewe ? Kwann mnaishikia sana ccm ushahidi km yenyewe ndo Mungu wa nchi ? Wema yupo huru wafuac wake wapo huru,wakiona mtu wao kaonewa,watatoa uamuzi wao,kumfuata au kutomfuata.Mafua anumwa Wema,kwann upate kz ya kumezesha umma wote piritoni /au kununulia umma wote hendikachifu ? Hakika Ndo sababu Wema alisema kuna ambayo hatayasema.ss naamini mnao ongea sana juu ya uhamji wake kunamnalolijua mnashinda tu kuwa wawazi.bac tuwapeni pole tu, iko cku mtaongea hata bila kuulizwa km alivyojisemea siro anapigiwa cm na wanawake wengi !
 
Naombeni niulize! Hivi ni sahihi chama cha siasa kumkataa mwanachama? Nimeona kuna watu wanakilaumu chama kwa kumpa mtu uanachama, nimeshangaa mimi, labda mimi ndio mshamba!
Kama hana sifa na haendani na itikadi ya chama anaweza kukataliwa.
 
Jamani,kwanini tunakataa kuamini kuwa kila mtu ana uhuru wakuamini anachokitaka/anachokipenda?Wema kuondoka ccm watu wameumia kiac kwamba hata kuhifadhi maumivu yao inashindikana.ss km chama chenu kina mcingizia mwanacha jambo kubwa km hilo na yy anaamini kaonewa kwann akae humo kuvumilia uonevu ? Ss mahakama ndo itasema kutokana na ushahidi.km kakosa au lah.ila ikiamuliwa kiccm mtamkomoa kwakua kawaaibisheni.unapodai wapenzi/wafuac wa Wema hatamfuata,wamekwambia hivyo hao wafuac ? Manake unaongea km we ndo Wema unayejua wafuac wako walivyo.iwe au icwe ww imekuhusu vp mpaka uongee aliyotakiwa kuongea Wema au wafuac wenyewe ? Kwann mnaishikia sana ccm ushahidi km yenyewe ndo Mungu wa nchi ? Wema yupo huru wafuac wake wapo huru,wakiona mtu wao kaonewa,watatoa uamuzi wao,kumfuata au kutomfuata.Mafua anumwa Wema,kwann upate kz ya kumezesha umma wote piritoni /au kununulia umma wote hendikachifu ? Hakika Ndo sababu Wema alisema kuna ambayo hatayasema.ss naamini mnao ongea sana juu ya uhamji wake kunamnalolijua mnashinda tu kuwa wawazi.bac tuwapeni pole tu, iko cku mtaongea hata bila kuulizwa km alivyojisemea siro anapigiwa cm na wanawake wengi !
Labda ungerudia tena kusoma ungeelewa mtoa mada amejikita katika jambo gani hasa.
 
Kama hana sifa na haendani na itikadi ya chama anaweza kukataliwa.
Tofautisha kuwa mwanachama na kuwa kiongozi, hivi kuna vetting ya kuchunguza wanachama? Mtu mpaka anaenda kuchukua kadi si amejiridhisha na itikadi ya chama husika? Watu wanafikili kura ya professor ina count kuliko kura ya kahaba, sijawahi kuona chama kinafanya vetting,
 
Huo ni uhuru wa kutoa mawazo na ndiyo maana kila mmoja ana nafasi ya kueleza kile anachokifahamu. Wewe waumiaje kuhusu hilo? Bila shaka wewe ni mmoja kati ya wahanga wa jambo hili na ndiyo maana limekugusa kiasi umeshindwa kuvumilia na kutoa maneno kama ya mtu mlevi aliyelewa na kushindwa kujitambua!!!!!!
Hata wewe una nafasi ya kuandika kile unachokifahamu au kukiamini,cha kushangaza unakurupuka kama alivyokurukupa mshirika wako. Sishangai maana niliyategemea haya hasa kutoka kwa watu wasiojitambua kama wewe!! Sina shaka wewe ni mfuasi namba moja wa Wema Sepetu na ndiyo maana limekugusa kiasi hicho kama si mwananchama wa wale wasemao Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeees.......Poweeeeeeeeeeeeer!!!
 
Back
Top Bottom