Kulikoni stand za mkoa na daladala Dodoma?!?!?

Ubumuntu

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,316
10,782
Salaam wanaJF!!!

Sote tunafahamu kua Idodomya (Dodoma) ndio makao makuu ya nchi yetu. Mahala ambapo ndipo panapaswa kua makao makuu ya serikali.

Lakini kuna kero kubwa ambayo inashusha hadhi ya mji mkuu huu; nayo ni stand yake za mabasi makubwa yanayotoka mikoani (Dar, Mwanza, Arusha, Mbeya n.k.) na stand ya daladala, pale Jamatini. Kwakweli hali ya stand hizo ni aibu kwa mji mkuu huu. Halafu cha ajabu zaidi ni kua, katika stand zote hizo mbili, mabasi na daladala hutozwa pesa pindi wanapotumia na kutoka katika stand hizo. Sasa najiuliza hizo pesa kazi yake ni nini? Mimi nilihisi pesa hizo zingetumika kutengeneza stand hizo na kuziweka katika hadhi ya mji mkuu (halafu wanaokusanya hizo pesa na watu ambao kimtazamo wa nje, wanaonekana ni wahuni tu, mateja, wavuta bangi n.k.).

Hapa pana kasoro, huo ukusanyaji wa pesa za stand unaambatana na dalili za wizi na ujanjaujanja, kwani pindi mvua zinaponyesha sana na stand kujaa tope, wale wakusanyaji huwa hawaonekani wakikusanya ushuru wa stand (nahisi huwa wana aibu kutokana na stand zinavyokuwa katika hali mbaya).

Nimekua nikijaribu kuwashawishi madereva wa daladala wagome kuingia katika stand ya Jamatini ili kushurutisha utengenezaji wa stand hiyo, lakini juhudi zangu hazijafanikiwa mpaka sasa (watu wa Dodoma ni wazito sana katika masuala ya kudai haki zao). Ila sijakata tamaa, nitaendelea na juhudi zangu, mpaka pale stand hiyo itakapojengwa katika hadhi ya makao makuu ya nchi.

Wasalaam

Nyanda.
 
ni maeneo ya muda ,stand mpya itakuwa maeneo ya Chadulu-makulu kama unaelekea Udom
 
Back
Top Bottom