Kulikoni Sitta na Makamba? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kulikoni Sitta na Makamba?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ulimbo, Sep 18, 2009.

 1. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Jana usiku nilishangaa sana kuona Makamba anampigia debe Mh. 6 jimboni mwake kuwaambia wapiga kura kuwa wao ni wajanja ndo maana waliweza kumchagua mtu ambaye ni mjanja, na pia kwa sababu wabunge nao ni wajanja, wakamchagua 6 kuwa Spika. Laa ajabu zaidi walekwenda mpaka nyumbani kumsalimia mama mzazi wa sita na machache yaliyozungumzwa ni kwamba sita na makamba hawana ugomvi wowote bali kuna watu wanawagombanisha. Wote wawili sita na makamba walipokezana katika kusema hiyo. Nijuavyo mimi hapa nyuma uhusiano wao haukuwa mzuri, Wana JF naombeni mnisaidie kujua ni nani aliowagombanisha? au kati ya hawa wawili ni nani msema kweli?
   
 2. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Makamba msanii tu na kigeugeu mkubwa. He actually knows nothing though.
   
 3. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kwa kweli baniani mbaya kiatu chake dawa
   
 4. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Thanks, but how about six, is he the same as Makamba?
   
 5. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Sasa kiatu cha nani dawa -SITTA au MAKAMBA? wananichanganya sana hawa.
   
 6. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeutaka uongozi wa chama hicho wilayani Urambo na mkoani Tabora kuhakikisha kuwa Mbunge wa jimbo la Urambo Mashariki ambaye pia ni Spika wa Bunge, Samuel Sitta, anapita katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
  Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, wakati wa ziara yake ya siku mbili wilayani Urambo mkoani Tabora.
  Rai hii mpya inayotoa sura mpya ya Mkamba ambaye alitoa kauli kali hadharani akisema wazi kwamba Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho ina ubavu wa kumdhibiti Sitta, baada ya kuelezwa kwamba kiongozi huyo wa Bunge alikuwa amekaripia kwa kuruhusu mjadala wa wazi bungeni unaoelezwa kujeruhi serikali na chama tawala. Makamba akiwahutubia wananchi wa jimbo la Urambo Mashariki kwa nyakati tofauti, Makamba, alisema kuwa wananchi wa jimbo hilo wakimchagua Sitta hawatakuwa wamefanya makosa.
  "Ni kwa kuona umuhimu wake wabunge kwa pamoja wakamchagua kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na juhudi zake za kuleta maendeleo ya jimbo hili
  zinaonekana pamoja na ujasiri na msimamo wake wa uongozi katika kuliongoza Bunge," alisema Makamba.
  Makamba alimtaja Spika Sitta kuwa ni bakora ya kuwapigia wapinzani, hivyo anastahili kuwa kiongozi kutokana na uwezo wake kielimu na busara alizonazo, na kwamba haitakuwa vyema kama wananchi na viongozi wa CCM mkoani Tabora na Wilaya ya Urambo wakimpoteza.
  Aidha, Makamba alipata fursa ya kuzungumza na mama yake mzazi Sitta, Ajati Zenna binti Said (84), nyumbani kwa Sitta.
  Katika mazungumzo hayo, Makamba alimwambia mama huyo kuwa watu wabaya wamekuwa wakiwachonganisha wakidai kuwa Makamba na Sitta ni maadui, madai ambayo aliyakanusha na kuyaita kuwa ni maneno ya kisiasa.
  Akizungumza na viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya vitongoji, vijiji, kata na tarafa, Makamba alisema kumpoteza Sitta watakuwa wamepoteza mtu wa thamani.
  Awali Katibu wa CCM Mkoa wa Tabora, Iddy Ally Ahamed na Mwenyekiti wa chama hicho mkoa, Hassan Wakasuvi, walisisitiza umuhimu wa Sitta katika jimbo hilo kutokana na juhudi zake za kupigania maendeleo kwa wananchi wake.
  Makamba alisisitiza kuwa wabunge wanaozunguka sehemu mbalimbali
  wakihamasisha jamii kupiga vita ufisadi wanasitahili kuungwa mkono, kwani bila kulisimamia tatizo hilo halitakwisha na wananchi wataendelea kupoteza haki yao kutokana na kutopata haki stahili.
  Hatua ya Mkamba kwenda katika jimbo la Urambo Mashariki na kumpigia debe Sitta imekuja wiki kadhaa baada ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kumkemea Sitta kwa madai kuwa analiendesha Bunge kibabe kutokana na kuruhusu mijadala inayokidhalilisha chama hicho na serikali yake.
  Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho walipendekeza Sitta anyang'anywe kadi na kufukuzwa uanachama.
  Baada ya kikao hicho, Makamba alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akitamba kuwa uamuzi wa NEC ulikuwa sahihi na kwamba chama hicho kina ubavu wa kumdhibiti Sitta kwa sababu aliupata wadhifa wa Spika kupitia CCM.
  Sitta amekuwa akishutumiwa na baadhi ya viongozi wa CCM kutokana na kushirikiana na baadhi ya wabunge wa chama hicho wanaovalia njuga vita dhidi ya ufisadi nchini.
  Msimamo huu mpya wa Makamba unaokana siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, kuzungumza na wananchi kwa kujibu maswali yao ‘laive' kwa njia ya televisheni yaliyoulizwa kwa simu za moja kwa moja, barua pepe na ujumbe mfupi wa simu za mkononi.
  Katika maswali hayo, Kikwete alisema wazi kwamba hakukuwa na mkakati wowote wa NEC kudhibiti wabunge wapambanaji wa ufisadi.
  Hivi karibuni pia taarifa zimetolewa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba nchi wahisani zimetaka maelezo kutoka CCM kama kweli limeamua kudhibiti Bunge ili lisiiwe na makali dhidi ya serikali. Wahisani hao wanahisi kuwa kukatwa kwa makali ya Bunge fedha zao wanazotoa kama msaada hazitakuwa salama.


  CHANZO: NIPASHE
   
 7. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kumjadili makamba ni kama kujiongezea tu hasira....makamba ni kigeugeu kwani hii ndo mara yake ya kwanza kuongea utumbo.....
   
 8. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,663
  Likes Received: 21,886
  Trophy Points: 280
  hawa wanajichanganya tuu kuficha jinsi ccm ilivyobomoka
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Nasikia hasira sana kuona huyu babu anaenda kuwafanyia usanii hadi kwa wazee jimboni inamhusu nini??
   
 10. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #10
  Sep 18, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Wakuu hapa tuweke akili kidogo, we should read between the lines and events.
  Makamba alikuwa katika kambi ya mafisadi kwa 100% na alijitahidi sana kumn'goa Sitta na "wapiganaji" wa ufisadi.
  Makamba na mafisadi walitumia madaraka ya Makamba na pesa ya mafisadi kujaribu kuwafisidi na kuwa ng'oa CCM.
  Bahati mbaya kwao ni kuwa akili yao bado ni ndogo na upeo wa matokeo ambayo yangeweza kutokea hawakuweza kuyafikiria.
  Moja ni kuwa kama Sitta angeng'oka kungekuwepo na uwezekano mkubwa kuwa na revolt ya wabunge wote na hatimaye kuiangusha serikali kwa kuwa na vote of no confidence.
  Mbili hawa jamaa(mafisadi) hawakutegemea kuwa wananchi wengi wangekipinga Chama (CCM) kuwa sasa ndio kimetekwa kabisa na mafisadi
  Tatu, hata wafadhili wameliona hili kuwa kuna mpango mzito wa kuziba pumzi ya watu wanaoikosoa serikali, na kuona kuwa kuna njama za kuwaziba midomo wabunge/watu wanao ikosoa,tena kwa usahihi kabisa serikali yao.
  Nne mgawanyiko katika chama ulikuwa unaonekana kukua na hivyo kupoteza imani ya watu katika mwaka unaoelekea uchaguzi mwakani 2010.
  INAVYOELEKEA-Makamba is under instructions ku make a U- Turn, and in public, so as to ammend the simmering rift, ili imani ya wananchi isiendelee kupotea
   
 11. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2009
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,272
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Watakuwa wameona mwelekeo waliokuwa wamechukua mwanzo ungewaletea matatizo zaidi kuliko faida. Kama wanasiasa uwezo wao wa kugeuka ni mkubwa na ndio siasa ilivyo. Nani alijua Guninita angekuja kuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam.
   
 12. K

  Keil JF-Expert Member

  #12
  Sep 18, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Na bado, mtasikia mengi sana mpaka ifikapo Novemba mwaka huu. Kumbukeni kwamba kuanzia Januari pilika za uteuzi wa wagombea zitaanza rasmi, kwa hiyo muwe tayari kusikia hata yale yasiyowezekana.
   
 13. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #13
  Sep 18, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Bado napata shida kidogo,katika mazungumzo yao mbele ya mama mzazi wa Sitta, wote wawili - Sita na Makamba walisema kuwa hawana uadui wowote kati yao. Yawezekana wao kama wao hawana uadui, lakini kichama wanauadui, Mbona sielewi vizuri hapa? KWA NINI SITTA MWENYEWE AKIRI KUWA HAWANA UADUI wakati ni wazi kuwa hali haikuwa nzuri kati yao?
   
 14. k

  kirongaya Member

  #14
  Sep 18, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kampeni za mapema hazisaidii wadanganyika tumeamka sasa itahitaji maelezo sana mpaka tuelewe
   
 15. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #15
  Sep 18, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Makamba ndo KATIBU MKUU TAIFA WA CCM..Kwa nafasi yake hiyoo anaongoza sekretariati ya chama hicho tawala na katibu wa vikao vyotee vya juu vya chama..

  Tukimjadilii kama kiongozi wa chama kitaifa tutatambua nguvuu yakee kichama.
   
 16. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #16
  Sep 18, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kiatu alichovaa Mh Makamba ni oversize inabidi akivue na kutafutiwa size yake.
   
 17. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #17
  Sep 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wameshagundua kuwa kuwapiga vita akina six ni kuwapiga vita wananchi wengi ambao wako nyuma yao. CCM ilishaona madhara ya kukosa support kutoka kwa wananchi wa kawaida ambao wengi wanaamini katika maneno ya akina six. Hiyo ni njia ya kujirudi ili kupata public support. Sijui kama hawajachelewa
   
 18. K

  Keil JF-Expert Member

  #18
  Sep 18, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hawajachelewa, kosa wangefanya kama wangefanikiwa kumnyang'anya kadi Sam Six kwenye kikao cha NEC kilichopita. Hawa jamaa wajanja sana wamepima upepo wameona hakuna dalili njema na kukumbatia mafisadi ni kujimaliza wenyewe, dawa ni kuwabeba wote.
   
 19. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #19
  Sep 18, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,464
  Likes Received: 1,401
  Trophy Points: 280
  CCM ni wasanii sana wameona hali ilivyo sasa wameanza kujififanya kumfuatafuata ili waonekane wapo nae
   
 20. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #20
  Sep 18, 2009
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Makamba ni mnafiki mkubwa sana> tena kama ccm hawajajua huyu ndiye anaekiharibu chama. Sijui yukoje huyo jamaaa
   
Loading...