Kulikoni Singida hakuna mwakilishi baraza la mawaziri? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kulikoni Singida hakuna mwakilishi baraza la mawaziri?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tumsifu Samwel, May 26, 2010.

 1. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #1
  May 26, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nilipata fursa ya kumuuliza mh. JK kwa nini mkoa wa Singida hauna mwakilishi kwenye baraza lake la mawaziri? zaidi ya John chiligati na ambaye siyo mzawa wa mkoa wa Singida? jibu: "we bana vipi? wabunge wengi wa singida elimu yao ni kidato cha nne unategemea mtu kama huyo umpe uwaziri afanye nini ?"

  Hivi mtu mwenye elimu ya kidato cha nne hawezi kuongoza wizara kwa sababu ya kiwango chake cha elimu?
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,528
  Trophy Points: 280
  Uteuzi wa nafasi za mawaziri hazitegemei ni watu wa wapi, ila pia sio kweli kuwa wabunge wa Singida wengi ni ma Form Four Levers,
  Nyalandu ni graduate, Dewjini graduate, Martha Mlata ni graduate, etc tena hawa ni wale ninaowajua kihivi hivi kabla hata sijapekua CV zao.
  Hivyo kwa Singida si afadhali hata mnaye huyo Chiligati, mngekosa kabisa ingekuwaje?.
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako Carthbetl,

  Nadhani yuko Mheshimiwa Lazaro Nyalando ni msomi wa chuo kikuu.
   
 4. O

  ODD Member

  #4
  May 26, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CL Hapo unatudanganya, jibu kama hilo hawezi kutoa JK. Hata hivyo Mkoa wa Singida una zaidi ya kabila tano ikiwemo ya Chiligati ambayo ni Mgogo. Si vibaya kujadili hoja yako kwa nini hakuna waakilishi.
  maelezo ya watu wa Mkoa wa Singida ni kwamba ni watu wa ajabu sana.si kwamba hakuna wasomi, wala si kwamba ni maskini sana, la hasha bali ni ule ushawishi wa kuingia kwenye siasa hawana.matatizo kwao ni kama sehemu ya maisha . We anagalia barabara sehemu ya mkoa huu tu haijakamilika na ndio kuu kushinda zote. Cha ajabu nikwamba wanajisikia wao ni mashini sana kwa hiyo hata akipwa fulana au shs 200 mtu anaona kasaidiwa sana. Halafu pia watu wa huko wanaangalia anagombea ni wa ukoo gani au babu/baba yake akuliwa nani kama hawamjui vizuri yaani aliwahi kuwasaidia hupati kitu.
  wabunge wa singida
  MANYONI - 2- level -MASTERS
  SINGIDA-3 -Level -Diploma
  IRAMBA-2- Level -F -IV na Diploma
  VITI MAALUM- F IV na DRS 7

  Kazi ipo kuweza kuwabalisha , labda mwaka huu - big up LISSU AND JUMBE
   
 5. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Martha Mlata ambaye ni Mbunge wa viti maalumu toka mkoa wa Singida ninayemfahamu mimi sio GRADUATE labda kama kagraduate leo.
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  May 26, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kwani suala la ujenzi wa barabara kuu ni la wananchi wa Singida au ni la Serikali kuu? Serikali ya Tanzania imewekeza nguvu zake nyingi Dar es Salaam pekee na Mikoa mingine imesahaulika kabisa au inakumbukwa kidogo! Sasa hivi Dar es Salaam haikaliki kwa msongamano wa ajabu! Na huko unakosema watu wa Singida wameridhika na vijishilingi 200 ni tusi kubwa sana na inaonesha una chuki na watu wa Mkoa huo. Hivi CCM wanapohonga chumvi, T-Shirt, Kofia, Vitenge, nk huwa wanavipeleka Singida pekee? Na kama sivyo hiyo mikoa mingine huwa wanapokea vitu hivyo kwa sababu wao ni "matajiri?" Hukumu kwa haki ndugu yangu na si kutoa kejeli zisizokuwa na msingi wowote!
  Kama JK alidai kuwa Singida hakuna wasomi isipokuwa walioishia kidato cha nne tu simwelewi mheshimiwa huyu. Labda kama alikuwa "anatania" kama alivyotania kwenye suala la TAKRIMA!
   
 7. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2010
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Huyu mama alikuwa UK akisoma kwa muda wa kama miaka miwili au mitatu. Nafikiri kwasasa ni graduate. Sijui kama alikuwa anasoma first degree au masters.

  Viongozi wakija, alikuwa ndiye anatuanzishia wimbo wa taifa.
   
 8. Kiungani

  Kiungani JF-Expert Member

  #8
  May 26, 2010
  Joined: Feb 2, 2007
  Messages: 274
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35

  Hapa unamuonea JK......

  Ili aweze kusema hivyo itabidi afikiri kwanza anachokisema, ......hapo tu ni kazi tayari.....
   
 9. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kwako Tyuti Mlenge Chumvi Mtembezi na Kitila Mkumbo,

  Je Wana wa Ilamba kuna majibu kwa hii hoja?
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Baraza la mawaziri ambalo halieleweki linafanya kazi gani? Hebu mtupumzishe huko..ebo
   
 11. P

  Paul S.S Verified User

  #11
  May 27, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
   
 12. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  We CathbertL hilo sio jambo la Kuuliza. Hivi haujui kuna maswala mbalimbali yanayohusisha logistics za Kimataifa. Sasa huoni kwa elimu hiyo tutaishia kuwa na mawaziri watakaokuwa wanaingia mikataba bila kuielewa sawasawa?
  Hapa ndugu yangu tuwe wakweli na tuache unazi.!
  Mimi ninachojiuliza je Singida hakuna hata Mbunge mmoja mwenye Degree?
  Kama ni hivyo mwaka huu tuwachague kina Tundu Lisu wengi.!
   
 13. P

  Paul S.S Verified User

  #13
  May 27, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mohammed Dewji graduate,chiligati graduate,Nyalandu Masters,martha mlata nadhani atakua amemaliza masomo uk shahada ya kwanza,
   
 14. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  je mawaziri kutoka mkoa wa tabora wote vimeo na ni wasomi wa kutosha
   
 15. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kwa mtazamo wangu sidhani kama Baraza la Mawaziri ni baraza la kuwakilisha mkoa, kwa nchi yetu baraza la mawaziri ni kubwa sana kulinganisha na nchi zilizoendelea kama USA na UK.

  Mtu unapozungumzia baraza la mawaziri yakupasa kujua kuwa ile dhamana ya Uwaziri si dhana ya kisiasa kama ilivyo kwa sasa, na nahisi imekuwa hivyo kwa kuwa siku zilizotangulia kulikua na wasomi wachace wanaojishughulisha na siasa tofauti na sasa.

  Inabidi Uwaziri iwe ni nafasi ya kuteuliwa kulingana na uelewa ("profession") juu ya wizara husika na si kuwa umetokea mkoa gani.
   
 16. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Eh! Wazawa wa Mkoa wa Singida ndio akina nani na Chiligati si mzawa kwa vipi? Kama Chiligati si mzawa wa Singida na Dewji naye tutamwitaje? Ni aibu sana kuzungumzia habari za 'uzawa' kwa misingi ya mikoa na wakati huo huo tunataka kujivuna kwamba tuna nchi ambayo imekwishatoka kwenye enzi ya ukabila!
   
 17. O

  ODD Member

  #17
  May 27, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na huko unakosema watu wa Singida wameridhika na vijishilingi 200 ni tusi kubwa sana na inaonesha una chuki na watu wa Mkoa huo. Hivi CCM wanapohonga chumvi, T-Shirt, Kofia, Vitenge, nk huwa wanavipeleka Singida pekee? Na kama sivyo hiyo mikoa mingine huwa wanapokea vitu hivyo kwa sababu wao ni "matajiri?" Hukumu kwa haki ndugu yangu na si kutoa kejeli zisizokuwa na msingi wowote!


  bucha: Sina chuki usinielewe vibaya .  Naheshimu sana mawazo yako lakini unapaswa kuheshimu watu wengine pia kabla hujatoa mawazoyako, unaposema singida hawana ushawiashi wa kuingia kakatika siasa umetumia kigezo gani hebu fafanua tafadhali,

  paul: kuna wasomi wengi singida mbona hawajitokezi kugombea nafasi za siasa? na hao wachache wanaojitokeza mbona basi hawapati? fanya utafiti uone watu waliojitokeza wasomi 2005 lakini wakshindwa? tatizo ni nini?

  kufanya uchaguzi kila mara hilo sio sababu kuwa na ushawishi , kinachotakiwa je wanachangua right person ? angalia kwa mtazamo huo wala mimi sina nia mbaya na watu singida
   
 18. MKUNGA

  MKUNGA JF-Expert Member

  #18
  May 27, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 443
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hutaweza kuongoza nchi kama ukitaka kila mkoa upate mtu katika teuzi mbali mbali. Huo ni ukanda na ni hatari kwa taifa kwani kwenye U-DC, U-RC ubalozi nanafasi zingine
   
 19. W

  WildCard JF-Expert Member

  #19
  May 27, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Ni Urambo tu yenye bahati nzuri. Imetoa Speaker, Mke wa Speaker, na Prof Kapuya wote wazito nji hii!
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  May 27, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,528
  Trophy Points: 280
  Thursday, 25 December 2008

  MH.MLATA AKWAA NONDOZZZ YAKE  [​IMG]Mbunge wa viti maalumu wa singida Mh. Martha Mlata katika picha pamoja na Prof. wa chuo mara baada ya kupokea Shahada yake majuzi hapa UINGEREZA
  at Thursday, December 25, 2008 [​IMG]
   
Loading...