Geza Ulole
JF-Expert Member
- Oct 31, 2009
- 59,188
- 79,404
8th January 10
CCBRT: Tumetimiza vigezo vyote vya usajili
Richard Makore
Hospitali ya CCBRT imesema imekidhi masharti yote ya usajili ambayo yanaiwezesha kutoa huduma hiyo kwa jamii.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali hiyo, Erwin Telemans alipozungumza na Nipashe ofisini kwake.
Alitoa ufafanuzi huo kufuatia taarifa iliyotolewa juzi na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) kuwa hospitali hiyo ni miongoni mwa Asasi 100 zinazotakiwa kufutiwa usajili wa udhamini kutokana na kukiuka masharti.
Telemans aliliambia Nipashe kuwa wana ushahidi wa maandishi kwa jinsi ambavyo wanafuata masharti.
Alifafanua kuwa CCBRT ni mshirika mkubwa wa serikali hivyo wasingeweza kuendesha hospitali hiyo kwa kukiuaka masharti ya aina yoyote.
Aliahidi kwenda Rita ili kujua kwa ni nini wamewaingiza katika orodha ya Asasi ambazo zinatakiwa kufutiwa usajili.
Ofisa huyo alisema walichobadilisha ni anuani pekee lakini vitu vingine ikiwemo marejesho ya wadhamini wameishalipia na risiti wanazo.
Alisema CCBRT inatoa huduma za matibabu bure kwa watoto wa chini ya miaka matano ambao wana matatizo mbalimbali lakini bado mchango wao hauonekani.
Juzi Rita ilitoa siku 30 kwa Asasi hizo zikiwemo za dini kutoa maelezo ya kwa nini zisifutiwe usajili wao.
Hata hivyo, alisema hatua hiyo ya Rita haitaathiri shughuli zao za kila siku za kutoa huduma kwa watu wenye matatizo mbalimbali ambao hawana uwezo wa kulipia matibabu.
Aliikumbusha jamii kwenda CCBRT na kupatiwa huduma ya bure kwa wanawake wenye ugonjwa wa Fistula na watoto wadogo wenye ulemavu ambapo huduma hizo zinatolewa bure.
NIPASHE
http://www.ippmedia.com/frontend/functions/print_article.php?l=12254
Mi ninachojua CCBRT husaidia wamama wajawazito ambao hulala wanne wanne mahospitali ya serikali na pia husaidia watoto walemavu ambao wamesahaulika na serikali ya Mbembeaji! Sasa huku kutaka kuifunga hii taasisi mbona kumekaa kiuzushi zushi na kisiasa zaidi? Naomba mnisadie kwa anayejua kulikoni?