Kulikoni serikali kutaka kuifunga CCBRT

Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
58,983
78,865
8th January 10
CCBRT: Tumetimiza vigezo vyote vya usajili

Richard Makore

Hospitali ya CCBRT imesema imekidhi masharti yote ya usajili ambayo yanaiwezesha kutoa huduma hiyo kwa jamii.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali hiyo, Erwin Telemans alipozungumza na Nipashe ofisini kwake.
Alitoa ufafanuzi huo kufuatia taarifa iliyotolewa juzi na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) kuwa hospitali hiyo ni miongoni mwa Asasi 100 zinazotakiwa kufutiwa usajili wa udhamini kutokana na kukiuka masharti.
Telemans aliliambia Nipashe kuwa wana ushahidi wa maandishi kwa jinsi ambavyo wanafuata masharti.
Alifafanua kuwa CCBRT ni mshirika mkubwa wa serikali hivyo wasingeweza kuendesha hospitali hiyo kwa kukiuaka masharti ya aina yoyote.
Aliahidi kwenda Rita ili kujua kwa ni nini wamewaingiza katika orodha ya Asasi ambazo zinatakiwa kufutiwa usajili.
Ofisa huyo alisema walichobadilisha ni anuani pekee lakini vitu vingine ikiwemo marejesho ya wadhamini wameishalipia na risiti wanazo.
Alisema CCBRT inatoa huduma za matibabu bure kwa watoto wa chini ya miaka matano ambao wana matatizo mbalimbali lakini bado mchango wao hauonekani.
Juzi Rita ilitoa siku 30 kwa Asasi hizo zikiwemo za dini kutoa maelezo ya kwa nini zisifutiwe usajili wao.
Hata hivyo, alisema hatua hiyo ya Rita haitaathiri shughuli zao za kila siku za kutoa huduma kwa watu wenye matatizo mbalimbali ambao hawana uwezo wa kulipia matibabu.
Aliikumbusha jamii kwenda CCBRT na kupatiwa huduma ya bure kwa wanawake wenye ugonjwa wa Fistula na watoto wadogo wenye ulemavu ambapo huduma hizo zinatolewa bure.

NIPASHE
http://www.ippmedia.com/frontend/functions/print_article.php?l=12254

Mi ninachojua CCBRT husaidia wamama wajawazito ambao hulala wanne wanne mahospitali ya serikali na pia husaidia watoto walemavu ambao wamesahaulika na serikali ya Mbembeaji! Sasa huku kutaka kuifunga hii taasisi mbona kumekaa kiuzushi zushi na kisiasa zaidi? Naomba mnisadie kwa anayejua kulikoni?
 
8th January 10
CCBRT: Tumetimiza vigezo vyote vya usajili

Mi ninachojua CCBRT husaidia wamama wajawazito ambao hulala wanne wanne mahospitali ya serikali na pia husaidia watoto walemavu ambao wamesahaulika na serikali ya Mbembeaji! Sasa huku kutaka kuifunga hii taasisi mbona kumekaa kiuzushi zushi na kisiasa zaidi? Naomba mnisadie kwa anayejua kulikoni?

mKUU maelezo ya CCBRT ni mazuri sana lakini ujue kwamba hata kama unamsaidia nani, ni lazima ufuate taratibu za nchi!!! kuna hata mashirika meeengi ya kidini hapa kwentu hata hilo sshirika mama la wakristu nalo limewekwa kwenye list pamoja na mashirika kadhaa ya kiislamu na madhehebu mengine

ushauri wangu ni kwamba hao CCBRT wafuate taratibu, wapeleke vigezo kesi yao itakuwa imekwisha na hawako peke yao

Tupunguze kutafutana uchawi kwa mambo yaliyo wazi mkuu

haya ni maoni binafsi tu
 
Wewee mimi sio mtoto kuweka hii article hapa hili swala lina ukiritimba ndani yake, kama serikali wako genuine na madai yao wangeweka hadharani ni nini CBRT haifuati katika hizo taratibu aka sheria za nchi! na sio kuambiwa tu ati hawafuati taratibu, zipi hizo nifafanulie!!!
 
Unadhani Serikali ingeweka wapi hizo taratibu ambazo CCBRT haijazifuata wakati notisi iliyotolewa ni kwa orodha ya asasi na mashirika mengi na CCBRT ni miongoni mwao?. Hiyo hoja ya kuitaka Serikali iweke hadharani nini CCBRT haikufuata unamaanisha kila asasi iliyopewa notisi ilipaswa ichambuliwe na kuanikwa mapungufu yake hadharani ???, na huko hadharani ni wapi, magazetini au habari maelezo???

Kama CCBRT wanaushahidi kuwa wao wapo kihalali ya nini kuhangaika kwenye vyombo vya habari badala ya kuwasiliana na RITA kuthibitisha kuwa uhalali wa shirika hilo?.

Sheria na taratibu ni lazima zizinagtiwe hata kama unatoa misaada bure. Hapa sio siasa mzee!....Kilichotolewa na Serikali ni notisi tu, CCBRT wanahaki ya kukanusha. Hizi porojo za kutaka "public mercy" hazina msingi kwenye utawala wa sheria!.
 
Hizi porojo za kutaka "public mercy" hazina msingi kwenye utawala wa sheria!.[/QUOTE]
Utawala wa sheria upi unaoulingia wewe hata Tz? Pana utawala wa sheria hapa kweli? Usije ukachekwa na watu! Tz hamna utawala wa sheria na unajua fika. Mifano ni mingi. Hapa pana chuki na upendeleo tu!
 
Unadhani Serikali ingeweka wapi hizo taratibu ambazo CCBRT haijazifuata wakati notisi iliyotolewa ni kwa orodha ya asasi na mashirika mengi na CCBRT ni miongoni mwao?. Ulitaka kila Taasisi icahmbuliwe kwenye magazeti kuwa haikufuata taratibu zipi???

Kama CCBRT wanaushahidi kuwa wao wapo kihalali ya nini kuhangaika kwenye vyombo vya habari badala ya kuwasiliana na RITA kuthibitisha kuwa uhalali wa shirika hilo?.

Sheria na taratibu ni lazima zizinagtiwe hata kama unatoa misaada bure. Hapa sio siasa mzee!....Kilichotolewa na Serikali ni notisi tu, CCBRT wanahaki ya kukanusha. Hizi porojo za kutaka "public mercy" hazina msingi kwenye utawala wa sheria!.

Huu utawala wa sheria unaosema wewe hauwagusi Maponjoro cum fisadis bali taasisi zinazosaidia walalahoi sio? Kama serikali iko genuine inapaswa kueleza wazi ni nini CCBRT imekosea (yaani taratibu gani hazikufuatwa) na sio kwa mtindo huo kama wa siasa siasa! Why not kwa nini wasiseme taratibu zilizokiukwa? Nina maana ya kuizungumzia CCBRT na si taasisi nyingine sababu najua wanachofanya (ujenzi wa mahospitali nakusaidia magonjwa ya wanawake na watoto kitu ambacho serikali ya Wakubembea imeshindwa) na pia kiongozi wake ameeleza hapo juu kwenye hii article kama umeisoma! serikali haipaswi kuanza kuchukua hatua au kuendeshwa kwa kupitia hisia za watu flani flani! ndo maana nataka ushahidi hapa! ikumbukwe walitaka kuzitoza kodi NGO's ila kwa kupitia shinikizo la Makanisa wakabatili uamuzi wao!
 
8th January 10
http://www.ippmedia.com/frontend/functions/print_article.php?l=12254

Mi ninachojua CCBRT husaidia wamama wajawazito ambao hulala wanne wanne mahospitali ya serikali na pia husaidia watoto walemavu ambao wamesahaulika na serikali ya Mbembeaji! Sasa huku kutaka kuifunga hii taasisi mbona kumekaa kiuzushi zushi na kisiasa zaidi? Naomba mnisadie kwa anayejua kulikoni?

Kosa kubwa wanalofanya CCBRT ni kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na kuhudumia watoto wenye mahitaji mbalimbali bure na kuwaepusha na vifo. Hili jambo ni kinyume na makubarianao kati ya watawala wetu na Lucifer boss wao hivyo amewatuma kuifunga CCBRT.

Sioni lingine hapo kwa akili zangu za kawaida
 
Wewee mimi sio mtoto kuweka hii article hapa hili swala lina ukiritimba ndani yake, kama serikali wako genuine na madai yao wangeweka hadharani ni nini CBRT haifuati katika hizo taratibu aka sheria za nchi! na sio kuambiwa tu ati hawafuati taratibu, zipi hizo nifafanulie!!!
Tafuta tangazo la serikali linaloeleza kwa nini mashirika yasiyo ya kiserikali zaidi ya 100 ( si CCBRT peke yake) yanataka kufutwa-humo wameeleza ni kwa nini yamepewa notisi ya mwezi mmoja kukamilisha hayo mapungufu kabla ya kufutia usajili. wala hakuna cha mkono wa mtu wala nini, uzembe wao wenyewe tu
 
Back
Top Bottom