Kulikoni na majina haya?

Fundi Mchundo

Platinum Member
Nov 9, 2007
8,936
6,846
Hivi karibuni pametokea majina yanayochanganya kidogo. Nilizoea kumwona MTOTO WA MKULIMA sasa naona kuna MTOT WA MKULIMA, vile vile nilimzoea MzalendoHalisi naona sasa kuna ZalendoHalisi. Hivi hawa ni hao hao au wana uhusiano wa namna fulani hadi kuchukua majina yanayofanana kiasi hicho? Au hao wengineni fan wa aliyetangulia na wangependa kufananishwa nao? Nauliza tu. Kulikoni?
 
Nafikiri baada ya kile kilichomkuta Kubenea watu wameamua sasa kujitoa muhanga kama jina la ZalendoHalisi yaaani ukitafsiri unaona kabisa ni mtu ambaye yupo tayari kwa lolote, ila nafikiri kwasababu nao wapo labda watupe siri ya Mabadiliko
 
Ebwaana mkuu mie haya majina yananichanganya sana,alafu nimekupa nlipata kimbembe siku moja.Herufi za kwanzaza Jina la demu wangu lilikuwa lina fanana na la mama,sasa katika kutuma SMS nikachanganya.....pata picha hapo msg ya demu wako inakwenda na mama yako.....

....kimbembe si mchezo na hawa ndio inakuwa ndivyo sivyo.Au ni mtu mmoja
 
..duh!bonge la noma,hasa kama ulikuwa unamuuliza yale maswali ya kutafutia usingizi!

Kaka hapo umeniacha hoi. Hebu tupe shule kidogo ni yepi hayo maswali? you never know I could ask one tonight, si unajua tena maisha yalivyo magumu siku hizi hata usingizi kupatikana ni tabu?
 
Hivi karibuni pametokea majina yanayochanganya kidogo. Nilizoea kumwona MTOTO WA MKULIMA sasa naona kuna MTOT WA MKULIMA, vile vile nilimzoea MzalendoHalisi naona sasa kuna ZalendoHalisi. Hivi hawa ni hao hao au wana uhusiano wa namna fulani hadi kuchukua majina yanayofanana kiasi hicho? Au hao wengineni fan wa aliyetangulia na wangependa kufananishwa nao? Nauliza tu. Kulikoni?

Aisee mkuu sijui ila hata mimi mwenyewe niliona post ya MTOT wa
MKULIMA nikachanganyikiwa nikasema labda mtandao una matatizo hadi baadae nikagundua kuwa sio MTOTO WA MKULIMA BALI NI MTOT WA MKULIMA. Mzee sijui kama tuna uhusiano kwani si unajua JF bwana na haya majina yetu Bandi? so inawezekana tuna usiano au hatuna ila mimi simfahamu
 
Pole mkuu! Ni kama vile viatu vya michezo vilivyokuwa vinauzwa bei poa na machinga ambavyo viliitwa Adibas badala ya adidas na stripe nne badala ya tatu. Ukiuliza unaambiwa ni 'genuine' kutoka ujerumani! Pole mkuu.
 
Fundi
MzalendoHalisi na ZalendoHalisi ni watu tofauti na wamejiunga JF mda tofauti. Wote tu marafiki na tunafahamiana hapa jamvini!

Wakati najiandikisha JF -mimi nilitaka jina la Mzalendo nikakuta limeshachukuliwa ndo nikaopt for MzalendoHalisi. Yawezekana pia ZalendoHalisi nae alitaka kuregister kwa Mzalendo akakuta liwechukuliwa, akaendelea na MzalendoHalisi nalo akakuta limechukuliwa ndo akaopt na ZalendoHalisi.

MzalendoHalisi
 
..duh!bonge la noma,hasa kama ulikuwa unamuuliza yale maswali ya kutafutia usingizi!
Mkuu acha tu maswali yalikuwa hayo hayo....maana kwanza huwa kuna ka salamu kale ka kuanzia mie nilianza nako!....sauti nasikia ya Bi mkubwa ilibidi nizuge zuge tu
 
Back
Top Bottom