Kulikoni MWALIMU NYERERE FOUNDATION? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kulikoni MWALIMU NYERERE FOUNDATION?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mnyamahodzo, Mar 25, 2011.

 1. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kabla na baada ya Mwl Nyerere kufariki, mfuko huu walikuwa na ofisi zao mkabala na Makumbusho ya Taifa, Dar.
  Baadaye, wakalibomoa jengo la ofisi zao wakiwa malengo ya kujenga ghorofa refu na zuri. Eneo husika, wakalizungushia mabati ikiwa maandalizi kuwa ujenzi utaanza mapema.
  Kinachonishangaza kwasasa ni kuwa jengo la ofisi la zamani limevunjwa, lile walilotaka kujenga halipo na wamekwisha kutoa mabati yote ya uzio na picha ya jengo litakavyokuwa nayo ilikwisha ondolewa.
  Naomba kujuzwa nini kiliendelea na kinaendelea.
   
 2. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #2
  Mar 25, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Ndo tanzania hiyo. Nasiki wapo Benjamini Mkapa Tower nadhani watakuwa wamepanga au??
   
 3. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Mzee Butiku anajua zaidi....
  Mkimfuatilia na kumuuliza, akiwajibu kwa upole itakuwa vema! Akiwajibu kwa ukali mtakuwa mmepata jibu.
   
 4. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Wamepigwa stop....kwa vile jengo lao litakuwa na ghorofa 22 basi watamchungulia Rais akiwa ikulu kama mita 400 hivi
   
 5. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Hivi toka yale maghorofa ya Wìzara ya Ardhi na Utumisì ama lile la pale karibu Ocean Road Cancer Institute hawawezi mchungulia.

  Mbona alipokuja Bush, waliichungulia Ikulu toka Kilimanjaro Hotel? Kama haitoshi mbona wataalamu wa IT kama M Melo wanaweza mchungulia toka ofisini/vyumbani mwao(kwa google earth, etc).
  Kwani majengo yakiwa ya level moja ndiyo usalama unakuwa juu? Connect with assasination of John F Kennedy.
   
 6. m

  msosholisti Member

  #6
  Mar 25, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ni lefu sana basi walipunguze. Mbona twin tower nalo ni lefu.
  Wale wazee longolongo tu. wanalimung'unya fungu la nyerere foundation taratiiibu.
   
 7. Observer2010

  Observer2010 Senior Member

  #7
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Baada ya kuona ufisadi umekithiri ndani ya serikali ya CCM, Sabodo (Mfadhiri mkuu wa hiyo foundation) ameamua kuhamishia hela zake ambazo zingesaidia ujenzi wa hilo jengo kwenye kuwachimbia visima watanzania wenye matatizo lukuki yasiyohesabika.
   
 8. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kwamba wanalimung'unya fungu la ujenzi wa ghorofa, nina mashaka.
  Ila nilichowahi kusoma kwenye gazeti wakati fulani huko nyuma ni kuwa kuna namna fulani "nyumba kubwa ya mzee wa kaya" wanaitilia ngumu hii taasisi. Na kwamba bifu lao likolezwa na lile Kongamano la miaka 10 bila Mwalimu, (lilikuwa mwaka jana sijui.
   
 9. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Habari yote iko kwenye red.
   
 10. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,180
  Likes Received: 487
  Trophy Points: 180
  Ukweli uko wazi, Nyerere foundation haina mahusiano mema na IKULU tangu mchakato wa kutafuta mgombea wa urais kupitia ccm 2005.
  Tangu hapo sijawahi sikia popote mkuu wa nchi akiitaja nyerere foundation wala Baba wa taifa.ila nimemsikia mara nyingi akitaja Mzee nyerere!
  *KULIKONI....? kuna mahali wanaminyiwa kütimiza malengo yao ili kuipunguzia nguvu za ushawishi mbele ya watanzania,kwa lengo kuwanufaisha wanamtandao 2015.
   
Loading...