Kulikoni Marian Boys na Girls matokeo ya kidato cha sita

ndo maana ukaitwa mtihani,hauwezi kila mwaka kuongoza wewe tu!
Kuna mkuu kasema FEZA hupewa mtihani mwezi mmoja kabla,siyo kweli mwanangu anasoma pale hilo jambo halipo kinachowabeba FEZA ni aina ya wanafunzi wanaowachukuwa pamoja na mazingira BORA ya shule.
interview ya form 5 wanafanya December kabla hata matokeo ya necta hayajatoka na December hiyo hiyo wanatoa selection pamoja na kumtaka mzazi alipe ada kabisa,wakati shule zinasubiri matokeo ya necta wao walishaanza masomo toka mwezi March!!!!
Hii ni inside job mzazi huwezi kujua. Wewe ndio fursa yenyewe inayotafutwa ili husiamishe mwanao na uwashawishi ndugu na jamaa walete watoto wao. Hupo?
 
Kwangu Mimi mshindi ni yule aliyetoka Temeke na Benjamin mkapa, kwa yule wa Temeke anastahili zawadi kuliko hao wengine...
Kokote uliko pokea hongera yangu, Je kuna mazingira gani kuwasaidia wanafunzi hawa?
Huyu dogo wa Temeke ndo the real TO aiseee
 
Wa kwanza Form six ametoka Feza Boys EGM, nilimpongeza kijana kwa juhudi zake pia juhudi za wazazi wake kumlipia ada ya Feza Boys.

Ni wapiga kura wangapi wenye uwezo wa kulipa ada hii?
Shule ngapi za kata zinaweza kutoa namba one?

Tabaka letu la wapiga kura litabaki kuwa la wapiga kura.

Namba 3 kitaifa ametoka TEMEKE SEKONDARI PCB shule yenye div 0 kama zote
 
Sijui nini kinaendelea huko. Nilibahatika kusoma Marian girls. usidanganywe aisee tulikuwa tunasoma, yaani majibu yakitoka utakuta wanafunzi 90, DIV 1 ni 87 wengine DIV 2. Watu walihisi tunapewa majibu ila uchawi ulikuwa ni kusoma, discipline na kusali.

Nahisi labda Father Bayo kazeeka sasa, hakuna usimamizi.

Hahahahahahahahahah, Mama mzungu habari ya siku nyingi??
 
Kuna uwezekano mkubwa hizi shule zikawa zinaiba mitihani mfano ni Alliance toka walivyodakwa wamepotea kabisa kwenye game
Shule nyingi ndivyo zinavyofanya ili kuvutia wateja. Wanafundisha mitihani kiaina ili majibu yasifanane na kujulikana. Wanafunzi wanakuwa hawajui, wakidhani wanafundishwa masomo ya kawaida. Elimu yetu bado kabisa inaabudu mno vyeti na mitihani! Ndiyo maana unaona watu wana-pass vizuri lakini inapofika suala la utendaji inakuwa ziro.
 
ndo maana ukaitwa mtihani,hauwezi kila mwaka kuongoza wewe tu!
Kuna mkuu kasema FEZA hupewa mtihani mwezi mmoja kabla,siyo kweli mwanangu anasoma pale hilo jambo halipo kinachowabeba FEZA ni aina ya wanafunzi wanaowachukuwa pamoja na mazingira BORA ya shule.
interview ya form 5 wanafanya December kabla hata matokeo ya necta hayajatoka na December hiyo hiyo wanatoa selection pamoja na kumtaka mzazi alipe ada kabisa,wakati shule zinasubiri matokeo ya necta wao walishaanza masomo toka mwezi March!!!!
Ada Yake ni kiasi gani
 
Naona unarusha mawe na wakati huo huo umejificha kwenye nyumba ya vioo! Hayo masanamu yatawaandama milele! Maana kuna St Mary's Mazinde juu pale ya Lushoto!

Ikitokea siku shule kutokea huo upande wenu ikaingia 10 bora itabidi kama taifa tufanye sherehe. Maana yatakua ni maajabu ya dunia.
Feza mbona zishaingia mara nyingi tu? Au unadhani feza zinamilikiwa na kigango? Pale baraza mlipageuza kigango pamoja na bibi yenu yule
 
Back
Top Bottom