Kulikoni Mamalaka ya Huduma za Meli (TASAC) kujilipa posho kwenye vikao vya bodi zaidi ya Tsh milioni 600!

Peramiho yetu

JF-Expert Member
May 25, 2018
5,304
14,913
Nawasalimu kwa jina la Muungano.

Wakuu kama Rais wetu mpendwa alivyosema leo mamlaka hii imefanya vikao 27 vya bodi ya mamlaka hiyo kwa mwaka jana pekee na wametumia kiasi cha shilingi bilioni moja kama posho za vikao tu.

Haya yote yamefanyika chini ya Rais wetu hayati John J P Magufuli.

Najiuliza ni taasisi ngapi au mamlaka ngapi zimefanya vikao vya aina hii visivyo na tija kwa taifa.

Kwa mantiki hiyo ina maana Hayati hakuweza kuliona hili jamani kwa kujipambanua kote kule?

Msaada ninaoomba tupate majina ya Mwenyekiti na Wajumbe wa bodi ya TASAC tuwajue hawa mchwa wasiokuwa na huruma na taifa hili.

#UKINIZINGUA NITAKUZINGUA

=======

The Tanzania Shipping Agencies Corporation (TASAC) held 23 dubious board meetings within one year at a cost of more than Sh600 million.

This was said today by President Samia Suluhu Hassan saying she was disappointed by misuse of public funds at the agency
“I am very disappointed, nothing has been improved at Tasac yet you conducted meetings and spent a lot of public funds , I have appointed you as a young man to work, I want to see improvements in this area and contribute to government revenue and not otherwise,” said President Hassan.

Ms Hassan said that on Tuesday, April 6 when she was swearing in permanent secretaries and deputy permanent secretaries at the State House following a minor reshuffle on Sunday.

“Let me tell you after nominating your name I slept around 4am reading the social media comments with most of them saying that you cannot perform because you are a new name,” she insisted.

She told the new director general Mr Kaimu Mkeyenge “You were also working in Tasac and you know all the evil that were happening at Tasac but I have decided to promote you now go and hard in collaboration with other staffs and clean up the institution,” said the President
 
TASAC ni Shirika lililofanya sana biashara ya kuingiza kipato mwaka jana na mwaka huu. Kwa pesa wanayozalisha hawapaswi kupewa ruzuku hata senti.

Wajanja wachache wamezivuna dollar kutoka kazi wanazofanya za Shipping Agent, Clearing and Fowarding,Ship registry, Seafarers registration.

TASAC wanatakiwa wawe ni wa pili baada ya TPA kwa mapato.
 
TASAC ni Shirika lililofanya Sana biashara ya kuingiza kipato mwaka jana na mwaka huu. Kwa pesa wanayozalisha hawapaswi kupewa ruzuku hata senti...
Kuna yule mzee anaitwa Reantus Mkinga, alikuwa anatumika sana kuongea kwenye TV wakati wa kampeni na kumfagilia mwendazake hadi akapewa Ujumbe wa Bodi, siku hizi hasikiki kumbe ndio walikuwa wanatupiga hizi hela. Kweli ukiwa unakula huruhusiwi kuzungumza!
 
Nilikua najiuliza siku hizi Renatus Mkinga simuoni kwenye tv na makalabrasha yake kumbe yuko tasac anakula posho za kufa mtu, 😂😂😂. Dunia hii.

Kelele zote zile za Mkinga kumbe ilikua kukosa posho tu.
 
Kuna Mzee mmoja anajiita Mkinga, alikuwa mkosoaji sana kila TV utamkuta anachambua mabaya ya serikali, alivyowekwa kwenye hiyo bodi kapumzika anakula posho tu.

Sisi wanyonge tunakanyagana uwanjani kuaga mwili wa mwamba wa Africa.
 
Rais achukue hatua siyo kututangazi halafu basi. Aanze na hao jamaa mpaka watapike hizo hela. Hayo ni matumizi mabaya ya kodi ya wananchi makini
 
Kuna yule mzee anaitwa Reantus Mkinga, alikuwa anatumika sana kuongea kwenye TV wakati wa kampeni na kumfagilia mwendazake hadi akapewa Ujumbe wa Bodi, siku hizi hasikiki kumbe ndio walikuwa wanatupiga hizi hela. Kweli ukiwa unakula huruhusiwi kuzungumza!
Nakuambia hata wewe ukiwa mwanabodi utanyamaza kimya tu, 🤣🤣🤣
 
TASAC ni taasisi ya uwakala wa meli Tanzania. Jana kwenye hotuba ya rais amegusia hiyo kuwa bodi ya TASAC imetumia zaidi ya milioni 600 kwa ajili ya vikao tu kwa mwaka.

Inafikirisha sana kwa nchi masikini kama Tanzania kutokea haya ambapo:

1. Watoto King'ong'o wanakaa chini
2. Dawa hazitoshi
3. Vyumba vya madarasa kila mwaka ni kero
4. Zahanati vijijini hakuna.
5. Watumishi wakipiga miayo kwa miaka 7

Juu ya haya yote watu wachache wana kutana kupiga soga na kutafuna zaidi ya milioni 600. Kuna tatizo kubwa kwenye mifumo yetu.

Pamoja na ukali wote wa hayati bado watu walidiriki kufanya haya. Kama nchi kuna sehemu tumefeli.

"Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"

KAZI IENDELEE
 
TASAC ni taasisi ya uwakala wa meli Tanzania. Jana kwenye hotuba ya rais amegusia hiyo kuwa bodi ya TASAC imetumia zaidi ya milioni 600 kwa ajili ya vikao tu kwa mwaka.
Inafikirisha sana kwa nchi masikini kama Tanzania kutokea haya ambapo:
1. Watoto King'ong'o wanakaa chini
2. Dawa hazitoshi
3. Vyumba vya madarasa kila mwaka ni kero
4. Zahanati vijijini hakuna.
5. Watumishi wakipiga miayo kwa miaka 7.
Juu ya haya yote watu wachache wana kutana kupiga soga na kutafuna zaidi ya milioni 600. Kuna tatizo kubwa kwenye mifumo yetu. Pamoja na ukali wote wa hayati bado watu walidiriki kufanya haya. Kama nchi kuna sehemu tumefeli.
"Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"
KAZI IENDELEE
IMG-20210406-WA0059.jpg
 
Kwahiyo kila kikao kilitumia hela hizi
26,086,956.5
Tasac hoyeee
 
Halafu MATAGA utawasikia "...amekata mirija ya upigaji, hakuna tena kupiga posho" and all similar nonsense huku wakisahau mirija iliyokatwa ni ya baba zao ile ya posho za 15K hadi 40K lakini wapiga posho za kuanzia 200K walikuwa wanapeta kama kawa!!
 
Hilo ni shirika moja tu, je yako mangapi ya aina hiyo ?
 
Back
Top Bottom