Kulikoni Makongo Juu?

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,012
Kulikoni Makongo Juu, mbona barabara ni mbaya na hapo Changanyikeni wametengenezewa vizuri na sisi tumeachwa?

Pili kuhusu maji:

Mabomba ya wachina yapo hadi mlangoni wenzetu wa Changanyikeni nasikia wanapata maji, KULIKONI MAKONGO JUU?

VIONGOZI MPO!?

TATIZO NI NINI?

Imetumwa na mdau Regina wa Makongo
 
Nimepata taarifa viongozi wenu wazubafu sana wamekaa Kiccm ccm tu wameridhika na hali halisi.
 
Nimepata taarifa viongozi wenu wazubafu sana wamekaa Kiccm ccm tu wameridhika na hali halisi.

Kweli panachefua - utafikiri ni kijiji kilomita 800 kutoka Dar. Ila wacha wafaidi matunda ya CCM! Halafu si huko si ndiko wanakoishi wazito wa CCM akina Yona, Mama Mongela, et.c. na 'middle class' wengi tu? Paradox!
 
Nimepata taarifa viongozi wenu wazubafu sana wamekaa Kiccm ccm tu wameridhika na hali halisi.
MMhm... Ni vema kwa wananchi wa eneo hilo kushiriki katika kutatua kero hiyo. Iwapo wataonyesha wazi kukerwa na tatizo hilo, hapana shaka vyombo husika vitatoa ushirikiano wa dhati.

Ni vema kutumia mikutano ya kata/tarafa kufikisha kero hiyo.

Fidel una hakika na hilo? Si ajabu wengi wa watu wa Makongo Juu, maji sio kero kubwa kwao..
 
WADAU napenda kujua yule mzee wa propoganda wa CCM AMEJIFICHA WAPI MBONA HATETEI TENA MAFISADI?HIZZA jitokeze jahazi linazama njoo useme chochote kama kawaida yako upo kimya sana
 
Kweli panachefua - utafikiri ni kijiji kilomita 800 kutoka Dar. Ila wacha wafaidi matunda ya CCM! Halafu si huko si ndiko wanakoishi wazito wa CCM akina Yona, Mama Mongela, et.c. na 'middle class' wengi tu? Paradox!

Yeah yaani hawa viongozi wapo tu imradi wamechanguliwa cha kusikitisha huko Makongo juu kuna vigogo kibao wanaishi huko wakichangishana harambee barabara ile inajengeka au wanataka aje JK ndo awahimize? Inakatisha tamaa na hao vibopa wameridhika na hali halisi.

MMhm... Ni vema kwa wananchi wa eneo hilo kushiriki katika kutatua kero hiyo. Iwapo wataonyesha wazi kukerwa na tatizo hilo, hapana shaka vyombo husika vitatoa ushirikiano wa dhati.

Ni vema kutumia mikutano ya kata/tarafa kufikisha kero hiyo.

Fidel una hakika na hilo? Si ajabu wengi wa watu wa Makongo Juu, maji sio kero kubwa kwao..

Wananchi wamelalamika mpaka wamechoka tatizo ni uongozi uliopo wa kiccm ccm na wewe Kibunango bana unajifanya kama chama chako hukijui au na wewe kuna vibonus unapata nn? Maana malengo makuu ya viongozi wa ccm sio kusaidia wananchi malengo yao ni kushibisha matumbo yao kwenye vikao ambavyo havina maana ajenda ndo hizo hizo kila wakati utekelezaji ndo hivyo wao wanashiba wananchi wanaendelea kusubiri.
Maji hili tatizo sugu kule mabomba mchina katandaza yamekuwa kama mapambo tu sasa hivi uliza nn kinacho kwamisha kuruhusu maji yatoke ni siasa tu bla bla kibao mpaka wanaingilia maswala ya kitaalamu.
 
..nikiwa kama mwana makongo juu mwenzio naungana na wewe katika hiki kilio!!! mi huwa nasema issue ya kwetu kuna mkono wa mtu..yaani miaka nenda rudi bara2 haiguswi hata kidogo....viongozi ni kama hawapo..damn!!!it really gets on my nerves...
 
Wana Makongo wameongea kwenye uchaguzi uliopita....diwani, mbunge wamepewa Chadema...hata kura za uraisi pia.....tunahitaji maendeleo bila kujali tuna kina nani kwani hawana msaada wowote....Mama yetu Mongela alifikia kutuambia kwamba jimbo lake ni UK, sasa tumtegemee aende akaishi huko...akibaki Makongo hatutamuelewa
 
Back
Top Bottom