Serikali ya Awamu ya Tano ilitoa utaratibu wa kuwezesha Watanzania kufungua mabucha ya wanyamapori mradi tu wawe wamefuata utaratibu. Hapa Mwanza kuna rafiki yangu alifuata taratibu zote na alianza kujenga bucha kwa gharama kubwa, alinunua gari ya kuwindia, alinunua bunduki ya aina yake kwa ajili ya kuwindia, alinunua mafriji kwa ajili ya kutunza nyama kutoka porini, alinunua mashine ya kukata nyama na vifaa vyote vinavyohitajika ili bucha yake ianze kazi.
Pamoja na kutimiza masharti yote alipigwa dana dana mpaka Rais wa Awamu ya Tano akafariki. Juzi nilipomuuliza kulikoni majibu niliyopata kwake yanasikitisha sana licha ya hasara kubwa aliyoingia. Yeye alinieleza kuwa vile vitalu ambavyo walitakiwa kwenda kuwinda tayari vimeishagawiwa na Serikali na hivyo hakuna yeyote atakayekuruhusu kuwinda kwenye kitalu chake. Aliendelea kunieleza kuwa awali nyati mmoja alitakiwa kuuzwa na Serikali kwa Tshs.600,000 sasa wenye vitalu ukitaka kumnunua nyati mmoja ni Tshs.1m/-. Anasema amepata hasara zaidi ya Tshs.150m/-. Tuiulize Serikali huu mradi nini hatma yake na kwa wale waliopata hasara watafidiwa?.