Kamanda Moshi
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 1,918
- 2,837
Habari za mchana wakuu,
Nimeandika kichwa cha habari hivo kilivyo ili kuvuta wahusika waone na kuchukua hatua ya hichi nitakachokieleza hapa chini.
Kwa sasa hapa jijini Dar es Salaam, unapopaki gari mjini unapewa risiti ya electronic ambayo inaonyesha number ya risiti kiasi kilichotozwa, jina la mlipaji na pia jina la mpokeaji.
Sina neno na mengine yote isipokuwa nina neno hapo kwenye mpokeaji. (KENYA AIRPORTS PARKING SERVICES LTD).
Jamani kabisa viongozi wetu na mamlaka husika mkakubali jina hilo liwekwe kwenye hiyo risiti? Sitaki kuamini kama kweli hamkuliona hilo, kweli kabisa jina la nchi nyingine linakuja kutokea kwenye risiti ya malipo halali ya nchi nyingine kweli kabisa viongozi wetu.
Uzalendo wenu upo wapi hapo? Au mmeamua kabisa kwa nafsi zenu na moyo wenu wote kumtangaza jirani, sasa mnashangaa nini jirani anaposema mlima Kilimanjaro upo kwake kama ninyi wenyewe mnashiriki kwenye kumkuza?
Mgeni/Mtalii anayekuja Dar es Salaam akapark gari kisha akapewa hii risiti mnadhani atafikiria nini? Jamani mnahosika angalieni hili jambo vizuri, kuweni makini na kinachosomeka kwenye risiti zitolewazo kwenye jamii, tena risiti kwa ajili ya malipo kwa serikali katika hili nafsi yangu imekataa kabisa, inaniuma na kuona tumekosa uzalendo kwa kiwango cha kimataifa.
Hii risiti ni nini inachofanya zaidi ya kuitangaza Kenya tena ndani kabisa ya kitovu cha nchi yetu? Na kama haya yametendeka hapa kwenye moyo wa nchi, si ajabu hata huko kwenye mbuga za wanyama watu wakawa wanapewa risiti zenye jina hili. Halafu eti tunalalamika watalii wanaenda Kenya...Ndio wataenda sana na wataendelea kuamini hapa Africa Mashariki kuna nchi moja tu - Kenya.
Naambatanisha na risiti husika kuonyesha haya maajabu yetu.
Nitakuwa Mzalendo Daima.- FITINA KWANGU MWIKO