Kulikoni gharama za tiba mbadala "herbal therapy" ni kubwa sana Tanzania?

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,057
10,715
Kwa kipindi sasa tumekuwa na hizi hospital zenye kutibu kwa miti shamba maarufu kama hospitali za tiba mbadala au herbal clinics.

Sina hakika sana taaluma za watoa huduma hizi japo wanajiita MADOKTA.

Ila Kinachoshangaza ni gharama kubwa wanazotoza kutoa huduma ikiwa ni pamoja na kuuza dawa hizo za miti shamba.
Yaani ukifikiria kwenda huko, kwa uchechefu sana uwe laki moja mfukoni.
 
Wamefanikiwa kuwaaminisha watu kuwa dawa zao ‘hazina madhara’ kiafya, pia wamefanikiwa kupotosha umma kuwa kuna ‘magonjwa sugu’ hayatibiki hospitali.... sasa wanawapiga kwelikweli.
 
Ni kama dini tuu.
Nguvu ya ushawishi na imani za wagonjwa
 
mkuu hujui dawa zinavyopatikana ,kuna wakati hukesha misituni kuchimba dawa hasa kwenye mikoa ya baridi na wanyama wakali niliwahi kumsaidia mjomba hii kazi mazingira mengine siwezi kuelezea yalivyo hatarishi ila ujue sio kazi rahisi kutibu magonjwa yaliyoshindikana hospital japokuwa tabibu mkuu ni Mungu.
ungekuwa wewe ungeuza hata milioni kwa dose.
 
Back
Top Bottom