Kulikoni Chuo Kikuu SAUT Mwanza Kumzuia Tundu Lissu kutoa mhadhara??!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kulikoni Chuo Kikuu SAUT Mwanza Kumzuia Tundu Lissu kutoa mhadhara??!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sajenti, Mar 1, 2012.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Leo asubuhi nimesikia habari Radio Free Afrika kuwa mwanasiasa machachari kutoka CHADEMA Tundu Lissu aliomba kufanya mhadhara katika viunga vya chuo kikuu SAUT Mwanza. hata hivyo hilo halikufanikiwa baada ya uongozi wa chuo hicho kumueleza Lissu kuwa endapo alitaa kufanya mhadhara huo basi condition mojawapo ni kumtaka akubali viongozi wa CCM waalikwe.

  Baada ya majadiliano ya muda mrefu na Mh. Lissu kuubana uongozi wa SAUT ilibainika kuwa uongozi wa chuo ulipata maelekezo kutoka kwa "wanaojiita usalama wa taifa" kuwa mwanasiasa huyo asiruhusiwe kufanya mhadhara huo.

  Akihojiwa na mwandishi wa habari wa RFA, Lissu alionyesha masikitiko yake kwa uongozi wa taasisi kubwa ya kisomi kama SAUT kuzuia wanafunzi kupata haki yao ya kusikiliza na kutoa maoni yao na hasa katika kipindi hiki ambacho Tanzania inapita katika mchakato wa kupata katiba mpya.

  Baadhi ya wanafunzi wa SAUT nao wakihojiwa waliulaumu sana uongozii wa chuo chao kukubali kuburuzwa na CCM na pia kuwanyima wao kama wasomi wa chuo kikuu kupata nafasi kumsikiliza mwanasiasa huyo na wao kupata nafasi kushiriki katika mhadharo huo.

  My take: CCM ni zaidi uijuavyo!!
   
 2. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2012
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  acha kudanganya umma wewe,unamjua kitima unamsikia?,unajua wakatoliki unawasikia?,usalama si chochote mbele yao,zaidi vc kitima na lissu ni marafiki sana ata kwenye kampen alimsaidia sana.kile chuo si cha kisiasa wapo kikazi bila kujal4 8zama
   
 3. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Acha weweee usiongee usichojua...wakati wa mgomo wa maDaktari walikuwa wakikutana kwenye ukumbi wa Don Bosco Upanga kwa malipo ya Tshs zaidi ya laki 3 kwa siku, na hakuna hata siku moja walishindwa kulipa. Siku moja ghafla viongozi wa kamati ya maDaktari walitaka kulipia kwa ajili ya mwendelezo wa mikutano kesho yake chasier akakataa kuchukua hela, msimamizi wa kituo akakataa madaktari kuendelea kukutana hapo kwa kupokea maelekezo toka uongozi wa juu wa kanisa katoliki!! Ikalazimu maDaktari kuhamia Star Light hotel...makanisa yanapokea maelekezo toka kwa intelijensia kuwabana wanaharakati na yanafanya hivyo!
   
 4. don-oba

  don-oba JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 1,384
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Huyu alotuma thread hii kweli hamjui Kitima, jamaa ana misimamo thabiti kuipinga serikali. Alishawahi itwa ikulu akaambiwa apunguze kelele, akadai aachi ng'o hata akipewa sumu. Ni mkuu gani wa chuo hapa nchini anaweza kusimama kuipinga serikali?. Kwa taarifa ako Kitima na Lissu wanatoka eneo moja na ni kabira moja. Hapa kilichotokea, ni mkuu department ya LAW mr Kilangi kuzuia. Kitima alikua hajui. Hata ivyo alimwaga cheche kwenye ofisi za CDM tawi la SAUT. Hebu ingia kwenye thread yangu usome nondo.
   
 5. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  Kwan kanisa katoliki si ndio hao hao ccm mafixadi wew huoni edward lowasa anavyozunguka makanisan na kupiga harambee kibao??

  Popote penye nia pana njia na siku zote ukweli hujitenga.
  Pamoja sana kamanda LISU ungekubali tu ufanye nao hao mapapa wa ccm kwan wanachuo wenyewe wanajua mchele ni upi na mchanga ni upi??

  Naona wanajitahidi kuzuia kusambaa kwa moshi kwa kuufunika na shuku.
   
 6. Mchochezi

  Mchochezi JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 6,952
  Likes Received: 1,155
  Trophy Points: 280
  kitima nae ni mamluki tuu wa jakaya
   
 7. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  hawa viongozi wa SAUT nao wanakuwa kama watoto wadogo-wanaendeshwa endeshwa tu-hawana maana
   
 8. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  lakini kwa kile alichokifanya lissu pale kwenye ofisi za cdm tawi la SAUT,sio siri alizisuuza nyoyo za vijana wa chuo hiki,mpaka saa mbili usiku vijana walikuwa tuliii wakimsikiliza.Bravo cdm,bravo lissu
   
 9. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chuo hicho ni cha CCM na Wakatoliki siku hizi wananyemelea hela za Lowasa wasingeweza kumuudhi Lowasa, Wakatoliki wameamua kujidhalilisha na viharambee vya kifisadi. Na wanakoelekea hawatakuwa tena na NGUVU ya kukemea ufisadi nchi hii, MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
 10. K

  Kiboko Yenu JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 312
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hapa ndio napata neno lile la tundu na sifa za kijinga jana ilikuwa siku ya masomo yeye kiherehere kwenda kuhutubia
   
Loading...