Kulikoni chuo kikuu muhimbili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kulikoni chuo kikuu muhimbili?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by drgeorge, Jul 14, 2011.

 1. d

  drgeorge Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani hivi leo tar 14.07.2011 katka chuo kikuu cha Muhimbili kuna polisi kutoka kituo cha Polisi Salender bridge kwa kushirikiana na auxillary polisi wa MUhimbili walitaka kuwakamata baadhi ya wanafunzi ili wawapeleke katika kituo hicho cha Polisi eti wakatoe maelezo kwa kinachodaiwa kwamba wameshitakiwa na baadhi ya wanafunzi wenzao.

  hakukua na RB, haijulikani kosa ni nini, hajulikani aliyeshitaki ni nani, haijulikani dhahiri kama kweli wanapelekwa polis au n sehemu nyingine, ila uongozi wa chuo ukaanza kuandaa gari ili kuwasidikiza wanafunzi hao. Na ifahamike kuwa kuna kesi imefunguliwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania-Dar es salaam kuhusu kufutwa kwa chama cha wanafunzi MUHASSO

  wanafunzi hawakuweza kwenda kwa sababu utaratibu wa kuwakama haueleweki. Halafu kihistoria wanafunzi hao wote waliwahi kuwa viongozi wa serkali ya wanafunzi MUHASSO, mmojawao ni aliyekuwa rais ambaye chama kilifutwa kipindi chake.

  Kwa kifupi haieleweki ila dalili na hali inavyoonesha inawezekana ni namna ya kutafuta kubambikiza kesi, haya n i mawazo yangu tu, ila naombeni wadau kutolipuuzia hili, hasa wanasheria tunahitaji msaada wa hali ya juu. watatu kati ya wanafunzi hao ni mwaka wa 5 udaktari, bado wki nne wamalize chuo. Inaniuma sana!! Asanteni.
   
 2. L

  Luiz JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Cjakuelewa kidogo mkuu kwani wameshakamatwa? Au walitaka kukamatwa?
   
 3. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135


  Kama unasomea udaktari sioni tofauti yako na walio fanya operation ya kichwa badala ya miguu.
  """"Soma hizo sentensi zinavyochanganya,mara wamekamatwa,mara hawakupelekwa,.........walitaka kuwakamata baadhi ya wanafunzi............
  ..
  hakukua na RB, haijulikani kosa ni nini, hajulikani aliyeshitaki ni nani....haijulikani dhahiri kama kweli wanapelekwa polis au n sehemu nyingine.............ni namna ya kutafuta kubambikiza kesi,........... haya n i mawazo yangu tu....."""""

  na ww ni mmojawapo??? andika kitu kinachoeleweka!
   
Loading...