Kulikoni CHADEMA baadhi ya wagombea majmboni kutorudisha fomu?!

.
So Maane what do you expect wapinzani wangefanya? Wananchi kule wamekuwa wanapata kile ambacho serikali ilipaswa kuwapa.........so hakuna agenda kwa wapinzani!

Next level, ... inauma sana pale unapokuta mtu anakwenda kuielezea jamii yake tofauti na uhalisia ilhali anajua fika jamii hiyo haiko hivyo kama anavyosema. Ndivyo unavyofanya wewe, ndivyo wanafanya CCM, ndivyo wanavyofanya viongozi wa CCM na ndivyo alivyofanya yule kijana aliyeambiwa na watu makini nyakati tofauti kuwa "hana hadhi ya kujibizana na mimi" anavyofanya.

Hivi ni kweli kuwa watu wa Njombe wanapata kitu kile wanachohitaji toka kwa serikali?
Hivi kweli nikienda Ngalanga hata kabla ya kwenda Uwemba, Lusitu ama Kifanya au Magoda unachosema nitakiona? Nitakuthibitisha kuwa mkweli?

Unatutaka tukuamini.... mmhhh.

Najua kuwa huyu bibi anavibaraka wengi wengine ni "waandishi" wa habari. Na wewe upo kwenye list?

Tafadhari nijibu.
 
ndo hapo mnatakiwa kutuelewa tunapopiga piga chini wagombea wasio na malengo na mapandikizi ya CHICHIEM

inawezekana pia kuwa jamaa walilazimika kuuza fomu kwa wagombea wa chichiem. Ufisadi na usaliti wa hali ya juu.
 
watakuja na maelezo ya ccm ndio wachawi.....mimi binafsi ningependa kuona demokrasia inakuwa na wapinzani wanapata nafasi hasa katika kata na majimbo (haimaanishi sitaki wapate rais). lakini naona baado. Binafsi siwasanifu kwa janga hili ila naona ambavyo bado tuna safari katika mageuzi ya siasa za tz. naamini si kosa la kiutendaji hili...hapa kuna shida ya mgombea mwenyewe sijajua though ni ipi..kuna shida ya baadhi (si lazima hawa ambao hawakurudisha fomu) ya wachumia tumbo kukubali kununuliwa ili kuuza jimbo...bado tuna njaaa bado tunataka demokrasi kidogo ina challenge sana. Nimewahi kusikia mgombea fulani alikuwa anauza ushindi wake kila uchaguzi kwa kukubali kusaini matokeo ya kushindwa ilhali anajua ameshinda...big shame! watu bado hawajajua wanataka nini lol
mix with yours
 
....mkuu in very brief, wapinzani kule wamegwaya! Mama was very smart tangia mwaka 2006 one year baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge.....matatizo ya kule hasa hasa ni pembejeo za kilimo (viazi na mahindi) hasa na barabara kidogo sana.....!

Sasa tangia mwaka 2006 mama alihakikisha kuwa kila kaya inapata ile mbolea na ruzuku, madawa ya ukungu, na pia ma bwana shamba kule kwetu hawakauki (tangia 2006).

Kila ifikikapo msimu wa kilimo kila mkulima huandikisha jina na kusema ni nini anataka eg mbolea mifuko 2 (dap,can,urea) na ridomil(very crucial hii kwa ukungu-viazi)! Wanapoanza kupanda mazao malori hupeleka kule mbolea na madawa na wakulima wanagawiwa bureeeeee.....free of cost...trust me!

Barabara kila baada ya miezi mitatu hivi inashindiliwa...so wakulima wanauhakika kupitisha mazao yao muda wowote katika mwaka......!

Tatu...kama utakumbuka issue ya lumbesa ilianzia njombe...mama alitupa hii kitu kwenye council ya halmashauri....ikapigwa moto hadi ngazi ya mkoa, then hadi taifani....ukaona kina wasira wanashikia bango.....! So sikuhizo unyonywaji wawakulima uliokuwa unafanywa na walanguzi hakuna siku hizi.....!

Kuna issue ya shule.....hili nalo si tatizo sana kule!

So maane what do you expect wapinzani wangefanya? Wananchi kule wamekuwa wanapata kile ambacho serikali ilipaswa kuwapa.........so hakuna agenda kwa wapinzani!

ccm hoyeeee........... Mama anna makinda hoyeee
 
Next level, ... inauma sana pale unapokuta mtu anakwenda kuielezea jamii yake tofauti na uhalisia ilhali anajua fika jamii hiyo haiko hivyo kama anavyosema. Ndivyo unavyofanya wewe, ndivyo wanafanya CCM, ndivyo wanavyofanya viongozi wa CCM na ndivyo alivyofanya yule kijana aliyeambiwa na watu makini nyakati tofauti kuwa "hana hadhi ya kujibizana na mimi" anavyofanya.

Hivi ni kweli kuwa watu wa Njombe wanapata kitu kile wanachohitaji toka kwa serikali?
Hivi kweli nikienda Ngalanga hata kabla ya kwenda Uwemba, Lusitu ama Kifanya au Magoda unachosema nitakiona? Nitakuthibitisha kuwa mkweli?

Unatutaka tukuamini.... mmhhh.

Najua kuwa huyu bibi anavibaraka wengi wengine ni "waandishi" wa habari. Na wewe upo kwenye list?

Tafadhari nijibu.

Unaishi wapi wewe? kwa mara ya mwisho umeenda lini Njombe Kusini?

Kwa taarifa yako mimi si mwanachama wa chama chochote, si mwandishi wa habari, sina kambi yeyote ile.....ila ni mpenda maendeleo wa kweli so pale yanapofanyika mazuri nasema hivyo! niliyoyasema niyale niliyoyaona kwa macho yangu mwenyewe!

Nenda vijiji vya Makowo, Mbega, Matola, Mtila, Kona/Makoga, Luponde, Lusitu.......utayaona hayo niliyoyasema hapo juu! Yes Jimbo la Njombe kusini ni kubwa ofcourse inawezekana kuna baadhi ya vijiji kuna mapungufu....lakini hivyo vijiji nilivyokutajia hapo nina uhakika na ninachokisema!

Usizungumzie Njombe kama Wilaya, hapa nazungumzia Jimbo la Njombe Kusini...lenye Kata za Matola, Makowo(mpya), Luponde, Uwemba, Njombe Mjini, Igominyi etc! binafsi natokea Jimbo hilo......na hayo niliyoyasema nimeyaona kwa macho yangu! ofcourse binafsi nilishangazwa sana!

Kama ukitaka kupata ukweli zaidi jaribu kumpigia Mr. Mwalongo, diwani wa kata ya Matola na MEYA wa mji wa Njombe...kama ukitaka sema nikupe Namba zake....he will tell you the same!

Usije ukawa kama tuliowengi tunakaa tu dar es Salaam na kuchallenge hewani hewani tu bila kuwa na data from the ground...jaribu kutembelea kule home uone exactly what is happening there currently! Muulize Bw. Msemwa kilimpata nini kwenye kura za maoni.....!

Need I say more......! with evidence!
 
Wakuu leo nimesikia asubuhi katika radio Wapo kuwa kuna baadhi ya majimbo wagombea ubunge wa CHADEMA hawakurejesha fomu zao hadi ilipofika jana kwa muda waliotakiwa.

Majimbo hayo ni pamoja na lile la Isimani kwa mh. Lukuvi na la Anna Makinda. Pia mengine sikuweza kuyapata maana nilipatwa na mshangao.

CHADEMA jitokezeni hapa mtueleweshe yaliyowasibu wanachama wenu hawa tena viongozi huko waliko na hawakurejesha fomu??!!

Je hii inaashiria nini?

Naamini mmeanza vizuri na ni vema mmalize vizuri. Msitoe nafasi ya changamoto kwa wagombea wengine. Kinachotakiwa ni kuongeza idadi ya wabunge mjengoni!!

Mkuu hoja yako ni ya msingi sana, na umemalizia katika shabaha ya msingi sana kitu kile CHADEMA wanachotakiwa kuangalia toka awali. Kwa ufupi naomba nikujibu hivi; rejea kitu kilichofanyika Mbeya katika uchaguzi mdogo pale mgobea wa CHDEMA aliposhindwa kushiriki kutokana na disari katika kujaza viapo katika fomu aliyoichukua na hata urudishaji wake. viongozi wa CHADEMA walisema watafanya uchunguzi kujua nani alihusika katika kuifanya dosari ile itokee wakijua wazi wao ndiyo walikuwa na nafasi ya kushinda na si CCM. Utakumbuka na namna watu walivyouziria uchaguzi ule.

Huo ni mchezo mchafu wa CCM kwa upande mmoja na kwa upande mwingine ni kutokujiamini ama kuogopa kushindwa kwa wagombea toka upinzani.

Mchezo mchafu ki namna gani? CCM wanatumia pesa chafu kuwaonga wagombea wa upinzani ambao hali zao kiuchumi si njema ...ni ukweli usiopingika... kwamba ajitoe atapewa fedha kadhaa, ama jaza fomu kimakosa sis tutaweka pingamizi lakini wewe tutakupa mshiko wako, ama anapewa fedha au nyumba halafu wakati wa kampeni anafanya maloroso hata kuwaudhi wapiga kura mwisho hachaguliwi, ama kufanaya lolote lile litakalo mfanya aonekane mgombea dhaifi na watu kumpuuzia. Yote insababishwa na fedha chafu.

Kimefanyika sehemu nyingi tanzania, Na ndiyo maana utakumbuka Alatanga Nyagawa baada ya kumkimbiza sana Makweta katika uchaguzi wa 2005, alihongwa na kutakiwa arudi CCM kutoka TLP akiahidiwa kuwa mwaka huu utakuwa wake baada ya MAkweta. Haikuwa hivyo na hadithi bado inaendelea... baada ya kubwagwa CCM amekimbilia CHADEMA sasa.

Ninawajua wagombea udiwani wawili wa CHADEMA ambao baada kuonekana tishio kwa wapinzani wao mmoja ameombwa ajitoe atepewa gari jipya toka "show room" na huyu wa pili asingizie afya yake imekuwa si njema ajitoe atapewa milioni 30. Kizuri nikuwa wote msimamo wao ni kuwa "HATUDANGANYIKI" mbele kwa mbele mpaka kieleweke.
 
inawezekana pia kuwa jamaa walilazimika kuuza fomu kwa wagombea wa chichiem. Ufisadi na usaliti wa hali ya juu.

hata chadema wanapokea pesa za mafisadi hadi kuuza fomu kwa wagombea wa CCM. Nichama kipi cha kukiamini!!!!!!!!!
 
Mkuu hoja yako ni ya msingi sana, na umemalizia katika shabaha ya msingi sana kitu kile CHADEMA wanachotakiwa kuangalia toka awali. Kwa ufupi naomba nikujibu hivi; rejea kitu kilichofanyika Mbeya katika uchaguzi mdogo pale mgobea wa CHDEMA aliposhindwa kushiriki kutokana na disari katika kujaza viapo katika fomu aliyoichukua na hata urudishaji wake. viongozi wa CHADEMA walisema watafanya uchunguzi kujua nani alihusika katika kuifanya dosari ile itokee wakijua wazi wao ndiyo walikuwa na nafasi ya kushinda na si CCM. Utakumbuka na namna watu walivyouziria uchaguzi ule.

Huo ni mchezo mchafu wa CCM kwa upande mmoja na kwa upande mwingine ni kutokujiamini ama kuogopa kushindwa kwa wagombea toka upinzani.

Mchezo mchafu ki namna gani? CCM wanatumia pesa chafu kuwaonga wagombea wa upinzani ambao hali zao kiuchumi si njema ...ni ukweli usiopingika... kwamba ajitoe atapewa fedha kadhaa, ama jaza fomu kimakosa sis tutaweka pingamizi lakini wewe tutakupa mshiko wako, ama anapewa fedha au nyumba halafu wakati wa kampeni anafanya maloroso hata kuwaudhi wapiga kura mwisho hachaguliwi, ama kufanaya lolote lile litakalo mfanya aonekane mgombea dhaifi na watu kumpuuzia. Yote insababishwa na fedha chafu.

Kimefanyika sehemu nyingi tanzania, Na ndiyo maana utakumbuka Alatanga Nyagawa baada ya kumkimbiza sana Makweta katika uchaguzi wa 2005, alihongwa na kutakiwa arudi CCM kutoka TLP akiahidiwa kuwa mwaka huu utakuwa wake baada ya MAkweta. Haikuwa hivyo na hadithi bado inaendelea... baada ya kubwagwa CCM amekimbilia CHADEMA sasa.

Ninawajua wagombea udiwani wawili wa CHADEMA ambao baada kuonekana tishio kwa wapinzani wao mmoja ameombwa ajitoe atepewa gari jipya toka "show room" na huyu wa pili asingizie afya yake imekuwa si njema ajitoe atapewa milioni 30. Kizuri nikuwa wote msimamo wao ni kuwa "HATUDANGANYIKI" mbele kwa mbele mpaka kieleweke.

Ndugu mwenye mawazo nimekubaliana na mawazo yako hapo juu.....! Sasa hapo nilipohiglight ndicho kilichotokea Njombe kusini kwa Makinda sawa.....?
 
Unaishi wapi wewe? kwa mara ya mwisho umeenda lini Njombe Kusini?

Kwa taarifa yako mimi si mwanachama wa chama chochote, si mwandishi wa habari, sina kambi yeyote ile.....ila ni mpenda maendeleo wa kweli so pale yanapofanyika mazuri nasema hivyo! niliyoyasema niyale niliyoyaona kwa macho yangu mwenyewe!

Nenda vijiji vya Makowo, Mbega, Matola, Mtila, Kona/Makoga, Luponde, Lusitu.......utayaona hayo niliyoyasema hapo juu! Yes Jimbo la Njombe kusini ni kubwa ofcourse inawezekana kuna baadhi ya vijiji kuna mapungufu....lakini hivyo vijiji nilivyokutajia hapo nina uhakika na ninachokisema!

Usizungumzie Njombe kama Wilaya, hapa nazungumzia Jimbo la Njombe Kusini...lenye Kata za Matola, Makowo(mpya), Luponde, Uwemba, Njombe Mjini, Igominyi etc! binafsi natokea Jimbo hilo......na hayo niliyoyasema nimeyaona kwa macho yangu! ofcourse binafsi nilishangazwa sana!

Kama ukitaka kupata ukweli zaidi jaribu kumpigia Mr. Mwalongo, diwani wa kata ya Matola na MEYA wa mji wa Njombe...kama ukitaka sema nikupe Namba zake....he will tell you the same!

Usije ukawa kama tuliowengi tunakaa tu dar es Salaam na kuchallenge hewani hewani tu bila kuwa na data from the ground...jaribu kutembelea kule home uone exactly what is happening there currently! Muulize Bw. Msemwa kilimpata nini kwenye kura za maoni.....!

Need I say more......! with evidence!

Naisoma signature yako tena na tena, inabeba maana kubwa sana lakini hutaki kuona. Sawa unaangalia na umesikia lakini hutaki kuona.
Tuliza munkari.
Uliyemtaja huyo Mwalongo ni kibaraka wa Anna. makinda anajua hana ushawishi wowote si kwao yaani kwa baba yake Yakobi na kanada za Uwemab hadi Luponde. hivyo amemtumia Mwalongo amsaidie katika ukanda wa njia ya Luponde, Kona, Matola.

Kwa Yakobi, Anna, nguvu yake ipo kwa Mzee(nalihifadhi jina lake) aliyekuwa anaheshimiana sana na Mzee Makinda mwenyewe. Mzee huyu anakubalika sana pale Yakobi kwani aliwahi kuwa Mzee wa kanisa KKKT la pale. Yeye kama yeye, Anna hana ushawishi. walimdharau zaidi pale alipokuja na MAKINDA CUP .. fuatilia matokeo yake.

Jambo jingine hujui ni madadu gani ambayo yalifanyika Halmashauri ikaandikwa ripoti feki, wanachi walimwambia Makinda lakini kwasabababu Mwalongo alihusika katika ulaji limekuwa kimya. Dodoma TAMISEMI wanaripoti yenye kuonyesha kuna miradi imekamilika. Nenda Njombe hakuna mrdai uliokamilika kwenye hiyo ripoti.

Acha kusema kitu ambacho hutaki kukiona unaangalia tu.
 
Mnyamahodzo,

Sema nikupe facts zingine au unaenda na wewe kukusanya data? Kama umeridhika, nitake radhi kwa kunisema vibaya kwenye post yako ya kwanza kny thread hii......!
 
Kilichotokea jimboni Chunya kwa mfano:Mwanachama mmoja wa CHADEMA alienda kuchukua form ya ubunge kwa tiketi ya CHADEMA,Uongozi wa mkoa wa CHADEMA ukamuwekea pingamizi kwamba sio chaguo lao na watasimamisha mgombea mwingie... TIA MAJI,TIA MAJI SIKU YA KURUDISHA FORM HII HAPA... CHADEMA haikupeleka mbadala wa yule waliyemuwekea pingamizi!
 
Unaishi wapi wewe? kwa mara ya mwisho umeenda lini Njombe Kusini?

Kwa taarifa yako mimi si mwanachama wa chama chochote, si mwandishi wa habari, sina kambi yeyote ile.....ila ni mpenda maendeleo wa kweli so pale yanapofanyika mazuri nasema hivyo! niliyoyasema niyale niliyoyaona kwa macho yangu mwenyewe!

Nenda vijiji vya Makowo, Mbega, Matola, Mtila, Kona/Makoga, Luponde, Lusitu.......utayaona hayo niliyoyasema hapo juu! Yes Jimbo la Njombe kusini ni kubwa ofcourse inawezekana kuna baadhi ya vijiji kuna mapungufu....lakini hivyo vijiji nilivyokutajia hapo nina uhakika na ninachokisema!

Usizungumzie Njombe kama Wilaya, hapa nazungumzia Jimbo la Njombe Kusini...lenye Kata za Matola, Makowo(mpya), Luponde, Uwemba, Njombe Mjini, Igominyi etc! binafsi natokea Jimbo hilo......na hayo niliyoyasema nimeyaona kwa macho yangu! ofcourse binafsi nilishangazwa sana!

Kama ukitaka kupata ukweli zaidi jaribu kumpigia Mr. Mwalongo, diwani wa kata ya Matola na MEYA wa mji wa Njombe...kama ukitaka sema nikupe Namba zake....he will tell you the same!

Usije ukawa kama tuliowengi tunakaa tu dar es Salaam na kuchallenge hewani hewani tu bila kuwa na data from the ground...jaribu kutembelea kule home uone exactly what is happening there currently! Muulize Bw. Msemwa kilimpata nini kwenye kura za maoni.....!

Need I say more......! with evidence!

NL mbona unakuja naushahidi kuthibitisha kile nilichosema. Mwalongo ni kibaraka wa Anna. Anna hana ushawishi kanda ya LUPONDE, Kona Matola. Naomba rudi nyuma kawaulize waliokuambia kwa maneno haya "Hivi Makinda alimfunikia Mwalongo kashfa gani ambayo ripoti yake ya uongo imekwenda TAMISEMI-Dodoma kwamba pesa zimetumika kiusahihi kwa miradi iliyokusudiwa ?"

Next L, tafadhari usiangalie tu jaribu kujitahidi kuona. Then, utasema ninachojua, ninakijua.
 
Kilichotokea jimboni Chunya kwa mfano:Mwanachama mmoja wa CHADEMA alienda kuchukua form ya ubunge kwa tiketi ya CHADEMA,Uongozi wa mkoa wa CHADEMA ukamuwekea pingamizi kwamba sio chaguo lao na watasimamisha mgombea mwingie... TIA MAJI,TIA MAJI SIKU YA KURUDISHA FORM HII HAPA... CHADEMA haikupeleka mbadala wa yule waliyemuwekea pingamizi!

Kweli haya?
 
Naisoma signature yako tena na tena, inabeba maana kubwa sana lakini hutaki kuona. Sawa unaangalia na umesikia lakini hutaki kuona.

..ok naangalia......sioni.....wewe unaona nini? nilivyoviona nimevitaja na ndivyo msingi wa hoja yangu kwamba wapinzani ndiyo sababu ya kugwaya.....wameshindwa kujenga hoja yenye nguvu.....niambie ulichokiona wewe au hata kusikia?

Tuliza munkari.
...mimi sio CUF okay!

Uliyemtaja huyo Mwalongo ni kibaraka wa Anna. makinda anajua hana ushawishi wowote si kwao yaani kwa baba yake Yakobi na kanada za Uwemab hadi Luponde. hivyo amemtumia Mwalongo amsaidie katika ukanda wa njia ya Luponde, Kona, Matola.
.....ooh my God! umeanza kuja kwenye hoja yangu...so which means Mwalongo anakubalika huko sio? so is like Mwalongo ni messanger wa Makinda sio? anachokifanya Mwalongo kuna mkono wa Makinda sio? so mazuri yote anayofanya Mwalongo kule Matola, Mbega, Mamongoro, Idihani yana mkono wa Makinda sio? sasa wewe unabisha nini hapa? mimi sio mwanasiasa, mimi nimeleta facts ya yale niliyoyaona ambayo wanancho wanafurahia.....! sasa kama Mwalongo ni kibaraka hapa ni immaterial point.....hoja ni kuwa kuna mambo yamefanyika kule na yamewafurahisha wananchi kwa level ya uelewa wao! sasa kama kuna ukibaraka hapo mimi hilo halinihusu......!

Kwa Yakobi, Anna, nguvu yake ipo kwa Mzee(nalihifadhi jina lake) aliyekuwa anaheshimiana sana na Mzee Makinda mwenyewe. Mzee huyu anakubalika sana pale Yakobi kwani aliwahi kuwa Mzee wa kanisa KKKT la pale. Yeye kama yeye, Anna hana ushawishi. walimdharau zaidi pale alipokuja na MAKINDA CUP .. fuatilia matokeo yake.
....wewe unaleta mambo taarab ndugu yangu, hizo hadithi zilikuwepo sana mwaka 1995 vs Ngunangwa....hoja ya ushawishi inakujaje hapa? is it necessary kuwa na ushawishi? watu wanataka matendo zaidi sio maneno ya kushawishi mjomba.....! watu wanataka DAP, RIDOMIL, CAN, UREA na wamepewa sasa unataka washawishiwe vipi wewe?

Jambo jingine hujui ni madadu gani ambayo yalifanyika Halmashauri ikaandikwa ripoti feki, wanachi walimwambia Makinda lakini kwasabababu Mwalongo alihusika katika ulaji limekuwa kimya.

Sasa hii ni issue ingine ambayo ilitakiwa uipoint kama una details zake kama mimi nilivyokuwa na details za watu kugawiwa pembejeo......sikubishii coz sijaisikia hii....! thanks for this!
Dodoma TAMISEMI wanaripoti yenye kuonyesha kuna miradi imekamilika. Nenda Njombe hakuna mrdai uliokamilika kwenye hiyo ripoti.
...inawezekana miradi haijakamilika kama ilivyooneshwa kny hiyo report, lakini kuna miradi ambayo personnally nimeona imekamilika......so don't generalize things mkuu!

Acha kusema kitu ambacho hutaki kukiona unaangalia tu
.No homu boi.....mimi si mwanasiasa, so nasema kile nilichokiona mzee wangu....sasa kama sijakisema kisiasa hilo halinihusu......! ila wewe naona unabukua tu na umejaa nadharia kule home hutembelei mara kwa mara...CPU yako haina updates za kutosha....! jamani tembeleeni kwenu mpate updates....Lol!
 
Mkuu hoja yako ni ya msingi sana, na umemalizia katika shabaha ya msingi sana kitu kile CHADEMA wanachotakiwa kuangalia toka awali. Kwa ufupi naomba nikujibu hivi; rejea kitu kilichofanyika Mbeya katika uchaguzi mdogo pale mgobea wa CHDEMA aliposhindwa kushiriki kutokana na disari katika kujaza viapo katika fomu aliyoichukua na hata urudishaji wake. viongozi wa CHADEMA walisema watafanya uchunguzi kujua nani alihusika katika kuifanya dosari ile itokee wakijua wazi wao ndiyo walikuwa na nafasi ya kushinda na si CCM. Utakumbuka na namna watu walivyouziria uchaguzi ule.

Huo ni mchezo mchafu wa CCM kwa upande mmoja na kwa upande mwingine ni kutokujiamini ama kuogopa kushindwa kwa wagombea toka upinzani.

Mchezo mchafu ki namna gani? CCM wanatumia pesa chafu kuwaonga wagombea wa upinzani ambao hali zao kiuchumi si njema ...ni ukweli usiopingika... kwamba ajitoe atapewa fedha kadhaa, ama jaza fomu kimakosa sis tutaweka pingamizi lakini wewe tutakupa mshiko wako, ama anapewa fedha au nyumba halafu wakati wa kampeni anafanya maloroso hata kuwaudhi wapiga kura mwisho hachaguliwi, ama kufanaya lolote lile litakalo mfanya aonekane mgombea dhaifi na watu kumpuuzia. Yote insababishwa na fedha chafu.

Kimefanyika sehemu nyingi tanzania, Na ndiyo maana utakumbuka Alatanga Nyagawa baada ya kumkimbiza sana Makweta katika uchaguzi wa 2005, alihongwa na kutakiwa arudi CCM kutoka TLP akiahidiwa kuwa mwaka huu utakuwa wake baada ya MAkweta. Haikuwa hivyo na hadithi bado inaendelea... baada ya kubwagwa CCM amekimbilia CHADEMA sasa.

Ninawajua wagombea udiwani wawili wa CHADEMA ambao baada kuonekanama ajitoe atapewa milioni 30. Kizuri nikuwa wote msimamo wao ni kuwa "HATUDANGANYIKI" mbele kwa mbele mpaka kielewektishio kwa wapinzani wao mmoja ameombwa ajitoe atepewa gari jipya toka "show room" na huyu wa pili asingizie afya yake imekuwa si nje

e.

Nadhani umekosea huu ni mchezo mchafu wa CHADEMA WA KUPOKEA HELA CHAFU ZA CCM
UTAPELI NA KUPENDA RUSHWA SI tabia ya CHAMA NI TABIA ZA MTU AWE CHADEMA, CUF, CCM, TGNP, KWA KAKOBE, KWA SHEHE MKUU, MAKANISANI NA KWA WAGANGA WA KIENYEJI
Ndio maana napingana sana na watu humu ndani wanaojaribu kujifanya wao pekeee ndio watakaoleta ukombozi nchi hii ni uwongo
watanzania bila kujali sura, chama, kimo na umri wengi wao ni MATAPELI/WENGI WETU NI MATAPELI WA KUZALIWA NA KURITHI

Tuogope watumishi wa Mungu!
 
Mnyamahodzo,

Sema nikupe facts zingine au unaenda na wewe kukusanya data? Kama umeridhika, nitake radhi kwa kunisema vibaya kwenye post yako ya kwanza kny thread hii......!

Tafadhari naomba usiwe na Munkari kiasi hicho kuwa mtaratibu. Sijakusema vibaya. nimesema ukweli. Kama nawe umo ndani, utang'aka. Kitu kizuri ni kuwa facts za kuniambia barabara zinatengenezwa kila baada ya miezi mitatu, au kuanzisha MAKINDA CUP, au kuwapatia vyerehani 60 wale wakinamama wa vijiji kadhaa(kijiji kimojawapo walipewa 2) ziwaendeleze wakinamama hawa wakitanzania. Facts za namna mwalivyojiandikisha majina kwa ajili ya mbolea ya ruzuku halafu wasiopate walichoomba na mbolea kuuzwa mkoa mwingine?
Facts ya kuwataka wanachi wajenge dispensary halafu nurse Glade B (sawa na wa RED Cross) ndiyo mkuu wa kituo, tabibu, nurse, na mgawa dawa vyote yeye? nikubaliane nazo hizo.

Sijui uko Njombe kweli au uko Pwani? Unajua wewe ulipo. Kikubwa ielzee ukweli hali ya Njombe na kitu kile huyu mama alichofanya kwa watu wa Njombe; ametumia ukimya wao na uoga wao kuwakandamiza.

Jivunie; Anna makinda amewafanyia nini watu wa Njombe Kusini for 15 years? ainisha kinagaubaga.
 
Hii inaashiria kwamba CHADEMA bado hawana mtandao wa kutosha kuunda serikali kama watashinda Urais hivyo ni mapema sana kuwapatia dola wakati wanashindwa kuweka wagombea wa ubunge na udiwani katika baadhi ya maeneo hata kabla ya kipenga cha mwisho Octoba, 31, 2010. kwa mtaji huu wanajimaliza wenyewe kisiasa kwani wajanja watampatia kura zao KIKWETE

Ndugu yangu unanishock sana. Yaani una maana Chadema ikishinda itabidi itafute watenbdaji wa serikali yake yote wapya nchi nzima? Watumishi wa umma (Civil servants etc) wanatakiwa wasiwe na vyama hivyo hubakia palepale, chama chochote kikishika dola. Wanaobadilishwa ni mawaziri tu na maRC na maDC. Sidhani iwapo Chadema itashindwa kuwapata hawa.
 
Back
Top Bottom