Kulikoni CHADEMA baadhi ya wagombea majmboni kutorudisha fomu?!

Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
15,287
10,842
Wakuu leo nimesikia asubuhi katika radio Wapo kuwa kuna baadhi ya majimbo wagombea ubunge wa CHADEMA hawakurejesha fomu zao hadi ilipofika jana kwa muda waliotakiwa.

Majimbo hayo ni pamoja na lile la Isimani kwa mh. Lukuvi na la Anna Makinda. Pia mengine sikuweza kuyapata maana nilipatwa na mshangao.

CHADEMA jitokezeni hapa mtueleweshe yaliyowasibu wanachama wenu hawa tena viongozi huko waliko na hawakurejesha fomu??!!

Je hii inaashiria nini?

Naamini mmeanza vizuri na ni vema mmalize vizuri. Msitoe nafasi ya changamoto kwa wagombea wengine. Kinachotakiwa ni kuongeza idadi ya wabunge mjengoni!!
 
Ni watu wa CCM disguised nini? Au wamekata tu tamaa?:confused2:

Nadhani ni matatizo ya kiutendaji ndiyo yalowafanya wakashindwa kurejesha hizo forms. Kwa kawaida CHADEMA mwaka huu nategemea itatisha kuliko chaguzi zake zote zilizotangulia, na kuliko chama chochote cha siasa kwa upande wa upinzani. Kikubwa ni mambo ya kusubiri na kuona.

:welcome:
 
Naweza kuelewa kwa nini Njombe Kusini kwa Anna Makinda Chadema wameshindwa kurudisha fomu..........!
 
Naweza kuelewa kwa nini Njombe Kusini kwa Anna Makinda Chadema wameshindwa kurudisha fomu..........!

Mkuu unanirusha roho hapa? Niambie ni kwa nini sasa? Ikiwezekana nitumbukizie kama huwezi mwaga kadamnasi.

nami nilitegemea baada ya operesheni ndefu ya sangara angalau chadema wangekuwa wamejaa nchi nzima, kumbe hata isimani hakuna wa kushindania kiti!

pia kuna rushwa za chinichini na hizi ndizo kubwa kwa wenye fedha kuwahonga washindani ili wajitoe ama wasirudishe fomu. yaani fungu la kamapeni linamegwa kwa mshindani halafu ni naffuu kidogo kuliko kukampeni.
kengele imelia, tafakari, chukua hatua
 
Hapo ubunge tu!Kuna kata nyingi maeneo ya nchi ccm wamepita bila wapinzani kuanzia kesho mtasikia
 
Mkuu unanirusha roho hapa? Niambie ni kwa nini sasa? Ikiwezekana nitumbukizie kama huwezi mwaga kadamnasi.

....mkuu in very brief, wapinzani kule wamegwaya! Mama was very smart tangia mwaka 2006 one year baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge.....matatizo ya kule hasa hasa ni Pembejeo za kilimo (viazi na mahindi) hasa na barabara kidogo sana.....!

Sasa tangia mwaka 2006 mama alihakikisha kuwa kila kaya inapata ile mbolea na ruzuku, madawa ya ukungu, na pia ma bwana shamba kule kwetu hawakauki (tangia 2006).

Kila ifikikapo msimu wa kilimo kila mkulima huandikisha jina na kusema ni nini anataka eg mbolea mifuko 2 (DAP,CAN,UREA) na RIDOMIL(very crucial hii kwa ukungu-viazi)! wanapoanza kupanda mazao malori hupeleka kule mbolea na madawa na wakulima wanagawiwa bureeeeee.....free of cost...trust me!

Barabara kila baada ya miezi mitatu hivi inashindiliwa...so wakulima wanauhakika kupitisha mazao yao muda wowote katika mwaka......!

Tatu...kama utakumbuka issue ya LUMBESA ilianzia Njombe...mama alitupa hii kitu kwenye Council ya halmashauri....ikapigwa moto hadi ngazi ya mkoa, then hadi Taifani....ukaona kina Wasira wanashikia bango.....! so sikuhizo unyonywaji wawakulima uliokuwa unafanywa na walanguzi hakuna siku hizi.....!

Kuna issue ya shule.....hili nalo si tatizo sana kule!

So Maane what do you expect wapinzani wangefanya? Wananchi kule wamekuwa wanapata kile ambacho serikali ilipaswa kuwapa.........so hakuna agenda kwa wapinzani!
 
Hii inaashiria kwamba CHADEMA bado hawana mtandao wa kutosha kuunda serikali kama watashinda Urais hivyo ni mapema sana kuwapatia dola wakati wanashindwa kuweka wagombea wa ubunge na udiwani katika baadhi ya maeneo hata kabla ya kipenga cha mwisho Octoba, 31, 2010. kwa mtaji huu wanajimaliza wenyewe kisiasa kwani wajanja watampatia kura zao KIKWETE

Wakuu leo nimesikia asubuhi katika radio Wapo kuwa kuna baadhi ya majimbo wagombea ubunge wa CHADEMA hawakurejesha fomu zao hadi ilipofika jana kwa muda waliotakiwa.

Majimbo hayo ni pamoja na lile la Isimani kwa mh. Lukuvi na la Anna Makinda. Pia mengine sikuweza kuyapata maana nilipatwa na mshangao.

CHADEMA jitokezeni hapa mtueleweshe yaliyowasibu wanachama wenu hawa tena viongozi huko waliko na hawakurejesha fomu??!!

Je hii inaashiria nini?

Naamini mmeanza vizuri na ni vema mmalize vizuri. Msitoe nafasi ya changamoto kwa wagombea wengine. Kinachotakiwa ni kuongeza idadi ya wabunge mjengoni!!
 
Hii inaashiria kwamba CHADEMA bado hawana mtandao wa kutosha kuunda serikali kama watashinda Urais hivyo ni mapema sana kuwapatia dola wakati wanashindwa kuweka wagombea wa ubunge na udiwani katika baadhi ya maeneo hata kabla ya kipenga cha mwisho Octoba, 31, 2010. kwa mtaji huu wanajimaliza wenyewe kisiasa kwani wajanja watampatia kura zao KIKWETE

Heri yao CUF wamesimamisha!
 
nami nilitegemea baada ya operesheni ndefu ya sangara angalau chadema wangekuwa wamejaa nchi nzima, kumbe hata isimani hakuna wa kushindania kiti!

pia kuna rushwa za chinichini na hizi ndizo kubwa kwa wenye fedha kuwahonga washindani ili wajitoe ama wasirudishe fomu. yaani fungu la kamapeni linamegwa kwa mshindani halafu ni naffuu kidogo kuliko kukampeni.
kengele imelia, tafakari, chukua hatua

kumbe hata chadema wanapokea rushwa na hongo basi hatuna chama cha kukiamini bora CCM waendelee kuongoza nchi huku tukikisafisha chama CCM taratibu. kumbuka mtoa na mpokea rushwa wote hawatufai inakuaje chadema wanahongwa kirahisi rahisi hivi mpaka wanaachia majimbo?
 
Kazi ipo...... Sasa naelewa kwa nini vyama vya upinzani vinachukua makapi ya ccm
 
Back
Top Bottom