Kulikoni BSS? Nasikia ilikuwa jana

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,877
2,758
BSS ya mwaka huu imepoteza mvuto. Jana ndo ilikuwa fainali na wengi hatujui kilichojiri huko. Wadau tuambieni nani alikuwa nani huko
 
BSS ya mwaka huu imepoteza mvuto. Jana ndo ilikuwa fainali na wengi hatujui kilichojiri huko. Wadau tuambieni nani alikuwa nani huko

Yeah man. Hawa mapimbi kweli. Kwenye TV hawajaonesha, magazeti hakujaandikwa. Mpaka sasa hatujui nini kilijiri Diamond Jubilee. Kuna jamaa kanambia Mkata Viuno kalamba 40M. mwenye info please tuambie nani kaibuka kidedea
 
dah! 40mil! Na huyo mkata viuno ndo nani tena? Maana hata sijajua walioingia tano bora
 
BSS ya mwaka huu imepoteza mvuto. Jana ndo ilikuwa fainali na wengi hatujui kilichojiri huko. Wadau tuambieni nani alikuwa nani huko

Hili shindano ni buree kabisa,yaani hawa washindi wake wakitoka hapo wanabakia kuwa wahuni na wazururaji mtaani...hamna kitu pale.
 
tukubali tu kuwa BSS haina tija. Tangu nimeanza kuifahamu, naona inazidi kushuka hadhi tu. Hakuna mdanii hata mmoja wa bss aliyeonyesha cheche baada ya mashindano kuisha. Wakiendelea hivi watakosa hata wadhamini.
 
Kama ni yeye anastahili ila sijajua kwa nini hawakuaonyesha kwenye Tv hata kusikia kwenye vyombo vya habari sijasikia.
 
Kama ni yeye anastahili ila sijajua kwa nini hawakuaonyesha kwenye Tv hata kusikia kwenye vyombo vya habari sijasikia.

isingekuwa rahisi kuonyesha pale itv kwa kuwa muda huo kulikuwa na kipindi cha maana zaidi cha kipimajoto kikimzungumzia Nyerere. Kimsingi walichemsha kufanya fainali siku ile
 
Kuna mwandishi nilipenda sana andiko lake....
"BSS ni uchochoro wa wasanii wachovu"
Hata hivyo mapema sana pale mwanzoni wakati inaanza wakina Ritta walipokuwa wanapishana na yule judge mhindi (sijui jina lake), nikajua tu hawa waandaaji ni makanjanja.
Na yule mhindi sikumuonaga tena hata screening hakumalizia
 
bss ni majambazi....haiwezekani waendeshe ile program kwa kuonyesha kwenye tv na kushawishi watu ku-vote kwa text then fainali haionyeshwi. huo ni wizi na ninaulaaani kwa nguvu zote, tena ni dharau walitegemea watu wa mikoani wote waje hapo diamond jubilee?? kama sio dharau na matusi kwa wananchi wa tanzaniaa ni nini?? alafu mpaka sasa hawajatoa tamko lolote hata kuomba msamaha kwa kushindwa kwao kuonyesha hilo tukio.

hawa watu waporwe licence, kwanza wanawatukana na kuwakatisha tamaa wasanii wachanga....
 
Back
Top Bottom