Kuliko kutopeleka bajeti majimbo ya UKAWA, Spika awanyime maslahi wabunge!

Martin George

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,695
1,470
Ndio, yeye Spika ashughulike na wabunge waliomchagua na akiweza basi awanyime posho na mishahara wale anaodhani waliikataa bajeti. Huku majimboni atuachie wananchi na serikali yetu, kwenye swala la maendeleo Rais Magufuli haangalii mambo ya vyama yeye anaiangalia Tanzania! ' Mambo' yenu ya vyama malizaneni hukohuko bungeni, waziri wa fedha ni wa watanzania wote fullstop.
 
Hakika mkuu umenena vema sana,huyu anataka kuleta siasa kwenye utendaji
 
Hivi vyama ndo vinatusumbua Tanzania na ingekuwa ni vya kuwaka ningeshavitia moto
 
Mimi nafikiri kama wale wa CCM wanapewa hela kwa vile wameipitisha bajeti ya serikali kupitia waziri Mpango, basi hata wapinzani wapewe hela ambayo ni kodi yetu sote ili watekeleze bajeti yao iliyowasilishwa na waziri wa fedha kivuli kupitia bajeti mbadala ya upinzani. Kila mtu apewe kulingana na alivyoomba. Kwa sababu najua upinzani wana bajeti yao na serikali ya CCM wana bajeti yao lakini wote wanategemea fedha yetu wote iliyo kwenye hazina ya Taifa.
 
Back
Top Bottom