Kuliko kutaga Magu atawale miaka 20, tungefuta uchaguzi wa Rais mwaka huu

kluger

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
2,093
1,894
Kumekuwa na hoja toka MATAGA, kuwa ikiwezekana Mheshimiwa Rais atawale zaidi ya miaka 20.

Kwa maoni yangu kabla ya kuwaza huko, ni bora tungeanza na uchaguzi wa Mwaka huu, kipengele cha Urais kingefutwa, Mheshimiwa aendelee moja kwa moja awamu ya pili na fedha za uchaguzi zielekezwe Standard Gauge Railway.

Cha ajabu MATAGA wao wanawaza tu mzee atawale milele.

Kiukweli kufanya uchaguzi, huku tukijua kabisa, mtu fulani piga ua garagaza hata iweje atatangazwa mshindi, ni kupoteza hela. Bora hata watu wangefanya kura za maoni tu tukamaliza shughuli na kuokoa mamilioni ya fedha yatakayopotea bila sababu.

Kwa upande wa wabunge pia, kuna mikakati ya MATAGA kushinda kila jimbo, kwa style ile ile ya piga ua garagaza lazima watu fulani washinde. Uchaguzi unakosa maana yake halisi.
Tungefanya kura za Maoni tu, mpitishe watu wenu wale ambao kwa sasa mnawahitaji. Then sisi mtuletee huduma tu za kijamii.
Ingependeza sana sana.

Kuigiza maisha au vitu fulani wakati uhalisia siyo, ni Unafiki au Upumbavu mkubwa, hivyo waafrica tubadilike.

Ni hayo tu, ushauri kwa watakaoweza kuupata, kuusikia na hata kupata mawazo mbadala zaidi ya haya.

Siku njema.
 
Kwa sababu Kikwete aliwahi kupata asilimia 80 na zaidi..
Nna uhakika huyu watatangaza asilimia 90 au zaidi..ndo lengo la uchaguzi wa mwaka huu..
Wait and see...
 
Kweli kabisa, tutaletewa maigizo tu mtu kashinda kwa kishindo asilimia 95.
Haina maana ya uchaguzi hapa, nikupoteza raslimali fedha na Muda tu.
 
Back
Top Bottom