Kulia kwa mayowe na sauti kubwa: Je, Waafrika tuko too emotional?!

Nimejionea jinsi tunavyoomboleza pale wapendwa wetu wanapotutoka. Pia nimejionea mbali na nyumbani, ughaibuni ndani ya usafiri wa umma, pale watoto wadogo wa Kiafirika wanapokuwa na wazazi wao wakiwa wanalia kwa sauti kubwa na kugalagala wakidai mahitaji yao.

Wakubwa kwa wadogo naona wote tunavilio vikubwa ambavyo havilingani ama sijapata kuviona katika kiwango hicho hicho kwenye jamii nyingine zisizo za Kiafrika. Are Africans more emotional? Naomba mawaidha yenu. Ahsanteni.

Kwa vile tunaishi na kufahamiana kwa karibu, mmoja wetu anapotutoka tunasikitika sana! Hata kwa wazungu, ikitokea mtu wanayemfahamu anawatoka wanasikitika sana.

Kwamba sisi tunalia kwa sauti kubwa na wengine ndogo au wanatoa tu machozi si kitu sana; kitu ni kwamba wote tunahuzunika!

Mimi nilikuwa siwezi kusoma mbele ya watu wengi na nikisoma nilikuwa natetemeka sana hata wanafunzi wenzangu kuanza kucheka. Nilijiona 'inferior' na nikawa ninakwepa 'chances' zinazonifanya nisome au niseme kitu mbele ya watu wengi.

Siku moja nilimwendea 'counsellor' nikamwambia kuwa mimi siko kama wengine na hivyo najiona mdogo sana! Huyu alikuwa mmoja wa walimu wangu katika university (in the 1990s).

Yeye alinijibu hivi: "Although you are a nerveous person you have many outweighing qualities. You are a realible person and we are very happy to have a student like you at the university. On your being nervous, I can say this: nervousness is just a way your body responds to external stimuli. Every person has his or her own way of responding to that: you shake, others sweat or 'bite' fingures etc... all that is a response to external stimuli. So, don't have a low self-esteem. You are more than being nervous."

Kuanzia siku niliyopata huo ushauri nikabadilika na kuanza kujiona sawa na wengine hadi leo hii!

Kwa hiyo, ninachoweza kusema ni kwamba mazingira tu ndiyo yanayotufanya tuwe hivyo lakini kila jamii ya watu wanasikitika kwa namna yao na sauti au otherwise, siyo kipimo kwamba sisi ni 'too emotional' kuliko wengine. It's only that we are different and respond to things differently!
 
Last edited:
Labda kutoa huku sauti kwa vilio, haswa kwa watoto, kunaelezea ni jinsi namna gani watu weusi mara nyingi wanakuwa na vipaji vya kuimba! i.e. Our vocal cords are well built for this, both in crying and singing...
 
Nimejionea jinsi tunavyoomboleza pale wapendwa wetu wanapotutoka. Pia nimejionea mbali na nyumbani, ughaibuni ndani ya usafiri wa umma, pale watoto wadogo wa Kiafirika wanapokuwa na wazazi wao wakiwa wanalia kwa sauti kubwa na kugalagala wakidai mahitaji yao.

Wakubwa kwa wadogo naona wote tunavilio vikubwa ambavyo havilingani ama sijapata kuviona katika kiwango hicho hicho kwenye jamii nyingine zisizo za Kiafrika. Are Africans more emotional? Naomba mawaidha yenu. Ahsanteni.

yani umeulizia kitu ambacho sikipendi kabisa. Tena nahisi kinaniboa na kuona ni ushamba kitu hiki kuingizwa ktk filamu (yani usiseme huko ktk filamu za kinageria na za kibongo).
 
yani umeulizia kitu ambacho sikipendi kabisa. Tena nahisi kinaniboa na kuona ni ushamba kitu hiki kuingizwa ktk filamu (yani usiseme huko ktk filamu za kinageria na za kibongo).

tupo pamoja mkuu...kule kulia kunanikera
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom