Kulia kwa mayowe na sauti kubwa: Je, Waafrika tuko too emotional?!

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
Nimejionea jinsi tunavyoomboleza pale wapendwa wetu wanapotutoka. Pia nimejionea mbali na nyumbani, ughaibuni ndani ya usafiri wa umma, pale watoto wadogo wa Kiafirika wanapokuwa na wazazi wao wakiwa wanalia kwa sauti kubwa na kugalagala wakidai mahitaji yao.

Wakubwa kwa wadogo naona wote tunavilio vikubwa ambavyo havilingani ama sijapata kuviona katika kiwango hicho hicho kwenye jamii nyingine zisizo za Kiafrika. Are Africans more emotional? Naomba mawaidha yenu. Ahsanteni.
 
Watoto wote wanalia sawa.Kuhusu katika misiba it has more to do with culture than emotion.If anything, one can argue that Africans are more humane in that aspect and fully cognizant of their ignorance of what comes after death, despite all the hoopla.
 
Bluray, kwa kweli hapo juu mimi sina uhakika sana. Maana nimeona watoto wa asili nyingine, mfano wakizungu, wakililia, tuseme nyonyo, na vile vile nimejionea watoto wadogo wakiafrika wakililia nyonyo, haijalishi ya chupa au ya chuchu za mama, kusema ukweli experience yangu naona watoto wa kiafrika wanaangua vilio vikubwa zaidi kwenye same needs. I could be wrong but this is just my sincere observation.
 
Nimejionea jinsi tunavyoomboleza pale wapendwa wetu wanapotutoka. Pia nimejionea mbali na nyumbani, ughaibuni ndani ya usafiri wa umma, pale watoto wadogo wa Kiafirika wanapokuwa na wazazi wao wakiwa wanalia kwa sauti kubwa na kugalagala wakidai mahitaji yao.

Wakubwa kwa wadogo naona wote tunavilio vikubwa ambavyo havilingani ama sijapata kuviona katika kiwango hicho hicho kwenye jamii nyingine zisizo za Kiafrika. Are Africans more emotional? Naomba mawaidha yenu. Ahsanteni.
Na haswa jamaa zetu wa Afrika Magharibi (Nigerian), maana wao hata kwenye kuongea tu balaa.
 
Bluray, kwa kweli hapo juu mimi sina uhakika sana. Maana nimeona watoto wa asili nyingine, mfano wakizungu, wakililia, tuseme nyonyo, na vile vile nimejionea watoto wadogo wakiafrika wakililia nyonyo, haijalishi ya chupa au ya chuchu za mama, kusema ukweli experience yangu naona watoto wa kiafrika wanaangua vilio vikubwa zaidi kwenye same needs. I could be wrong but this is just my sincere observation.

Ya kweli hayo...
 
hata kwenye love making!the same scenario,AS PER MY EXIPERIENCE
 
Ukiacha misiba na watoto, wanawake wenye tabia ya kulia kwa kila jambo ni waongo! Au wana tabia ya uongo. Na iwapo wapo kwenye mahusiano basi ni dalili tosha kuwa ana tabia ya kucheat
 
Kibunango, unataka kusema tukimsikia mtu msibani analia sana tena kwa makelele haswa tujue kuwa kuna walakin au...?
 
Ukiacha msibani, let say mpenzi wako wamekusindikiza kupanda basi na unasafiri kwenda mbali na safari itakayo chukua muda mrefu mpaka urudi tena.

Then mpenzi wako anaanza kulia kuwa unamwacha peke yake na blah blah zingine.. Hapo jua fika kuna uwalakini
 
Hiyo ya kuliliwa stand ya bus kwa sauti hiyo sasa kali. Lakini kuona machozi tu ya udhuni hiyo kawaida hata kwa wanaume.
 
Nimejionea jinsi tunavyoomboleza pale wapendwa wetu wanapotutoka. Pia nimejionea mbali na nyumbani, ughaibuni ndani ya usafiri wa umma, pale watoto wadogo wa Kiafirika wanapokuwa na wazazi wao wakiwa wanalia kwa sauti kubwa na kugalagala wakidai mahitaji yao.

Wakubwa kwa wadogo naona wote tunavilio vikubwa ambavyo havilingani ama sijapata kuviona katika kiwango hicho hicho kwenye jamii nyingine zisizo za Kiafrika. Are Africans more emotional? Naomba mawaidha yenu. Ahsanteni.

...mbwembwe tu zile kaka, njaa ni kitu mbaya sana aisee!
 
Ila siku hizi nasikia kuna vikundi maalum vya maombelezo na uliaji. Pesa kidogo tu na ukiwahakikishia mlo na pesa ya kilevi, basi watatia team msibani na kujaza msiba na vilio vyao na nyimbo za maombolezo.
 
Potential talents.... ironically, what does this explain?!
 
Kulia watu wanalia kulingana na matukio yaliyopo mbele yao sina uhakika sana kusema wabantu tu ndo wanalia sana kuliko wengine hapo bado.
Ila mabigwa wa kulia mara nyingi ni wanawake na watoto kama unabisha nitashuka na data za ukweli hapa.
 
hata kwenye love making!the same scenario,AS PER MY EXIPERIENCE

huyu jamaa mbona kama anauzunguka na kutaka kuukumbatia mbuyu?,
nahisi hii ndio ilikua point yake!.
icon10.gif
 
Kwa watu wazima kulia kunategemea utamaduni wa watu. Jamii nyingi za kiafrika zina namna tofauti za kulia kwenye misiba: wengine wanapiga mayowe, wengine wanalia utadhani wanaimba aina fulani za nyimbo, wengine wanalia wakighani sifa za marehemu, nk. Zote hizo ni aina za kulia. Na mara nyingi ni vilio vyenye sauti kubwa.

Watoto wadogo sidhani kama kulia kwao kuna tofauti na watoto wa jamii zingine japo hilo siwezi kulipinga.

Lazima kukubali pia ukweli kwamba waafrika tuko MOTO kuliko pengine wazungu kwa mengi. Inawezekana ni kutokana na mazingira yetu ya joto. Wazungu wako baridi kwa mengi. Waafrika tuko motomoto: mfano nyimbo zetu au miziki ni ya harakaharaka na ya kishindo (mapigo mazito), tukifurahi tunacheka kwelikweli, tukicheza tunacheza kwa kishindo, kwenye sex pia ni shughuli pevu, nk. Kwa hiyo, mi nadhani tofauti zipo, na zinatokana na mazingira na tamaduni za jamii zetu.
 
njaa hata mcbani? ...au mie ndio niko nje ya mstari nini.

...naaaaam, kulia hakuchukizi...kinachochusha ni mayowe na maneno wanayoyatoa 'wafiwa'...

yasikize kwa makini, mengi ni kero tupu lengo nia na madhumuni ni kutafuta sifa, utasikia "...mlimuona fulani katika kilio cha fulani alivyolia?"

Kwetu kulia kwa mayowe/kwa sauti ni mwiko!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom