Kulewa kwa kupitiliza kunataka kumfanya Baba yangu atake kustaafu mapema

KingPower

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
1,099
1,746
Habar wakuu

Nina kisa cha Baba yangu ni mtumishi serikalini kweny moja ya majeshi

Mwanzoni kabisa Baba yangu alikua mtu smart sna nilimuadmire sna Ila Mambo naona yanaenda tofauti.

Aliminika na watu na kuwa msaada Kwa watu hadi ilipofika 2015 Mzee akazidi matumizi ya pombe analewa sana mpaka anaokotwa na kurudishwa nyumbani

Alipungua mwili na kuchakaa Kwa haraka sna mpaka leo hii 2022.

Sasa ivi hadi kutembea anatembea kwa shida sna ni anatia huruma mno

Mama ameangaika naye Kwa waganga wa kila aina ila swala la kuacha pombe limeshindikana kbsa, alitolewa position nyingi kazini kwake na kuamishwa sna yupo moja ya wilaya mkoani manyara

Mambo mengi yameharibika kwa sababu ya pombe yani ukimuona Kwa mbali kabakia shati Tu (inaniuma).

Watu kazini kwake wamemchongea sna Kwa viongozi wa makao makuu ikiwa pamoja na kumnunulia pombe Mzee ili kazini akutwe amelewa

Na hii naona kama imemkalia pabaya maana wenzake wote waliopata nyota 3 na yeye ,, wote wana Mienge.

Inafikia stage hadi kazini analewa na anarudi kabebwa kweny toroli (uniform zote zimechafuka )

Tumesali sna ikiwa pamoja na kwenda Kwa waganga lakini wapi

Toka jana anataka kuandika barua ya kuomba kustaafu ambavyo anataka kuipeleka kesho (bado miaka 8 kustaafu) Kwa sasa anamiaka 52.
Anazidiwa nguvu hata na mzee wa miaka 70

Anadai amechoka sna, na pia mdogo wetu wa mwisho ambaye anamsomesha yupo mwaka wa 2 chuo

Anasema anaweza asifike umri wa kustaafu miaka 60 ,

Mipango yake ni kujenga nyumba ya familia, pia anasema ili tusije kumlaumu.

Hii scerio inafanana kabisa naya Babu yangu (Baba yake) baada ya kustaafu (alikua magereza) alizidi ulevi mara dufu hadi kufikia stage ya kuokotwa, anaomba vitumbua ect. Ni kama kuna laana ya ukoo. Ana miaka 32 kazini

Na pia ni nguzo muhimu sna kweny familia yetu, Ni kama nyota kweny ukoo wetu na inataka kuzima (Mungu amnusuru) Aiseee pombe imemrudisha sna nyuma Mzee wangu. Natamani hata nimpe msaada (mweny uwezo wa kumsaidi katika ili naomba ajitokeze ) Yupo kweny stage mbaya sna.

Nashauri Ndugu zangu pombe mnywe Kwa kiasi mtazisumbua familia zenu na kuzipitisha kwenye mateso sna

Sijakataa kustaafu kwake na ninaheshimu maamuzi yake, Je hawa watu wa PSSSF hawatamzungusha kweny mafao yake?

Pia naomba msaada wa ushauri wenu juu ya hili

Asante
 
Habar wakuu

Nina kisa cha Baba yangu ni mtumishi serikalini kweny moja ya majeshi

Mwanzoni kabisa Baba yangu alikua mtu smart sna nilimuadmire sna Ila Mambo naona yanaenda tofauti.

Aliminika na watu na kuwa msaada Kwa watu hadi ilipofika 2015 Mzee akazidi matumizi ya pombe analewa sana mpaka anaokotwa na kurudishwa nyumbani

Alipungua mwili na kuchakaa Kwa haraka sna mpaka leo hii 2022.

Sasa ivi hadi kutembea anatembea kwa shida sna ni anatia huruma mno

Mama ameangaika naye Kwa waganga wa kila aina ila swala la kuacha pombe limeshindikana kbsa, alitolewa position nyingi kazini kwake na kuamishwa sna yupo moja ya wilaya mkoani manyara

Mambo mengi yameharibika kwa sababu ya pombe yani ukimuona Kwa mbali kabakia shati Tu (inaniuma).

Watu kazini kwake wamemchongea sna Kwa viongozi wa makao makuu ikiwa pamoja na kumnunulia pombe Mzee ili kazini akutwe amelewa

Na hii naona kama imemkalia pabaya maana wenzake wote waliopata nyota 3 na yeye ,, wote wana Mienge.

Inafikia stage hadi kazini analewa na anarudi kabebwa kweny toroli (uniform zote zimechafuka )

Tumesali sna ikiwa pamoja na kwenda Kwa waganga lakini wapi

Toka jana anataka kuandika barua ya kuomba kustaafu ambavyo anataka kuipeleka kesho (bado miaka 8 kustaafu) Kwa sasa anamiaka 52.
Anazidiwa nguvu hata na mzee wa miaka 70

Anadai amechoka sna, na pia mdogo wetu wa mwisho ambaye anamsomesha yupo mwaka wa 2 chuo

Anasema anaweza asifike umri wa kustaafu miaka 60 ,

Mipango yake ni kujenga nyumba ya familia, pia anasema ili tusije kumlaumu.

Hii scerio inafanana kabisa naya Babu yangu (Baba yake) baada ya kustaafu (alikua magereza) alizidi ulevi mara dufu hadi kufikia stage ya kuokotwa, anaomba vitumbua ect. Ni kama kuna laana ya ukoo.
Ana miaka 32 kazini

Na pia ni nguzo muhimu sna kweny familia yetu
Ni kama nyota kweny ukoo wetu na inataka kuzima (Mungu amnusuru)

Aiseee pombe imemrudisha sna nyuma Mzee wangu
Natamani hata nimpe msaada (mweny uwezo wa kumsaidi katika ili naomba ajitokeze )
Yupo kweny stage mbaya sna.

Nashauri Ndugu zangu pombe mnywe Kwa kiasi mtazisumbua familia zenu na kuzipitisha kwenye mateso sna

Sijakataa kustaafu kwake na ninaheshimu maamuzi yake, Je hawa watu wa PSSSF hawatamzungusha kweny mafao yake?

Pia naomba msaada wa ushauri wenu juu ya hili

Asante
Pole sana mkuu, Tunamuombea sana,hilo la waganga achana nalo,omba sana Mungu pia mshirikishe katika Maombi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom