Kule Kutakiana Kheri Wakati Unaenda Kufanya Interview Huwa Zinatoka Moyoni au?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,212
Hii Kitu Nimekuwa Nikiiona Kama Siyo Kukutana Nayo Sana Tu Pale Ambapo Watu Mnakwenda Kufanya USAILI Wa Kazi ( INTERVIEW ) Fulani Halafu Kabla Ya Kuanza Huo USAILI Mnajikuta Wote Mpo Katika Chumba Kimoja Kusubiri Kuitwa Na Bahati Nzuri Unakuta Wote Mliopo Hapo Mnaigombea Hiyo Hiyo Nafasi Moja Huku Wote Hapo Mkiangaliana Na MIDOMO Ikiwa IMEWAKAUKA Kwa Njaa Na Kupigika Na Maisha Lakini Utakuta Pale Tu Mmoja Wenu Akiitwa Na WASAILI Na Kuwaageni Utasikia " NAKUTAKIA KILA LA KHERI MWAYA au MWENYEZI MUNGU AKUTANGULIE au KAWAONYESHE WEWE NI JEMBE au KAWAKOMESHE KAMANDA ".

Sasa Naomba KUULIZA Kama Tunatakiana KHERI Namna Hii Kwanini Tu Tukishakuwa Pale USAILINI Na Tukaona Kwamba Mwenzetu Mmoja ANAFAA Kuichukua Hiyo NAFASI Basi Tusipoteze Muda Na Badala Yake Pale Pale TUWAFUATE WALE WASAILI Na Tuwaambie Kuwa Tunadhani Sisi Wote HATUFAI Ila Huyu Mwenzetu ATAWAFAA Kisha Tuondoke Zetu Pale?

Je Huku KUTAKIANA KHERI KWETU PALE UKUMBINI Wakati Mwenzetu Mmoja Anaenda Katika Chumba Cha Kufanya USAILI ( INTERVIEW ) Huwa Ni Kwa UKWELI KUTOKA MOYONI au Ni UNAFIKI WA HALI YA JUU ( ULIOTUKUKA ) Tu?

Karibuni.
 
Kama nafasi ni yako lazima itakuwa yako tu. Mtakie kheri,kama atafanya vizuri Inshallah apate hiyo nafasi.
Kumtakia kheri hakumaanishi kwamba atashinda LA haula! Bali unampa moyo kwamba anaweza na Mungu amjalie.
Ni kama sala ya mwisho kwa marehemu,haimaanishi itamuondolea dhambi ambazo hakutubu bali tu unamuombea Mungu ampokee
 
Sio unafiki ni utamaduni wa Watanzania. Sio kwenye interview tu, hata ukiwa unaenda sokoni "majirani watakutakia kila la kheri." Watanzania ni watu wa ajabu mno.
 
Sio unafiki ni utamaduni wa Watanzania. Sio kwenye interview tu, hata ukiwa unaenda sokoni "majirani watakutakia kila la kheri." Watanzania ni watu wa ajabu mno.

Acha KUPEPESA Macho au KUTIKISA Masikio au KUTINGISHA Miguu SEMA TU UKWELI Kuwa WATANZANIA " Naturally " Ni WANAFIKI TULIOTUKUKA.
 
Ni utamaduni tu na kawaida yetu tuliyoizoea, mtu anatumia nconscious mind kukutakia heri hata kama mnafukuzia nafasi moja, ila mwenzake akufanikiwa kupata na yeye akakosa, ndipo automatically anatumia subconscious mind maana hapo ataanza kufikiri namna gani ata-solve matatizo baada ya kukosa kazi.
 
Kama nafasi ni yako lazima itakuwa yako tu. Mtakie kheri,kama atafanya vizuri Inshallah apate hiyo nafasi.
Kumtakia kheri hakumaanishi kwamba atashinda LA haula! Bali unampa moyo kwamba anaweza na Mungu amjalie.
Ni kama sala ya mwisho kwa marehemu,haimaanishi itamuondolea dhambi ambazo hakutubu bali tu unamuombea Mungu ampokee

Je Hiki Ulichokiandika Hapa Kina Tofauti Gani Na Dhana Nzima Ya Neno " UNAFIKI? " Hivi Kusema Kweli Kutoka Moyoni Kwa Psychological Nature Ya MWANADAMU Ile Ya Kwamba Ni " EGOIST " Huku Kutakiana Kwetu Kheri Ni Kwa Kheri Kweli?
 
Ah!! Sasa ulikua na haja gani kuuliza swali mkuu?

Kwani MWALIMU WA SHULE ANAPOWAFUNDISHENI SOMO FULANI DARASANI HALAFU ANAULIZA au ANAWAULIZENI " MMEELEWA? " NA MNAJIBU " NDIYOOOOOO " Lakini Bado Mwalimu Huyo Huyo ATAWAPENI MTIHANI Unadhani Huyo Mwalimu au Hao Walimu Huwa Na Maana Gani?
 
Duh. Any way
 
...anakuwa anataka kuthibitisha kama kweli mmeelewa!...ila wewe hapa ukipewa majibu tofauti unang'ang'ana na jibu lako!
...baki nalo kama waamini ndilo sahihi zaidi!
 
Wanyarwanda wana vipaji ajabu aisee! Huyu fundi wa rangi kaamua kuhamishia ujuzi wake jf anatandika tu masms na kuyapiga rangi mkuu sijaiona herufi yenye rangi ya kijani tupia na hiyo mkuu wanyarwanda wabunifu jamani si mnaona mambo yao sms inachanganywa rangi kama kachumbali ya x mass acha kabs chezea toto ya kagame ww
 
Acha UZUSHI Wako Wewe Sawa? Sipo Tanzania Sasa Ni Mwaka Wa 11 Na Nipo Kwetu Kigali Nchini Rwanda. JF Naifahamu Kupitia Humu Humu Tu.
ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu.sie wewe uliesema umemaliza St Augustine? sasa St Augustine ilianza lini na wewe ulimaliza lini? Leo unasema una miaka 11 rwanda
 
Kwani MWALIMU WA SHULE ANAPOWAFUNDISHENI SOMO FULANI DARASANI HALAFU ANAULIZA au ANAWAULIZENI " MMEELEWA? " NA MNAJIBU " NDIYOOOOOO " Lakini Bado Mwalimu Huyo Huyo ATAWAPENI MTIHANI Unadhani Huyo Mwalimu au Hao Walimu Huwa Na Maana Gani?
wewe ni bonge la limaamuma lililotukuka
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom