Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,798
- 34,170
Vitu vitamuvitamu kama keki, kuku wa kukaangwa, vibanzi ni vitamu lakini je vinafaa? Mwili wako hauwezi kuwa katika hali nzuri ya kiafya kwa kuvitegemea hivi vyakula pekee. Kula vyakula vilivyo na rutubishi vya kusaidia moyo wako, na sehemu ya tumbo (isiwe kubwa) utaishi maisha marefu na ya afya nzuri.
Ulijua eti kuna baadhi ya vyakula vinavyoweza kuusaidia mwili wako kupambana na uvamizi wa magonjwa. Ndio. Ni nani asiyetaka hivyo?
Kulingana na taasisi ya lishe bora ya huko Marekani, vyakula virutubishi ni matunda, mboga, nyama isiyo na mafuta, sehemu ya titi ya kuku, mikate ya wishwa, maziwa yasiyo na mafuta, mayai na njugu.
Hivi vyakula havijajazwa mafuta ya kununuliwa na vina virutubishi vyote vinavyohitajika na mwili wa binanadamu. Usitafute vyakula vya kuiva harakaharaka vinavyofanya maisha yetu rahisi kwa sababu tunavipika haraka haraka na kwa urahisi.
Vina mafuta mengi na hunonesha tu mwili lakinii havina virutubishi vya kutosha. Vyakula vilivyowekwa kwenye jokofu, vilivyohifadhiwa ndani ya makaratasi na mikebe, vinaweza kuwa na madini nyingi ya sodium.
Kula vizuri kunahusu kufanya uamuzi unaofaa kila mara. Lengo lako liwe tu kula lishe bora lenye virutubishi vyote visivyo na mafuta mengi na ambavyo si vya kunonesha.
Pia ni muhimu uchunge kiasi cha chakula unachokila. Usiweke tu mlima wa chakula kwenye sahani yako!