Kula huku kula gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kula huku kula gani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 15, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kula huku kula gani, kula bila ya kunawa?
  Kula huku kula gani, kula bila kupumua?
  Kula huku kula gani, kula bila kuchagua?
  Kula huku kula gani, vya watoto navyo mwala?

  Kula huku kula gani, mikono yote miwili?
  kula huku kula gani, mbona nyinyi si makuli?
  Kula huku kula gani, mwala hadi pilipili?
  KUla huku kula gani, vya watoto navyo mwala?

  Kula huku kula gani, kula huku mwacheua,
  Kula huku kula gani, na meno mmekenua,
  Kula huku kula gani, huku mnajisheua,
  Kula huku kula gani, vya watoto navyo mwala?

  Kula huku kula gani, mwala huku mwavimbiwa,
  Kula huku kula gani, na harufu mnatowa,
  Kula huku kula gani, na jasho hilo mwalowa,
  Kula huku kula gani, vya watoto navyo mwala?

  Kula huku kula gani, mwagawiana sinia,
  Kula huku kula gani, zamu mnajipangia,
  Kula huku kula gani, mwala tena mwarudia,
  Kula huku kula gani, vya watoto navyo mwala?

  Kula huku kula gani, mnakula hadi mbegu,
  Kula huku kula gani, mwayala hata magugu,
  Kula huku kula gani, huku mwatuita ndugu,
  Kula huku kula gani, vya watoto navyo mwala?

  Kula mmeshakwishakula, sasa muda wa kulipa,
  Vya wanetu mmekula, kulipa na mtalipa,
  Mlidhani tumelala, wajanja mkatukopa,
  Vya kwenu hatutavila, na kura hatutawapa!

  Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
   
 2. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hapa kusadikika,
  Twala hata Sadaka,
   
 3. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Asante kwa utezi wako babu yangu
   
 4. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mzee wa Kijijini Kwetu Shikamoo!
  Huwa nikisoma tenzi zako zinanikumbusha enzi zile tukiita middle school au primary school kabla haijawa shule ya msingi, kabla ya lile azimio letu la Musoma. Azimio lile halikuwa baya lilitufanya wengi tukajua kusoma na kuandika lakini halikutufanya tuelimike. Azimio lile ni sawa na Maamuzi ya shule za kata za Mkapa za Bila azimio, wengi watamaliza Vidato lakini MM nakwambia watoto hawajui kitu kinaitwa Bunsen Burner. Nasikia wanafanya Alternative to Practicals, sijui ndio zikoje? Nachotaka Kusema HONGERA sana kwa kuelimika Mzee.

  Kwenye hawa jamaa waliokula, naogopa kukwambia kuwa msimu wa kupanda umefika, sasa hii habari yako imetushtua sana kuwa wamekula mpaka mbegu, tutapanda nini? bahati mbaya hata yale majani yalikuwa yanafaa kwa mboga za majani yameliwa na tembo na wanyama wa poli, inasemekana baada ya nyani kuvuna mahindi yote shambani sasa wale wanyama wa pori waliokuwa waji kijijini wamekuja kwa wingi tu, si kwa mazao yalioko juu ya aridhi hata yale yalioko chini ya aridhi yameliwa na Fuko. Mjomba alisema ataangalia upya uzio unaotenganisha kijiji na hifadhi za wanyama pori ili wakija basi nasi japo tupate nyama kidogo za wanyama lakini tunaona mpaka leo kimya.

  Mzee Mwakijiji, akina shangazi na binamu nao wamesema ni ndugu zake na baba na wanahaki na mali na aridhi za ukoo wetu. Kwa hiyo inakuwa shida sana kuitisha kikao cha familia kujadili japo kubadilisha taratibu za kugawana hayo mazao. wamesema hata wakila kuna shida gani? nao si wanandug? lakini kibaya zaidi wapo wengine wanaotoa mazao wanaenda kuhifadhi kwenye vihenge vya vijiji vya mbali, nadhani utakapo rudi utaona hata mabua wamehamisha.

  Nashukuru kwa moyo wako wa kuwaambia kuwa walipe, na kuwa muda umefika, na kuwa kama hatawalipa watakipata cha mtema kuni. Mimi na wadogo zangu tunaogopa sana kuwawajibisha hawa akina shangazi na binamu na hata mjomba. Mwaka 1995 walituambia kama tutampa mtu mwingine kuwa msimamizi wa mirathi kutawaka moto kam kwa jirani yule mwembamba mrefu, si unaona hata yule dada walimpelaka mahakami kwenye sijui wanaita "Dar Haiji". Tukafikiria tena mwaka 2005, waksema si unaona huyu mnayetaka kumpa usimamizi wa mirathi atawavalisha wote Kombati, mtapiga gwaride weeee usiku na mchana. Walipoona tunaonekana hatuwasikilizi, wakasema huyu ni mchawi sana, si mnaona anaruka juu na Ungo, anawanga mchana kweupe.

  Sasa mimi nimechanganyikiwa, sasa hivi wanasema kama mnataka kumpa mtu mwingine basi asiwe yule dogo wa kushinda kwenye matreni hajakomaa kisiasa, mara alishanunuliwa, tukasema basi tumpe yule mwinjilist maana ni msema ukweli mtu wa Mungu, nao wana hoja wanasema kama alishindwa kutunza mkataba na kanisa ndio ataweza kutunza mikataba na nyie yatima,

  Mzee wetu hali ni ngumu, sijui kama tutaruhusiwa kuwa na wasiofungamana na itikadi ya familia yoyote, maana wanaonekana hawaipendi hii hoja pia. upande wao inaonekana ile hoja ya kusema watoto wa mjomba watamtaka Mjomba kwa hiari aachie usimamizi wa mirathi imepingwa vibaya mno na wazee na vijana wanaomzunguka mjomba. Hadi Mtera nao walisema hawaoni sababu.

  Kuna akina binamu watoto wa mjomba wanonekana kuja juu sana kwa maneno sijui kama watakuwa tofauti na baba yao, labda wanafanana rangi lakini matendo ni tofauti, labda watasema mali za yatima ziwafikie walengwa sijui, unawajua akaina Jafari, akina mashaka, akina Bernad, akina Lawrence sasa hivi ni wakubwa sana. Ila yule mtoto wa mzee wa strategy za ushindi wakati ule alishindana nao kwenye ujenzi wa nyumba ya vijana, yupo kimya sana.

  Mzee ninayo mengi ya kukwambia lakini muda hautoshi, Nitakuandikia siku nyingine, wasalimie huko kwako, nasikia vi-nzi vyako vinafanya kazi ya "Nge" Kama hujawasikia hao nge walikuwa wanaangalia mali za kijiji cha kule chini ambako baba yao alifungwa kisiwani kwa miaka 27. Mkuu waangalie walipowaua hawa Nge, lakini naamini kama hata sungusungu wetu wangefanya kazi hata kwa miezi sita tu kama hao nge, kijiji chetu kingekuwa cha mfano. Inawezekana nzi wakawa ni njia mbadala ya sungusungu, tuwape chakula, nitatuma noti ya sh.20 unitumia lile karatasi walilochafua hao nzi kule wapi sijui asia.

  Nisalimie wazee wenzio watakapokuja kunywa kahawa Jamvini.
  Mwanao
  Kijijini Kwetu :(
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hebu niulize swali...
  Hivi ni nani aliyewachagua hao wanaokula kuku na vifaranga...!
   
 6. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  kwani kuna kuchaguliwa ndugu yangu?? wanatumia maguvu kujiingiza kwenye kusimamia mirathi, wanayumbisha vyombo vya habari waandike kuhusu wao, mpaka vija wa ubongo wa fleva wanapewa VG Centi wawafagilie, hai mgambo ndio usiseme kutembeza virungu kwa kwenda mbele kitisha watu yaani wee acha tu, ili maradi wazidi kunenepa kwa mazao na kuku ana viafaranga mpaka mayai waliyoatamia yote wanasakafia.
   
 7. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #7
  Jul 15, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Muyaka naye anajibu:

  akutendeae mema
  kumshukuru ni lazima
  jaza ya mema ni mema
  Maovu kutoyatia
   
 8. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kumbe mjomba ana wapinzani.........kweli kukumbatia maji kama jiwe ni ujinga...
   
 9. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #9
  Jul 15, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Big up to you Mbogela. Nimeipenda mistari yako, japokuwa hujaiweka katika hali ya ngojera wala shairi, lakini mistari imesimama.

  Big up to you Mwanakijiji too. Excellent work. Wengine hatuna hata clue mtu anaanza kutunga mashairi kama hayo. Its a God given talent I guess.
   
 10. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #10
  Jul 15, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Hata mimi nikisoma mashairi ya MM huwa nashngaa sana, maana inanichukua nusu saa kwangu kutoka na beti moja, na nahitaji kumusi iliniweze kupata maneno yenye vina vinavyofanana. Hongera MM kikubwa meseji za ujumbe zimetulia.
   
 11. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #11
  Jul 15, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Eti Kula Huku Kula Gani?

  Kula huku kula gani? twala tulichootengewa
  Kula huku kula gani? wakati si twarushiwa!
  Kulahuku kula gani? twala tena twasindilia
  Kula huku kula gani? cha watoto wasingizia

  Kula huku kula gani? twala mchuzi na mbilimbi!
  Kula huku kula gani? Mmetupa kwa bakuli!
  Kula huku kula gani? Nyi wenyewe wala si wakali!
  Kula huku kula gani,cha watoto wasingizia

  Kula huku kula gani? mbona bado mwatusifia
  Kula huku kula gani, twawapa kitenge na bia
  Kula huku kula gani? Tisheti,mchele mwapokea
  Kula huku kula gani?,cha watoto wasingizia

  Kula huku kula gani, makofi mbona mwatupigia?
  Kula huku kula gani?twawahonga vibajia!!
  Kula huku kula gani?,gari zetu mwadandia!
  Kula huku kula gani? cha watoto wasingizia

  Kula tumeshakula,na bado twaendelea
  Mtabakia masakala,vitambi vyteu vyaning'inia
  Kulala mmelala,na mtaendelea kusinzia
  Vitenge,pilau na bia!, Kura mtatupatia
   
 12. B

  Bint Member

  #12
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimefurahishwa na ulivyojibu!
   
 13. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #13
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  [FONT=&quot]Kula huku kula gani, hadi ndoto mnakula,
  Kula huku kula gani, mwaota mwala vitamu,
  Kula huku kula gani, pia mwajua mwala si vyenu,
  Kula huku kula gani, sasa mwatafuna mpaka magodoro?[/FONT]
   
 14. M

  Msindima JF-Expert Member

  #14
  Jul 15, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ndo maana naipenda Jf kuna burudani kweli yaani nimefurahia sana shairi la mwanakijiji,hongera mzee mwanakijiji,kweli Kula huku kula gani tutakula mpaka madege yasoliwa kwa uroho wetu.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Jul 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Unajua kimsingi mtu anakula kwa sababu ya njaa. Lakini inakuwaje pale mtu anakula wakati ameshiba? Ni kitu gani kinamsukuma kula hivyo?

  Nimependa majibu yenu nyote hususan Mbogela.. aisee hapo umezama sana..ningependa kuitumia hiyo kwenye Cheche; AmanG, jibu lako kwa kweli linadokeza tu kile kinachoendelea mawazoni mwa watawala wetu.. Naam!
   
 16. Kobe

  Kobe JF-Expert Member

  #16
  Jul 15, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 1,756
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Hongera pia.
   
 17. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #17
  Jul 15, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hongereni sana wote wenye vipaji hivi....vinaburudisha na kutoa ujumbe mwanana.
   
 18. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #18
  Jul 15, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mzee M.M.M
  Hakuna shida kuibandika kwenye Cheche.

  watu wameshiba bado wanakula hawa tunawaita walafi, kipindi fulani mimi na rafiki yangu tulifikilia kuwa ngoja tuwatoe majirani zetu, unajua ilikuwa krismas, tukawaomba jamani tunaomba leo tukawape moja baridi moja moto. Basi wale majirani wakafurahi sana, kwanza kwa sababu tulikuwa siku zote wanatudhania kuwa tunawa-ignore na kuwafungia vioo. lakini pia walikuwa wanatusikia sisi ni watu wa kutumbua sana tukiwa kwenye viwanja vya starehe.

  Kufika kwenye kiwanja chetu tukaanza kuzigida, mara agiza nyama choma, sijui supu ya mkia, chapati whaterver ili mradi tuwape hawa majirani raha ya pombe (mimi na rafiki yangu ndio walipaji, No cost sharing). sasa wakawa wameutwika kisawa sawa lakini kwasababu hii ofa leo ndio imepatikana basi wakawa wanatoka kama wanaenda kupata huduma kwenye vile vyumba vyetu vya kupata huduma ya kupunguza maji mwilini. basi kufika huko Mzee unajua walikuwa wanafanya nini?? wanaingiza vidole mdomoni watapike pombe alafu wanakuja kukaa mezani tuendelee kunywa, mmmmmh can you imagine? Mtu kama huyu tumuite nani? Mlafi? sina jina, maana ameshiba katosheka bado anajitapisha swala aendelee kufakamia maji. Hii ndio nchi yetu, hakuna kuridhika, watakula tu.

  Ulisikia habari ya yule jamaa aliyekuwa anaagiza suti zake kufuliwa uholanzi?? (sijui habari hii kama ni ya kweli) lakini kama kweli utashangaa, ukafulie suti Uholanzi isafirishwe kwa DHL bado uje uvalie kwenye Vumbi la Makete, haiji akilini, lazima uwe punguani fulani, Mkuu ukija kijijini kwetu na DVD player watu hawataioona umuhimu wake, kwani sisi kule tumezoea redio kaseti yenye kanda zinazoimba Kasongo yeyee, sasa hawa wakuu utashangaa wanafanyia shoping paris, London, hawajui kuwa hizo nguo zao na vitu vyao havionekani thamani kwasababu wakuona hizo thamani wapo Hoi tabani, wanalala chini huko hospitali.

  Wananchi wanatembea kwa miguu kushuka na kupanda Livingstone ranges (Km 2900) kutoka Tukuyu (Mwandosya) Kyela (Mwakyembe) kwenda Makete (Mahenge) kuuza na kununua ndizi na maparachichi. watu hawa wanapigwa jua na baridi milimani huko, hawa hawahitaji mashangingi, wanahitaji basi la siti 60 wabanane wafike huko waendako wanashangaa wanapomuona mkuu wa wilaya pekee yake anatembelea Landcruiser VX/GX ya zaidi ya milioni 70 wakati afisa Elimu, Hospitali ya wilaya haina Ambulance. wanajiuliza kwanini hawakumnunulia Mkuu wa wilya Landrover ya Milioni 25 ili pesa inayobaki inunue Lnadrover zingine mbili kwa ajili ya Idara ya Elimu na Hospitali? hakuna wa wakuwapa majibu.

  Wakati umefika wasitudanganye na hii hoja yao ya kuwa hata hao wapinzani wako wangapi kuwapa nchi waongoze, Mmoja aliniambia ukiwachagua wapinzani hata baraza la mawaziri lenyewe hawatoshi kuunda. Wanasahau kuwa kila mtanzania ana haki ya kuchaguliwa kuwa kiongozi, Vipi wao wajione wana haki zaidi, vipi wajione kuwa walio kwenye chama pekee yao ndio wanaweza kuongoza?

  Tutajaribu, tumeamua Enafu izi Enafu, Enzi za kuambizana utulivu na amani uliletwa na chama sio kweli utulivu upo kwasababu sisi wote kama Watanzania tumetulia, tunawambia kuwa Amani ipo kwasababu hatujaamua kuchukua mapanga na kukimbilia msituni, na wala hatufikilii labda wao ndio waanzishe.

  Mzee M.M.M Ukitafakari sana haya mambo unapatwa na hasira sana, hakuna sababu ya kupata matibabu kwa kufahamiana, hakuna sababu ya kuogopa kuendesha gari madirisha wazi jijini Dar, hakuna sababu ya kukalia matofali darasani kipindi hiki, hakuna sababu ya watu kufa kwa maralia karne hii, hakuna sababu ya kushindwa kuwapa maji, wakati nchi kama Botswana unakunywa maji kwenye choo cha stendi gaborone, maji hayakatiki na yameletwa kilomita 600 kutoka kasikazini ya botswana iweje sisi maji kutoka Ruvu yasitoshe Dar peke yake?,

  Hizi sifa za kusema sijui anakubalika kimataifa ni zakupumbazana, kukubalika kimataifa maana yake nini? Wanyonyaji siku zote wanamkubali mtu asiye mbishi anayekubali sera zao za kuwanyonya. Hatuhitaji kukubalika kimataifa tunahitaji mataifa yatutambue yatuhesabu kama Patners kwenye biashara, hii dhana ya misaada inatumaliza jamani. NIMEAMKA WEWE JE?.
   
  Last edited: Jul 15, 2009
 19. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #19
  Jul 16, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kula wataendelea kula sisi ndio tunawapa kula
  Kula wataendelea kula, sababu sisi tumelala
  Kula wataendelea kula, watanzania ni majalala
  Kula wataendelea kula, sababu tunapenda wale

  Kula wataendelea kula, milele na milele
  Kula wataendelea kula, hata tukipiga kelele
  Kula wataendelea kula, uku wanapiga vigere gere
  Kula wataendelea kula, sababu tunapenda wale.
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Jul 28, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  safi!! hii nilichelewa kuiona!
   
Loading...