Kula Breki!!!

Sura-ya-Kwanza

JF-Expert Member
Nov 17, 2007
566
10
Baada ya kutoa dukuduku ya Uwezekano wa JF kugeuzwa kuwa chama cha siasa, mitafaruku yaanza kuonekana katika baadhi ya wana JF hao.

Baadhi ya wakereketwa wamesikika wakisema wanajitoa mhanga kwa kile kinachosemekana kuwa wana JF kadhaa walikuwa hawana imani na HE.J.K.... kwa hivyo basi wanarudi kwenye chama tawala


Mmoja wao alinukuliwa..."Kwa kadri ninavyochukia dhana na mifumo ya vyama vya siasa na siasa zenyewe (kama zilivyo na zinavyoendeshwa Bongo), naanza kukusanya virago vyangu kuondoka humu kama kweli jambo hili litaonesha dalili zozote kudhihirika hapo baadae!", alikaririwa.

Kwa kuwa wana JF wamejizatiti baadhi ya wanachama wake wakereketwa wamewataka wanachama hao kungatuka!

Vyanzo vya habari hizi zinapatika katika midahalao mingi ndani ya JF!

By Thread-o-journalist ;)
 
Last edited:
Jamaa ni mzushi halafu ni 'intateina' mzuri sana........namfananisha kwa mbali na yule mtunzi wa mashahiri na hadithi za mapenzi, bwana nanilii( jina kapuni).
 
Habari zinazotiririka kwa njia ya streaming zinaonyesha mshangao Mkubwa kwa wanavijiji makada wa upinzani na hata chombo cha habari cha sahara na hata kufanya maengineer kuchangaya nyimbo na papa baharini !:)
Haya yalibainishwa leo na mwandishi wa kugandia(embedded journalist)ambaye
alimnukuu humu msanii mwingine alieapa “ngoma ni kugangamala mpaka kieleweke” Na wasomi wa mdahala huo walipiga kichuguu pale waliposhindwa kusoma sentensi hii Labda "amejitoa" mhanga; siksoma posts zote. Wasomi walibakia wamebutwaa na siksoma yake!:eek:

Wakati mwanga wa mbalamwezi unamulika jukwaa hilo la mdahalo huo ilikuwa vigumu kutofautisha kiongozi na kingozi!;) Na mtu mwingine aliyeonekana kama mzungu ambaye alijulikana kwa jina la Ben alirudisha nyuma maendeleo ya Kiswahili, alinukuliwa akisema wakati wa mdahalo huo “Ila unadhani wewe kuwepo hapa JF kunarudisha maendeleo nyunma au mbele.” Ilisema sentensi hiyo kinyumna nyumna!
Mpaka tunarudi mtamboni bado ni Hasara tu kujitoa katika mdahalo huu unaoendela

Mwandishi wa Kugandia(embedded journalist)
JF Vijijini.
 
Ndugu zangu mimi ndiye niliyesema hayo ya kujitoa humu JF (wala si kujitoa mhanga!). Ila hayo ya kurejea kwenye chama tawala ndiyo UZUSHI WA HALI YA JUU! Mimi si na wala sijawahi kuwa wala sitakaa niwe mwanachama wa chama cha siasa! Someni maoni yangu sawasawa na kwa usahihi!
Naomba mtoe hoja na si kupandikizia wengine hoja!!
 
Jamaa ni mzushi halafu ni 'intateina' mzuri sana

your nameis mine nop ni mzushi tu but never an entarteiner but rather a borer.Masikini hajui uandishi ni kipaji kinachohitaji kujituma kwa uadiifu na si vinginevyo. Mi nashauri ajiendeleze ili awe na constructive ideas zaidi kuliko pumba.
 
Na mwandishi wa kugandia(embedded journalist):)

Kalamu ya mwana harakati mmoja kutoka JF Ville yakutana na Upinzani na Uadui kwa maandishi "taarifa nzito sana isiyohitaji utani" lilimwaga kalamu hiyo. Wakati huo huo kalamu hiyo ilionekana kama imehukumu haraka na ndio wanavijiji wa JF Ville walipookoa wino wa kalamu hiyo kutoka kwa maadui na wapinzani kwa kusema watasidia kuweka maandishi hayo hadharani!
Naye mwanahudhuria wa JF ville JINALAKOlako aliiona kalamu hiyo Hardball! wakati mjumbe mwingine akionyesha umahari wa juu wa kike wa kiafrika kwa kutumia wino mwekundu ipasavyo kuonyesha sehemu zilizokosekana wino wa kalamu!

Miungu huko JF Ville iliamka pale Sala na Injiri za Maria ziliposikika "Boss, you are blowing this issue out of prportion unnecessarily" ilisema moja ya injiri hizo! Bila kusita kalamu hiyo ilimwaga maandishi na kubaini injiri hizo hazipo. Wakati wino huo wa kalamu kuonyesha udhaifu katika maandishi, Umahiri wa kike wa kiafrika wa kutumia wino mwekundu ulipooneekana... Vilevile Wanavijiji waliona huu wino wa kalamu umeisha na kushauri uongezewe maji" Kama hukumaanisha makali ya maneno hayo unaweza kuyamwagia maji kidogo..." mwandishi wetu alinukuu

Naye Mkuu wa majeshi wa JF Ville(Field Marshall) aliomba waongeze wino wa kalamu "wekeni facts hapaa..." alihamaki. Fundi mwingine wa JF Ville aliona kauli za mkuu huyo kama tageti "Tatizo? aliuliza na kuongeza..."Ni kuwa target wa wasiopenda watu..." pale pale mkuu huyo alijibu na kusema "sina any apology wakuu..." Mkuki kwa mkuki au kwa kininiho "spade ni a spade tu"

Mpaka mwandishi wetu akirudi mtamboni kalamu hiyo ilionekana inaisha wino! Habari zaidi bofya hapa...Kwa kweli Upinzani si Uadui!
 
Last edited:
nilidhani ni proposal ya kuanzisha JF gazzete lakini kumbe kuna mashairi humu... lol
enewei alisema YESU "yaacheni magugu yakue pamoja na ngano" ila siku ya mwisho yatang'olewa na kutupwa motoni....

Natoa ushauri kuntu kwako sura ya kwanza,
kama una dhamira safi ya kuendeleza mdahalo huu hakikisha unagandia nukuu za kweli ili hatimaye mlengwa aweze kujibu au kufafanua hoja ulizomnukuu na usimfanye mlengwa kusahihisha kwanza nukuu.
kwa kuwa haujawahi kuninukuu sina ugomvi nawe kwa sasa ila patakuwa hapatoshi hapa endapo ukaninukuu kisha ukakosea....
 
Na mwandishi wetu wa kugandia(embedded journalist)

Kaka wa fedha taslimu wa JF Ville au (CMB) alinukuliwa "Serikali kushindana na JF"
Kwa kile ambacho kimewashangaza vijana na watoto wengi JF Ville ni pale bubu mmoja kuongea ! Bubu huyo alisikika akisema "Hawatakuwa na mafanikio makubwa" na ndipo shilingi iliporushwa kuona upande mwingine wa serikali na ndio ilipobainika kuwa DNF(Daily New-Forum) Danganyika!

Mda mchache baada ya vuguvugu hilo kuanza mwandishi wetu alinukuu "nani mjinga atakwenda kupost kwenye site ya serikali na issue serious?" Aliuliza mwanahudhuria mmoja wa JF Ville. Naye mwanhudhuria mashuuri (m-the great) alidai DNF ni propaganda "Dunia ya hoja yenye msingi na ukweli siku zote hujitenga na Propaganda"

Mda mwingine haukupita kwani kombora aina ya ‘rpg' ilipigwa DNF na kusema haita acha hata chembe moja ya huko! Mlio huo wa kombora hilo uliwaamsha wanavijiji wa JF Ville na kuona ni rahisi zaidi kupigana makombora hayo kwa kujiunga nao-" naenda kujiunga nao nione" alisikika mwanakijiji mmoja huko... Wakati huo huo ngurumo za kombora hiyo ilimtoa nyoka gamba shimoni mwake na kusema "halafu nimecheki list yao" mwandishi wetu alibaini.

Wasanii JF Ville hawakuwa mbali kwani michango yao ya sayansi kwenye midahalo huitajika…wasanii waligundua kwa kufanya uchunguzi wa taipureta kuwa wana DNF(Danganyika[sic] News Forum) kuwa sio asili "niliwaambia…sio mwenzetu ana asili…angalieni typings..." Ulibainisha uchunguzi huo wa kisanii. Hii iliwafanya watanzania waishio huko JF Ville kuanguka kicheko "kwi kwi kwii"

Tahadhari: "Tangu nijiunge JF nimekuwa kiakili na sasa nategemea kuoa karibuni" Haija julikana kama ni ndoa ya Mwana JF na Mwana DNF au ya JF na DNF.
Nayo nyota moja huko JF Ville ilingara pale ilipoonyesha wazi jiko la DNF na kuonekana vyakula havipakuliwi na vimejaa nyongo! "Natumaini watakuwa…bila kinyongo" alinukuliwa. Naye mwanahudhuri wa kujisafisha alisema DNF ina wasaliti ambao aliwataja kwa ‘ID zao kede kede'([sic])

Umahiri wa kike wa kiafrika haukupitwa, kwani alifanya utafiti kwa kutumia supa(office)kompyuta kuona nguvu ya DNF na kubainika "Wana system kali sana" hata hivyo alisitisha zoezi hilo kwa kile alichoamini kuwa JF Ville kuna "Protection ya ID's za membaz wake." Bila ya kueleweka tahadhari nyingine ilitolewa kwenye mdahalo huo "JF, hiyo kuweni macho," kilieleweka.! Wanakijiji nao, waliogopa, pale walipogundua "wana system kali sana" na kujihoji.

Tahadhari hizo ziliendelea kutapakaa JF Ville na kufikia JF Ville forest reserve, Nyani huko aliuliza kama watu wanajua majina yao…alijiuliza na kujijibu "labda uwe unaishi kwenye kisiwa…" alijijibu na kuona! Lakini kwa kile kilichomshangaza mwandishi huyu ni kule Nyani huyo kula babaiku kila wikiendi. Hii ilimwacha hoi mwandishi huyu alipobainisha hayo na kujiuliza, ‘Nyani hula babaiku'? Kwi

Mwandishi wetu pia alibainisha kuwa maarifa ya JF ni kuwa tayari na madongo "niko huko tayari…NITWAPA madongo…" alibainisha. Maarifa hayo yalipigwa ki-mkumbo!

Mjadala huo uliendelea mpaka pale mainjinia wa DNF walipoomba dua na ushauri "sisi tukiwa kama IT-technicians ‘Danganyika News Forum' tufanyeje?" Dua lake lilijibiwa na kuonyeshwa picha ya jinsi gani wafanye!

Wakati mwandishi huyu akirudi mtamboni wanahudhuria na wanaharakati DNF walidai Insurbordination imefanywa , mwandishi wetu amepelekwa huko kutuletea kisa mkasa.

Kwa habari zaidi bofya hapa……
Na hapa....
 
Last edited:
Hivi karibuni mwandishi wetu aliweza kuwaletea habari za midahalo Na jinsi gani hoja hizo huchambuliwa. Baada ya kutoa dukuduku ya uamuzi wa “JF kugeuzwa kuwa Chama?” Kura zilipigwa na asilimia 64% iliyona Yawezekana na asilimia 36% kama haiwezekani! Ni baada ya hapo tu ndio mdahalo wa Serikali kushindana JF kuibuka na kuleta hoja kede kede. Midahalo haikuishia hapo tu JF iliweza kuona ongezeko la wanahudhuria baada ya kuwa na wasiwasi wa usaliti wa wana JF Ville kwenda Danganyika (DNF) Ndio hapo mwandishi wetu wa kugandia (embedded journalist) alipopelekwa huko kuona kisa mkasa . Hapo chini ndio yaliyoletwa na mwandishi wetu….

Wanakijiji wa JF Ville waanika uwani Taahiri za mhariri mmoja wa Danganyika News

“Whoever wrote this crap should be fired!” Madogoli yakaanza kusikika JF Ville ambayo ilimfanya Muganga(haijathibitishwa kama ni wa kienyeji au la)kwani aliweza kutabiri jina baada ya madogoli hayo “Nafikiri mwandishi huyo ni salva” alitabiri.
Na mkazi wa maeneo ya mbunango huko JF Ville ambaye sasa ni mwanahudhuria wa JF Ville aliongeza vituko vya kisiwani kwa kuuliza “Kuna tatizo gain hapo juu?” Wanakijiji kwa kuona mkazi huyo kama ameshausweka bia badala ya maji walimsubuhu kwa kumuomba asome “you need to read…”kwani hakuona madogoli yalipokuwa yanachezwa! Mikumbo ilipigwa huko kwani insubordination ndio ilionekana tatizo.

Haikuishia hapo kwani wakati madogoli yalipokuwa yakipigwa Dua zilisomwa “He is the president…unless he dies”. Miujiza mingine ikafuata huko…kwaani kwa kujiumauma kibogoyo mmoja aliweza kutamka “The president is responsible for all maters in Tanzania so are Tanzanians” Kumumuna huko kulimfurahisha Nyani, kwani aliruka na kujipiga kifuani “hey” alihamaki “mwite mbwa, taka…That’s called democracy People alisikika akiwaambia watu.

Wanakijiji wa JF Ville walijikusanya na kuamua kufanya upasuaji wa Taahira huyo (read taahiri/mhariri) Nyani alikubali upasuaji huo kwa kile alichoamini utabainisha kama huyo taahira (soma mhariri) yuko smart “After you do that…if they are smart…” tutajua! Wawakilishi walikubali kwa pamoja “well said…well said… nacho kituo kimoja cha sauti ya kusini mwa sahara lilitoa support “I support you”

Wanahudhuria wengi walifika huko na kutoa hoja zao ambazo kwa kweli ziliweza kumfanya Taahira yule wa Danganyika asilale usingizi mnono kwani madogoli ya JF Ville hayazimwi usiku na mchana, kwa kweli madogoli hayo yalisikika Danganyika.

Mwandishi wetu ilibidi aondolewe huko mapema kwani midahalo bado inaendelea Huko JF Ville
Bonyeza hapa...https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/7572-leave-president-alone-you-insurbodinates-daily-news.html#post104521
 
Last edited:
Mkandamizaji mmoja wa JF Ville adai Waziri kuwatumikisha wasichana( mwandishi wetu aligundua waziri ni mwanamke)

Umempa? Umempa? alisikika akiuliza kuhusu madai yake. Mwandishi wetu aliweza kubaini yaliyotokea huko kwani alikuwa amejigandia(embedded)

Mkandamizaji huyo aliendelea kuuliza

“Je Bi Salha kama unavyo jiita ama unavyo penda uitwe umemuombea, Unaongea nini Bungeni, unatenda nini nyumbani…?” “mtoto wa mwanamke mwenzio pia…?”, Hebu tueleze ya kuwalipa kiasu cha shiling 100,000 wachache hawa,? “wewe ndugu waziri nawe uingie….”

Mwandishi huyu alibakia na butwaa kwani alikuwa hajui huyu waziri alikuwa aingie wapi, kimaswali-maswali. Ilikuja kugundulika Vijana nao walihusika:- mkandamizaji aliwataja baadhi “Kuna Jamila,Esther Mlokole, Jesca, Tabu, Judith.” Butwa likazua Butwaa Vijana nao majina wamebadili au ndio majina yao ya kinyemela…mwandishi wetu aliendelea na butwaa na kujiuliza kimaswali-maswali!

Watu wenye akili timamu huko JF Ville nao hawakutaka kupitwa kimaswali-maswali… “Shame Shame Shame” walisema kwa utimamu…. “in bongo, go figure!” Naye mwanhisabati mmoja wa ugomvi wa kuingiliana(conflict of interest) alidai anaenda kuchuka mahindi ya milipuko(pop-corn) tayari kwa maswali maswali na majibu. “hii itakuwa tamu zaidi weekend ikifika” alisikika akisema wakati akibwagia mahindi milipuko hiyo.
Mwanakijiji mmoja wa JF Ville naye aliona mahindi milipuko ndio haswa pakuanzia alisikika akisema “Hata mimi, I need to recharge my battery.. I'll be spinning a lot”. haikueleweka kama ana charge betri tayari kwa mahindi milipuko au ana spini kwa utamu unaokuja.(udaku)
:D
Naye akiongea kama kipenzi cha walalahoi wa JF Ville bila hata ya kujua alikuwa akinukuu kitabu kimoja kikuu “Mungu Wangu Eeeh!!!” alisema kwa mshangao na kuongeza “Inatia Shaka Serikali Kuwa Na Mawaziri Wadini Namna Hi.. Hawachelewi Kutoa Amri Za…'Ghasia” alisikika wakati upepeo mwananana ukitokea pwani ya JF Ville. mwanahudhuria wa JF Ville–Pwani divisheni aliona havinogi “hivi mada hainogi mpaka tusukume huko au tukandamize kidini” alisema kimaswali.

Mkuu wa majeshi JF Ville naye alijibu mashambulizi kwani aliona ujasusi watawala na kusema “unatamka wazi wazi kwamba Wakristo si watu na walio watu wa dini hiyo kwako they should stop practising it wakiwa watumishi wako ? Whaaat? Aliuliza kiunaga ubaga.

Maswali yaliulizwa kimaswali maswali na majibu hayakuwa ya kutosheleza pamoja na mkandamizaji huyo kudai madhambi yalitendeka na kuwa na data…” nikiwa na data kibao ambazo nangoja, Jiulize kwa nini wanakuchukia kabla huja anza kuwa mtu wa vituko” alisikika akimuuliza Waziri huyo kimaswali-maswali wakati ukweli ulibakia data hakuwa nazo na vituko alianzisha kwa ukandamizaji.

Mpaka wakati mwandishi wetu kujigandua huko ukweli haujajulikana.

Kwa habari zaidi kuhusu Salha bofya hapa....
 
Last edited:
Ujasusi wakoromea wana JF Ville.

Bofya hapa kwa zaidiTahadhari members wa JF
"Wewe memba wa JF unayenitumia PM kila mara kunionya kuwa niwe makini" - "Niko hapa at my own risk!:mad: ", alionya. Tahadhari hiyo ilisikika.
Umahiri wa kike wa kiafrika wa kutumia wino mwekundu ulidhihirisha hiyo tahadhari
"Napenda kuwatahadharisha na PM kutoka kwa some new members ambao wameingia hapa in the last 2 to 10 days. Hao memberz wanatuma PM kwa members wengine…walipata virus"

Mwakilishi mmoja wa majimbo ya JF Ville alitoa shukrani kwa tahadhari hiyo. Kwa kutumia kanuni za uendeshaji wa JF Ville alitoa onyo kali kwa yeyote anaye husika "we dare talk openly", "yeye aanzishe tu thread yake atoe madukuduku yake ili mradi hakiuki TOS"
Aliongeza.

Mwandishi aliona vile Wanahudhuria JF Ville na wale wanaoishi karibu na Nyumba inayohifadhi mchwa na nguchiro kwa pamoja bila mkwaruzo walivyoshtushwa na hiyo tahadhari kwani waliona bora na wao(virusi na minyoo):D watolewe hadharani! "…ninadhani kuwa ingekuwa vizuri kumtaja mtu huyo anayezua upuuzi huu kusudi itusaidie kupanua mtazamo wetu:confused: wakati tunasoma posts zake." walisikika
Wafwatiliaji wa mambo huko JF Ville na wenye mtindio wa ubongo JF Ville Rehabilitation center:) walikubaliana(thank) na jirani kutaka atajwe.

Lakini kwa kile mwandishi wetu alivyobaini kwa kutumia luninga ya tarakilishi:rolleyes: ni tofauti na maandishi ya kalamu kwani kalamu hiyo iliandika tofauti na mtazamo wa hapo juu… "Kama Mkjj ni mwanausalama, he must be a very lousy one!". Ehh!

Kaka Mkubwa wa Makaka wa watu wa organaizesheni ya Kaka na Dada JF Ville nao bila ajiza walisikika "And who cares….Usalama wa taifa?… maskendo mengineyo humu:eek: " Mwandishi wetu alibaini.

Nao wananchi wengine wa Ngambo,walitahadharika kwani waliona nako nchini kwao Tanzania labda kuna jambo. "JF sipawezi, yaani mara hii Mtanzania…, …. ni wana usalama" walisikika kimaswali maswali. Lakini hawakuacha hapo kwani waliona labda ni vibaka "Hao ni vibaka tu wanajaribu bahati zao na wala hawana la maana lolote" na ndio pale alipobainisha labda mmoja wa wanakijiji wa JF Ville ni mwanausalama (haijajulikana).."Mwanakijiji atakuwa mwanausalama…" Mkuu wa majeshi JF Ville na yeye alimshukuru(thank) mwana wa ngambo huyo kwa Taarifa hiyo.

Ukimya wa JF Ville Forest Reserve haukuwa tena, kwani wanyama wa huko walihakikisha hatishwi Nyani:D "mkijua kuwa Nyani Ngabu ni mwanausalama wa taifa…" mwandishi wetu alibaini pia kuwa umdhaniaye ndiye siye na kinyume chake.([sic])Mcheza sinema wa JF Ville Forest Reserve alisikika "Nyani nakumbuka sana… wewe ni usalama…" (alisema kishreki shreki). Katibu wa tarafa moja karibu na reserve hiyo nae aliona tahadhari hiyo na wanahusika ziwekwe bayana "pasua pasua mweke upenuni huyo wakuja iliashuhudiwe na kadamnasi"

Wengine nao walinukuliwa...
Wachambuzi yakinifu "JF we talk about facts in Economic,Political and Socially" :rolleyes: , wakandamizaji "Pole sana huyu jamaa hajaoa labda anataka kuleta neno hebu mvumilie uone mwelekeo wake kwanza:cool: ", na wenye umri mdogo mdogo "tusianze kuwa majuha wa kujadili kitu bila ushahidi :mad: " walinukuliwa huko.

Kwa habari zaidi fuata unganishi "Tahadhari" hapo juu!

Wakati mchakato huo ukiendelea ujasusi ulifanywa na ikagindulika chanzo cha Tahadhari hizi JF Ville. Daktari asiyejulikana alibainiswha ndio chanzo gonga hapa...https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=8128

Wakati mwandishi wetu akijigandua huko hoja zilizuka nyingi za kijasusi. Je, 'jipu' hili litamuuma na kumkosesha usingizi Mkjj au litasinyaa na kutoweka bila hata kovu kubakia? Naomba Udhuru N.K
 
Last edited:
Na Mwandishi wetu.
JF Ville Mjini.

Kwa kile kiliochoonekana Ukosefu wa madawa katika JF Ville Rehabilitation Centre Wakurugenzi , madaktari, wana-dini na mtanzania mmoja wamejaribu ku priskraibu dawa mbadala. kwa kile kilichoonekana kana mikwaruzo ya wenye mitindio ya hoja.

Wakati huo huo Mazuzu:cool: wa JF Ville Rehabilitation Centre, waomba kazi, wakati huu mgumu.

Wakuu wa huko walipata patashika hii na mwandishi wetu alipelekwa huko kuona kinachoendelea.

"Jamani mimi natafuta kazi Amerika… process inanichanganya:eek:, Ntaka kuhama hapa nyumbani":???:

Uzuzu wake haukuthibitishwa na mwandishi huyu kwani patashika ya huko Rehab iliokana kama tatizo.

Mwandishi aliweza kubainisha kuwa haya yalisemwa kutokana na ukosefu wa madawa ya midahalo.

Mtanzania, mmoja tu, amedai ukosefu huo wa madawa haya umeleta kashfa:(,kebehi:rolleyes:,matusi:p na mengine ambayo hayakubaliki katika jamii. Yamekithiri! Alisikika akisema. Mwandishi wetu alimnukuuu "Kwa bahati mbaya au nzuri, niliyemuona amekithiri ktk matumizi ya namna hii ya maneno ni Bw. Mtindiowaubongo" ...aliendelea kudai, 'lugha zimeachwa na hazithibitiki'

Watu wenye mitindio ya hoja, mazuzu, wazua uzozo, wenye kebehi na matusi wote wanaweza kuonekana huko JF Ville Rehabilitation Centre kwa matibabu tofauti.:D

Mtanzania huyo aliendele kuuliza menejimenti ya huko JF Ville Rehabilitation centre, kulikoni?

Watu wa JF Ville hawakuchelewa ku-pri-skraib madawa "Aise huku…Mpe *maandiko, *vifungu…*mtaelewana" kana kwamba maandiko na vifungu havitoshi. Wanataaluma wa JF ville walisikika wakisema kwa mara ya pili "second…*be warned or *banned" mwandishi wetu alibaini.
*Madawa haya hayajathibitishwa na JF Ville Drug Administration.:cool:

Naye bila yakujulikana anatokea wapi aliona madawa asilia hayawezi na kutaja baadhi kwani alinukuliwa " Ndugu yangu hatujapaona huko…unajua kuna kondoo,.. utumbo":mad: Kwa kile mwandishi huyu alichobaini ni yale yanayoendelea huko JF Ville Rehabilitation centre,hakujua hizi dawa asilia ni zile za babaiku au la, lakini kabla hajanyanyua vidole vyake kutoka kwenye taipu-reta –ya-tarakilishi, bila ya yeye kuonekana lakini anaonekana kama mkurugenzi wa JF Ville Rehab, aliongeza kuwa labda dozi ya 1month ban itamfaa. Dawa hii huko juu ilibainishwa ni kali. Alimaliza kwa kuomba radhi kwa walioathirika "Kunradhi na walioathirika huko" vilevile alishukuriwa kwa hili.

Wanahudhuria wakasana kuona madawa hayo yanafika hata ikiwa kwa kuombewa "Dini Dini"

Habari zilitapakaa JF Ville kwa kile kilichoonekana kama mwarobaini na klorokwini kuchanganywa(hukumu), mwanahudhuria mmoja wa JF Ville Rehabilitation centre mwenye utindio wa ubongo aliona ‘kumkoma nyani giladi mchana kweupe ndiyo chanzo cha magonjwa yake ya hoja , alidai. "Kuna vitu kadhaa hapa inabidi viwekwe wazi maana naona hata regulators/moderators wanaanza kushindwa kuelewa na kulinda ile dhana ya kumkoma nyani giladi mchana kweupe.:mad::p:twisted:" Alinukuliwa .

Source:https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=8727
https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=8685
 
Last edited:
Baada ya sakata la JF Ville Rehabilitation kuyoyoma, sasa hisabati za kitengo kingine cha mambo yasiyokuwa ya ndani JF Ville haikubaliani na hoja za Waziri mmoja wa nchi wa mambo yasiyokuwa ndani kuhusu kuteteta hisabati za safari za wakuu wa nchi hiyo.


Mwandishi wetu akitumia luninga na taipureta ya tarakilishi alileta habari hizo.


Hisabati za ugomvi unaoingiliana za kitengo cha mambo yasiyokuwa ya ndani JF Ville haikubaliani na hoja za waziri wa huko, MEMBE.:mad: Kwa kweli, mwandishi wetu alibaini jina nalo limekaa kimraba-mraba. Membe huyo alidaiwa kujuana na watu wasio punguani wa John Hopkins.:cool:

Waziri asiyekuwa wa ndani alinukuliwa(sio na mwandishi wetu) "Ataanda orodha" Asema safari zina tija, adai nchi za kusini mwa afrika na uganda wakua kiuchumi kutokana na hisabati nzuri tu za wakuu. Mwandishi wetu aliweza kunukuu hisabati hizo hadharani.

Kwa kile kinachoonekana kama kuweweseka na mwanahudhuria mmoja huko, alitokea, na kuuliza "Hivi…. ana akili kweli? Akirejea kwa waziri anayejuana na John Hopkins. Aliendelea kuuliza kwa kihisibati zenye mbinu ya miundo…"Uganda na S.A…wameshaweka…barabara, maji na umeme…wawekezaji wa nini? Aliuliza kwa mbinu za miundo akitaka kujua kwanini hisabati za membe na JF Ville International and Strategic Studies Institute zinatofautiana.:(

Midundo ya kimasai, majasusi wa JF Ville wakiwa karibu na Nyumba ya nguchiro kwa kusindikizana na mwimbaji mkongwe wa huko walichezeshwa ngoma ya nyani- kigiladi- giladi:D pasua! kwani walimshukuru muweweseka huyo.:D

Mjumbe mwanahudhuri wa mtaa wa bulyankulu JF Ville adai mkuu huyo mwenye kumelemeta na Ari mpya (mwandishi wetu hajabainisha kama hii Ari mpya ni manukato au usemi tu) ameshajaza vitabu vitatu vya kusafiri-alifanya hisabati kwa kutumia formula ya "(Just Kidding)"- Mwandishi wetu aligundua hiyo fomyula ni ya kutoka JF Ville Statistical Mumble Jumble Institute.:cool:

"Membe anashangaza…Wawekezaji makini sio watu wa kusubiri kuitwa na kubembelezwa kuwekeza mahali, wao wana mikakati na taratibu zao za kusaka masoko na sehemu za kuwekeza mitaji yao" Alinukuliwa kihisabati sabati.

Mwanahudhuria huyo aliendelea kuongeza "Kuna urasimu sana…. ya njoo kesho,kwa sababu muda ni mali"
"Umeme unakatika bila taarifa…. Mvua zikigoma na umeme hakuna!"

Aliendelea kudai wakuu hawajui hisabati za kuwavutia wawekezaji" Viongozi wetu wengi hawana utashi…" "Shida ni nini? Aliuliza na kumalizia kusema "Ni Mtazamo tu!"

Kwa kweli mwanahudhuri huyo wa bulyankulu alishangiliwa exponentially.(thanked):)

Mdau mwingine mwanahudhuria wa mtaa wa ontario JF Ville ajulikanaye kwa ufupi tu yaani Fee-Dee alidai yeye hajakata tamaa na hisabati "Siku hizi ninakuwa mtazamaji tu.... ila sijakata tamaa ..." alinukuliwa huko.


Kama vile sinema za kung-fu za uchina kwa kumumuna mwanahudhuria mwingine huko ambaye ni babu:rolleyes:, alidai "Itakuwa vizuri tukianza kukusanya data za safari za Mbeki na M7 ili kujua ukweli umelalia wapi. Kwa kumbukumbu zangu za haraka haraka safari za Muungwana haziwezi kabisa kulinganishwa na Mbeki na M7, VDG anajichukulia Gold medal kirahisi kabisa." Aliongeza kwa kihisabati.

Walalahoi wa JF Ville nao waliona hizo safari za wakuu kama za enzi hizo za Vasco-de gama "Ana kila sababu ya kutetea utalii wa JK kwa sababu wote huwa… kwa huyu Vasco da Gama ..."

Bado mwandishi wetu yupo huko kuelewa hisabati hizi za safari za wakuu na waziri asiyekuwa wa ndani, wawekezaji, na hatimaye kupata uelevu ambao unaweza kusaidia kupata hisabati za kuongeza Wadakuzaji wa stendi ya habari Kula Breki!!! :D

Pindi habari zikiendelea kutiririka basi hisabati zitatawanywa JF Ville!.


Chanzo cha habari hizi bofya hapa...https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=8759na zingine... Sababu Mojawapo Ya JK Kwenda Nje Ni Hii? https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=8781
 
Last edited:
Baada ya nchi ya Tanzania kuondokewa na Mkuu wa Majeshi https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=8749

Mkuu wa uwanja wa kivita wa JF Ville adai akumbana na kikosi cha kijasusi cha midahalishi FEBEYINI. Atishiwa amani, aelemewa, anaomba msaada, baada ya mkuu huyo kuahidi kuleta siri kubwa kuhusu kile alichokiita ‘ishu ya Mwana-Halisi na acid'https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=8669

Majasusi wasioonekana hadharani:cool: kwenye jumba la mdahalo JF Ville walionekana huko na kueleza mbadala kinachoendelea.Kwa kile kilichoitwa ukimbizaji wa hati za maandishi kwenye mtambo unaorahisisha kazi ya mawasiliano na uwekaji wa rekodi na hesabu la midahalo JF Ville. Majasusi wa JF Ville walifikia wajibu, kwani walifanya maharamisho ya itifaki ya vidahilishi:rolleyes: kutokea ofisi za mkuu huyo ambayo ndio iliyonekana kianzio cha ukimbizaji wa hati za maaandishi ambayo yangeweza kuleta madhara katika mtambo wa JF Ville!. Majasusi hao, pia walidai ni uzembe wa hali ya juu hili kutokea kwa mkuu huyo.

Mwandishi wetu aliweza kudaka mwasiliano hayo mafupi ya ukonyezo kwenye mtandao huo…

"Wakuu wote heshima mbele, toka siku nilipo-post dataz kwenye ishu ya Mwana-Halisi na acid, na kuahidi kuwa nitaleta zaidi nimekuwa siwezi tena kuingia JF kuna maneno mazito ya kutisha ati kutoka FBI kwamba nikiingia mara mbili tu nitatafutwa nao, yaani FBI, sasa kwa wale mlio na ujuzi zaidi wa intrnet hebu nipeni info what to do najua kuna mfisadi mmoja ananichezea, he should know better kuwa hawezi kitu" Ilisema moja ya mawasiliano hayo

Kwa kile kilichoonekana hayuko kwenye ofisi zake baada ya kutishiwa mkuu huyo alikuwa kwenye aarat na hivyo kumfanya aende sefu pres, mwandishi wetu aliweza kunukuu alikojificha "Ahsante Wakuu nipo kwenye mtuwameli-AT-yahoo.com"

Mwasiliano hayo yalianza kujibiwa, kama kawaida ya kumkoma nya giladi…:mad:

Mhamiaji wa portugal huko JF Ville hakujua ni kwanini hao febeyini wanamtafuta au labda ni moja ya njia ya kijasusi kutoa data za ishu zilizopita "Hao wanakupiga fiksi tu mkuu, sasa (muted)'febeyini' watakutafuta ili iweje?:confused: labda wakuajiri kwa sababu utawasaidia kuwapa dataz za kuwapata wahalifu, (muted) si kama polisi yetu ya bongo." Alinukuliwa huko huku akipongezwa na majasusi wa huko.

Mwanamuziki mmoja wa JF Ville:) naye alijaribu kuondoa wasiwasi kwa mkuu wa uwanja wa kivita huyo, kwani aliona febeyini hao sio kama wa mashariki ya kati kwani febeyini wanaomsumbua mkuu huyo wana mapanga mabutu hivyo aliomba apewe butu hilo na kulifikisha kwa wahusika.:D ‘Mhh, (muted) wa kutumia mapanga butu? Alianza kinyimbo nyimbo:D "Naamini…nitamfikisha kwa wahusika":rolleyes: alimalizia

Kama kawaida ya patashika za JF Ville, mcheza sinema maarufu kutoka JF Follywood naye alinukuliwa (kishreki-shreki);)"You need not to spit it here FMES… "…huyo NDULI" mwandishi wetu alibaini hiyo FMES ndio jina la siri la mkuu wa uwanja wa kivita huko JF Ville! Mcheza sinema huyo aliongeza "Well, naamini wewe ni mtu wa ma-connection....utapata mtu wa kukupiga tafu Mkuu wangu" alinukuliwa kwenye mawasiliano hayo yaliyodakwa.

Wanahudhuria wengine huko nao walimuuliza mkuu huyo "unaongea ukweli au unapiga mkwara???:confused::confused:, kimaswali-maswali na kutoa ushauri kuhusu itifaki ya vidahilishi... "kama kweli wanakutafuta unaweza kuwa kwepa kwa kutumia komputa tofauti tofauti kwa mahali tofauti tofauti… una post…bagamoyo…kariakoo…' alimalizia kusema ‘hakamatwi mtu'.
Lakini kile kilichoonekana kuwa ni moja ya sababu za kijasusi kwenye ofisi za mkuu huyo mwanahudhuria huyo alitoa shauri jingine "Kifupi data mhimu inabidi watu wajifunze kuhifadhi ktk komputa isiyokua na mtandao yani haiko ktk internet(network of network)." Ilisema kiunaga ubaga.:)

Maandishi ya kalamu nayo yalinukuliwa "Haya nayo ni mambo makubwa ya JF. Mwaka huu tutaona mengi" alisema hayo mbele ya Nyumba inayohifadhi mchwa na nguchiro kwa pamoja bila mkwaruzo ambamo nako kulidakwa mawasiliano haya "Hao wanakupiga fix tu;(muted) febeyini hawafanyi kazi namna hiyo:eek:. Labda weka firewall kama itasaidia". Mwenye jina lako langu naye alijaribu kuondoa mashaka ya mkuu huyo "hakuna lolote, wanakutania tu;)."

Mwandishi wetu aliondolewa huko baada ya vichuruziko hivyo vya ukonyezi kushugulikiwa na majasusi wasionekana kwani waliondoa mara moja maharamisho hayo ya itifaki za midahalishi.
"Am really sorry that you were the victim of this damn ban. It wasn't my intention. I have released all IP addresses in this ban and you wont get such messages." Alimalizia kwa unyenyekevu "Thanks for your patience."

Kwa vimemo hivyo bofya hapa……https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=8830
 
Last edited:
Unajitahidi burazakaka, akchuali unakuwa beta bai ze dei.........inapendeza kwa "kura bureki."
 
Wakati Waziri asiyekuwa wa ndani wa nchi ya nga'mbo Kula Breki!!!:eek:


  • Sasa Mkono umetokea kumtetea Kipunguza spidi za mahela!:D

JF Ville kwa waka moto,Tena! .......Waandaa Resolution!


Mwandishi wetu wa kugandia amepelekwa kwenye majukwaa kuona kulikoni.
 
Sura-ya-Kwanza... unaniacha hoi, poa sana... Surely, You are a trend setter and not a follower!! lol
 
Sasa Mkono umetokea kumtetea Ballali!

  • Mwanakijii mmoja wa kutokea JF Ville atinga jukwaani na kubaini juu ya Mkono hu(y)o, Alinukuliwa JF Ville.

"Mbunge wa wasomi wa sheria Nga'mbo ya JF Vijijini-Musoma Vijijini Bw. Mkono amesema kuwa yuko tayari kumtetea aliyekuwa na Uhakiki wa mahela ya moja ya mabenki makuu Benki Kuu endapo Kipunguza mwendo wa mahela-Gavana- huyo atafunguliwa mashtaka katika mahakama ya sheria". Akitumia mkono...Aliashiria azma yake hiyo.

Nyota Inayongara JF Ville Follywood alicheka kwa kebehi "Ha Ha…:D" na kuuliza ki JF Ville Follywood lingo- "…baada ya kutemper na evidence...:mad:?- iligundulika, ‘kutemper' ni lingo ya huko! Mwandishi wetu hakuweza kubainisha kama huo mkono umashashika au kugusa ‘evidence'.Mwanahudhuria mwingine naye alinukuliwa akisema "Huu mchezo wa kuigiza una vibweka vingi:D. Yangu macho!":eek:

"Huyu Mzanaki bado haamini…. ' Ukilewa pesa za wizi huwa….' ‘wan ka-confidence na dharau ya hali ya juu….' ‘Unaona wanavyo anza kujenga hoja za ajabu…..' ‘Hapa hafungwi mtu !!' ' Balali katenguliwa uteuzi basi, end of story!'" Alisikika mzalendo mmoja mwenye halisi ya JF Ville akisema jukwaani humo.

Habari za mzalendo huyo zilifikia matuta "nimekusoma mkuu…." Na kuongeza "… Hoja zao hizo za kutaka kupindisha sheria."

Habari hizo zilitapakaa jukwani humo na kudakwa na mtanganyika aishie huko JF Ville "I still wait and see what measures will Attorney general takes. To fight with Mkono is not a easy battle:confused:" alisema kitanganyika(read kimombo) akiashiria nguvu za Mkono huyo. Wanahudhuri huko wali kasana kuonyesha mkono huo "He is still reviewing!"

Mkuu wa majeshi JF Ville kwa kutumia kipaza sauti alimnukuu mwanahudhuria mmoja na kumjibu "Ukistaajabu ya Balali, utayaona ya Mgonja!" haijaeleweka kama huyo balali ni mgonjwa au Mgonja safi!

Akibangaiza mitaa ya kati Famora:cool: JF Ville mwanahudhuria wa jukwaa hilo alidai "Huyu Mzee Mkono naona keshaanza kupagawa" mwandishi wetu alikuwa na butwaa kwani hakuelewa mkono huo unagawa vipi!

Kana kwamba kasheshe za vurumai ndani ya jukwaa hilo zinapamba moto, sauti za mwanahuduria ilisikika ikisema: "Mkono is right…Kazi ya Law Firm yoyote ni exactly hiyo...:mad: sio kazi ya Law firm kuangalia mtu atakuwa guilt or not…so there is no wrong doing for him to help Balali tuache unazi!:p" alimalizia kikasheshe kasheshe, na kimombo.


Kama perogativu;) "Jamani mimi naomba nisaidiwe kuna kitu sielewi hapa kuhusian na huyu fisadi…" alisikika ki nyimbo nyimbo nakuendelea na ubeti huu "I think............"

Wakati ubeti haujamalizika mwandishi wetu alijigandua kwenda kwenye jukwaa lingine mbadala lakini kabla ya kujingatua Wanavijiji wa JF Ville walisikika "si ndiyo wanaitwa mafisadi mabepari wa kijamaa?" akiashiria vibweka vya Huko Danganyika Ville.


Mwandishi wetu amepelekwa kwenye sababu za Rezolusheni….

Kwa habari zaidi bofya hapa…https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=9059.
 
Last edited:
Back
Top Bottom