Kukwepa makazi yaweza kuwa bora kuliko kutoa fidia katika ujenzi au upanuzi wa barabara

jsekiku

Member
Jan 12, 2009
25
7
Jambo ambalo linaniacha mdomo wazi, ni pale ninaposhuhudia ujenzi au upanuzi wa barabara nchini, unapotumia nguvu za ziada kama vile, kubomoa bila huruma, kuvunja bila hata kuzingatia haki za binadamu, kutumia jeshi la polisi kutawanya wananchi wanaokata kubomolewa makazi yao ili kupisha ujenzi au upanuzi wa baranara hizo, unapowaacha wananchi bila makazi, kuharibiwa mashamba.. hata kama uwepo wa barabara mpya ya kisasa ina manufaa kwao.

Sehemu nyingi nchini ambapo ujenzi au upanuzi wa barabara unafanyika, unakuta kuwa, tayari makazi ya wananchi yanaathirika, kwa kuwa ama wanadaiwa wamevamia barabara. Uzoefu wangu umeonyesha kuwa, barabara nyingi zilianzishwa na wananchi kuunganisha vitongoji au vijiji vyao. Maendeleo yaliletwa na wao wenyewe. Kadiri maendeleo yalivyoongozeka, na miundo mbnu nayo ikaongezeka na kukua.

Hoja yangu ni kwamba:

Wakati wa ujenzi wa barabara mpya au wakati wa kupandisha hadhi barabara zilizokuwepo, kwa nini badala ya kuvunja makazi ya wananchi, makazi yao hayo yasikwepwe, ili kupunguza bugudha na usumbufu kwa wananchi hao? Mfano unakuta makazi ya wananchi yamejengwa karibu na barabara jambo ambalo ni sawa miaka mfano 20-30 iliyopita. Kufuatana na maendeleo ya nchi, inaweza kuonekana mwafaka kuweka baranara kuu karibu na kijiji hicho.

Kwa nini wataalam wa ujenzi wa barabara, wasijaribu kukwepa kuharibu au kulipa fidia ili kuwafanya wananchi wapishe barabara inayojengwa? Binafsi naona kuwa,

KUKWEPA MAKAZI yaweza kuokoa pesa nyingi zinazotumika katika kulipa FIDIA. Pesa hiyo ya fidia ingelitumika katika ujenzi halisi wa barabara.

Ninaomba TANROADS na wote wanaohusika katika upanuzi au ujenzi wa barabara, watazame upya suala hili. Badala ya kujikita tuu katika kutoa fidia, waangalie uwezekano wa kukwepa makazi na mashamba ya wananchi, kwa kukwepesha barabara mpya ipite katika maeneo yasiyohitaji KULIPA FIDIA.

Hata hivyo, FIDIA inawezekana kwa majengo, mashamba, makaburi na maendelezo mengine. Hili ni jambo zuri. Lakini ni vigumu kufidia HISTORIA YA MAKAZI hiyo inayofutika kabisa. Na pale inapotumika nguvu ya ziada, yapo maadhara ya kisayikolojia inayojengeka.

Mfano ninaposhuhudia nguvu zikitumika mfano katika KUBOMOA BOMOA makazi ya wananchi wanaokahidi, mbele ya wenye makazi hayo, mbele ya watoto... mfano unaona dreva wa grader inabomoa nyumba, na pengine kuwaacha wananchi wanalia, pengine kukiwa na kutoelwana, ninadhani tunakuwa tunapandikiza ROHO MBAYA ndani ya watoto wetu wanaoshuhudia ubomowaji wa makazi yao au ya wazazi wao.

NAPENDEKEZA, wataalam wa TANROADS waliangalie upya suala hili. Panapowezekana, makazi yakwepwe na barabara kuu zipitishwe katika maeneo yasiyopita katikati mwa vijiji. Hakuna FIDIA inayoweza kutosha. Na si lazima barabara kuu ipite katikati mwa kijiji. Barabara inayounganisha wilaya kwa wilaya au mkoa na mkoa au nchi na nchi, yaweza kukwepa kabisa kuwasumbua wananchi na ikapitishwa katika maeneo yanayowakwepa kabisa, kwani malengo ya barabara hizi kubwa ni kuunganmisha maeneo hayo.
 
Back
Top Bottom