Kukwama kwa miradi mikubwa ya NHC kunaumiza, kunaliza kunasikitisha sana. Ni wazi Nehemia Mchechu alikuwa bora? kwanini Lukuvi na Jenista bado wapo?

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,173
41,976
Wasalaam

Ni wazi kila Mtanzania anajua kabisa hali iliyokuwa nayo shirika la nyumba la Taifa kabla ya ujio wa awamu ya tano ya Hayati John Magufuli... ni wazi kila mmoja wetu atakubaliana nami kuwa shirika lilikuwa limechangamka na lilikuwa na muelekeo mzuri sana na watanzania walikuwa wamewekeza pesa zao nyingi kwenye hiyo miradi mukubwa na wengi wao walikuwa wamenunua miradi husika kabla hata haijaanza ujenzi na kabla ya 2015 ujenzi ulikuwa unaendelea kwa kasi sana.

Nehemia Mchechu pamoja na mapungufu yake kama binadamu wengine lakini shirika hili chini yake lilikuwa limechangamka na lilisaidia kuipamba miji yetu mikubwa hasa jiji la Dare-es -salaam... lakini aliondolewa pale lakini matarajio ya wengi ilikuwa ni kuona shirika hili kusonga mbele zaidi na kumaliza miradi kwa haraka na kwa ufanisi maana yeye alionekana ana matumizi mabaya ikiwemo kufanyia vikao dudai.

Nakumbuka Mh Lukuvi baada ya kumtoa Mchechu alisema kuwa bodi ya shirika ihakikishe inamaliza miradi yote ya zamani kabla ya kuanza mipya lakini ilikuwa kinyume chake bali tukawa tunaona shirika linafanya miradi mipya.

Bado najiuliza Waziri Lukuvu, waziri Jenista Muhagama na Angelina Mabula wanaweza wambia nini watanzania kwenye hili?
Kwanini hawa watu wanaendelea kuwepo pamoja na shirika na miradi kusimama wao wakiwa kwenye viti?

Ikumbukwe miradi mikubwa inayo ongelewa hapa ni
. Kawe City-Dar
.Morroco-Dar
.Capripoint mwanza

Jamani kwenye hii miradi pesa za watanzania zimelala na mikataba ikivunjwa tutakwenda kulipa gharama kubwa kuliko gharama ya kuimalizia ...na ukiangalia hii nmiradi ilikuwa nikumaliziwa tuuu.

Mtu yeyote akipita pembezoni ya miradi hii lazima utasikitika sana, utalia nakujiuliza maswali mengi kuhusu serikali na hatma ya hii miradi na kwanini Lukuvi ameachwa kwenye baraza la mawaziri.

Ni wazi kila mtu atakubaliana namimi kuwa serikali chini ya Hayati Magufuli imechangia kuharibu miradi hii ya NHC ni wazi pengine Nehemia mchechu alionewa na kinachotakiwa hapa ni serikali chinin ya Mama Samia kurekebisha na kuhakikisha miradi hii inakwisha.

Wasalaam
 
Hiyo miradi imejaa wizi na ubadhirifu mtupu!
Eti mtu kama Shambwe unamuweka kama Mkurugenzi pale NHC, kijana mwenye majigambo yaliyopindukia, mhuni tuu na kujiona kwingiii kusikokuwa na kifani.

Sometimes uswahiba na watu wasiofaa ulimgharimu sana Mchechu aliwaweka marafiki zake kwa kupitiliza kwenye key posts ambapo badae walikuja kumgeuka. Most of vijana aliosoma nao darasa moja aliwapa key posts NHC.

Lakini kwa muda aliokaa nje atakuwa amejifunza kitu.
 
Waliagizwa mabadilishe modal yao ya ujenzi haswa kwa zile nyumba zao, unakuta kajumba kadogo lkn iyo gharama yake sasa ... Utakimbia

Lkn ninwazi pia ile miradi yao mikubwa kama Moroco square imekwamaaa kabisa jengo lile naona sasa litaota kutu 😀😀😀
 
Yale maghorofa pale Morocco yamekamilika kwa asilimia kama 80 hivi, lakini yametelekezwa na pesa za watanzania zimelala pale.
 
Wasalaam

Ni wazi kila Mtanzania anajua kabisa hali iliyokuwa nayo shirika la nyumba la Taifa kabla ya ujio wa awamu ya tano ya Hayati John Magufuli... ni wazi kila mmoja wetu atakubaliana nami kuwa shirika lilikuwa limechangamka na lilikuwa na muelekeo mzuri sana na watanzania walikuwa wamewekeza pesa zao nyingi kwenye hiyo miradi mukubwa na wengi wao walikuwa wamenunua miradi husika kabla hata haijaanza ujenzi na kabla ya 2015 ujenzi ulikuwa unaendelea kwa kasi sana....
MKUU amekutuma umsemee nini?kwani kilala wewe unapunguakiwa na nini wakati walikuwa wanajenga na kuuziana wenyewe pia haya mamiradi makubwa yalikuwa ni justification ya upigaji.miradi iko tanzania vikao durbai hao ni wazalendo au!yabaki hivyo hivyo ss hayatusaidii.tunataka miradi enedelevu.mijengo kibao mikoani lkn hakuna wapangaji hiyo akili au matope ya viongozi wetu.wacha yafe tu.
 
Mimi huwa na jiuliza maswali mengi sn kuhusu Tanzania especially kwenye maswala ya Really Estate ambayo hufanywa na mashirika makubwa hivi huwa inafanyikaja study ya kutosha kweli.kwasababu nikiangalia haya majumba makubwa mengi ya mashirika yaliyo jengwa yanakuwa hayana ya wapangaji naweza kusema laabda 20% inakuwa imepangishwa na inakuwa hivyo kwa muda mrefu sn.
 
Yale maghorofa pale Morocco yamekalika kwa asilimia kama 80 hivi, lakini yametelekezwa na pesa za watanzania zimelala pale
Inaumiza sana na habari ni kwamba NHC waliomba hela kumalizia hiyo miradi lakini wakanyimwa toka 2017 wameomba hiyo pesa lakini hadi leo hawajajibiwa... cha msingi hapa ni lazima hiyo miradi imalizwe maana serikali na watanzania wamewekeza pesa nyingi sana
 
MKUU amekutuma umsemee nini?kwani kilala wewe unapunguakiwa na nini wakati walikuwa wanajenga na kuuziana wenyewe pia haya mamiradi makubwa yalikuwa ni justification ya upigaji.miradi iko tanzania vikao durbai hao ni wazalendo au!yabaki hivyo hivyo ss hayatusaidii.tunataka miradi enedelevu.mijengo kibao mikoani lkn hakuna wapangaji hiyo akili au matope ya viongozi wetu.wacha yafe tu.
Mimi sijataka Mchechu arudi lakini unaona ni sawa miradi hii kukwama hadi sasa toka 2014? sio lazima mchechu arudi lakini cha msingi miradi hii imalizike kama ilivyo ahidi serikali
 
Mimi huwa na jiuliza maswali mengi sn kuhusu Tanzania especially kwenye maswala ya Really Estate ambayo hufanywa na mashirika makubwa hivi huwa inafanyikaja study ya kutosha kweli.kwasababu nikiangalia haya majumba makubwa mengi ya mashirika yaliyo jengwa yanakuwa hayana ya wapangaji naweza kusema laabda 20% inakuwa imepangishwa na inakuwa hivyo kwa muda mrefu sn.
Cha msingi hii miradi imalizwe maana watu walisha wekeza pesa zao nyingi sana
 
Hizo apartment wanazouza mil. 200 huyu mtanzania mnyonge anaweza hata kuota kununua kweli? kuna apartments maeneo ya morocco yanapigwa vumbi tu, hivi wanashindwa kupangisha hata kuwapa watu wakae bure angalau wawe wanafanya usafi tu. Hiyo miradi ingekuwa haikufanyika kibadhirifu ingeweza kurudisha pesa hata kwa kuwapangisha wafanyakazi, wafanyabiashara na wajasiriamali.
 
Miradi alishaikopea hela kwa dhamana ya serikali, expenditure control measures zake za ovyo, matumizi mabaya ya mikopo, watu wanapeana tender za ajabu hela za mkopo zikaishia kati.

Bado tena anarudi serikalini impe dhamana ya kukopa yeye mwenyewe mabank hawana imani nae, na kulipa hayo madeni badala ya kujenga nyumba zinazouzika anaweka bei ya nyumba ya vyumba viwili Mkinga Tanga na Lindi kwa 45 million (yule mtu akili zake azikuwa sawa), don’t forget he had economies of scale too. Alipoona nyumba aziuziki kuweza kulipa madeni mzigo akauamishia kwa wapangaji wa NHC walipe madeni yake, hizo kodi alivyokuwa anawaongezea mungu anajua.

Hakujawahi tokea M.D wa ovyo Tanzania kama Nehemia, hao watu walichekewa sana ku abuse wananchi chini ya JK. Deni la taifa 2 trillion kalitengeneza yeye.

Anyway zama za kuharibu nchi zinaelekea kurudi sitoshangaa akipewa ulaji tena, either way Nehemia hana uwezo huo kama anavyosifiwa.
 
Mbona watanzania waliweza kununua? kwa hiyo mradi umesitishwa na kutelekezwa kwakuwa bei ni 200mil?
 
Miradi alishaikopea hela kwa dhamana ya serikali, expenditure control measures zake za ovyo, matumizi mabaya ya mikopo, watu wanapeana tender za ajabu hela za mkopo zikaishia kati.

Bado tena anarudi serikalini impe dhamana ya kukopa yeye mwenyewe mabank hawana imani nae, na kulipa hayo madeni badala ya kujenga nyumba zinazouzika anaweka bei ya nyumba ya vyumba viwili Mkinga Tanga na Lindi kwa 45 million (yule mtu akili zake azikuwa sawa), don’t forget he had economies of scale too. Alipoona nyumba aziuziki kuweza kulipa madeni mzigo akauamishia kwa wapangaji wa NHC walipe madeni yake, hizo kodi alivyokuwa anawaongezea mungu anajua.

Hakujawahi tokea M.D wa ovyo Tanzania kama Nehemia, hao watu walichekewa sana ku abuse wananchi chini ya JK. Deni la taifa 2 trillion kalitengeneza yeye.

Anyway zama za kuharibu nchi zinaelekea kurudi sitoshangaa akipewa ulaji tena, either way Nehemia hana uwezo huo kama anavyosifiwa.
kwa hiyo sasa nini kifanyike kuliko hela kuendelea kulala pale kwanini serikali isiwape hela hiyo miradi ikamalizwa?
 
Back
Top Bottom