Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,182
- 42,001
Wasalaam
Ni wazi kila Mtanzania anajua kabisa hali iliyokuwa nayo shirika la nyumba la Taifa kabla ya ujio wa awamu ya tano ya Hayati John Magufuli... ni wazi kila mmoja wetu atakubaliana nami kuwa shirika lilikuwa limechangamka na lilikuwa na muelekeo mzuri sana na watanzania walikuwa wamewekeza pesa zao nyingi kwenye hiyo miradi mukubwa na wengi wao walikuwa wamenunua miradi husika kabla hata haijaanza ujenzi na kabla ya 2015 ujenzi ulikuwa unaendelea kwa kasi sana.
Nehemia Mchechu pamoja na mapungufu yake kama binadamu wengine lakini shirika hili chini yake lilikuwa limechangamka na lilisaidia kuipamba miji yetu mikubwa hasa jiji la Dare-es -salaam... lakini aliondolewa pale lakini matarajio ya wengi ilikuwa ni kuona shirika hili kusonga mbele zaidi na kumaliza miradi kwa haraka na kwa ufanisi maana yeye alionekana ana matumizi mabaya ikiwemo kufanyia vikao dudai.
Nakumbuka Mh Lukuvi baada ya kumtoa Mchechu alisema kuwa bodi ya shirika ihakikishe inamaliza miradi yote ya zamani kabla ya kuanza mipya lakini ilikuwa kinyume chake bali tukawa tunaona shirika linafanya miradi mipya.
Bado najiuliza Waziri Lukuvu, waziri Jenista Muhagama na Angelina Mabula wanaweza wambia nini watanzania kwenye hili?
Kwanini hawa watu wanaendelea kuwepo pamoja na shirika na miradi kusimama wao wakiwa kwenye viti?
Ikumbukwe miradi mikubwa inayo ongelewa hapa ni
. Kawe City-Dar
.Morroco-Dar
.Capripoint mwanza
Jamani kwenye hii miradi pesa za watanzania zimelala na mikataba ikivunjwa tutakwenda kulipa gharama kubwa kuliko gharama ya kuimalizia ...na ukiangalia hii nmiradi ilikuwa nikumaliziwa tuuu.
Mtu yeyote akipita pembezoni ya miradi hii lazima utasikitika sana, utalia nakujiuliza maswali mengi kuhusu serikali na hatma ya hii miradi na kwanini Lukuvi ameachwa kwenye baraza la mawaziri.
Ni wazi kila mtu atakubaliana namimi kuwa serikali chini ya Hayati Magufuli imechangia kuharibu miradi hii ya NHC ni wazi pengine Nehemia mchechu alionewa na kinachotakiwa hapa ni serikali chinin ya Mama Samia kurekebisha na kuhakikisha miradi hii inakwisha.