Kukwama kwa miradi mikubwa ya NHC kunaumiza, kunaliza kunasikitisha sana. Ni wazi Nehemia Mchechu alikuwa bora? kwanini Lukuvi na Jenista bado wapo?

Wasalaam

Ni wazi kila Mtanzania anajua kabisa hali iliyokuwa nayo shirika la nyumba la Taifa kabla ya ujio wa awamu ya tano ya Hayati John Magufuli... ni wazi kila mmoja wetu atakubaliana nami kuwa shirika lilikuwa limechangamka na lilikuwa na muelekeo mzuri sana na watanzania walikuwa wamewekeza pesa zao nyingi kwenye hiyo miradi mukubwa na wengi wao walikuwa wamenunua miradi husika kabla hata haijaanza ujenzi na kabla ya 2015 ujenzi ulikuwa unaendelea kwa kasi sana.

Nehemia Mchechu pamoja na mapungufu yake kama binadamu wengine lakini shirika hili chini yake lilikuwa limechangamka na lilisaidia kuipamba miji yetu mikubwa hasa jiji la Dare-es -salaam... lakini aliondolewa pale lakini matarajio ya wengi ilikuwa ni kuona shirika hili kusonga mbele zaidi na kumaliza miradi kwa haraka na kwa ufanisi maana yeye alionekana ana matumizi mabaya ikiwemo kufanyia vikao dudai.

Nakumbuka Mh Lukuvi baada ya kumtoa Mchechu alisema kuwa bodi ya shirika ihakikishe inamaliza miradi yote ya zamani kabla ya kuanza mipya lakini ilikuwa kinyume chake bali tukawa tunaona shirika linafanya miradi mipya.

Bado najiuliza Waziri Lukuvu, waziri Jenista Muhagama na Angelina Mabula wanaweza wambia nini watanzania kwenye hili?
Kwanini hawa watu wanaendelea kuwepo pamoja na shirika na miradi kusimama wao wakiwa kwenye viti?

Ikumbukwe miradi mikubwa inayo ongelewa hapa ni
. Kawe City-Dar
.Morroco-Dar
.Capripoint mwanza

Jamani kwenye hii miradi pesa za watanzania zimelala na mikataba ikivunjwa tutakwenda kulipa gharama kubwa kuliko gharama ya kuimalizia ...na ukiangalia hii nmiradi ilikuwa nikumaliziwa tuuu.

Mtu yeyote akipita pembezoni ya miradi hii lazima utasikitika sana, utalia nakujiuliza maswali mengi kuhusu serikali na hatma ya hii miradi na kwanini Lukuvi ameachwa kwenye baraza la mawaziri.

Ni wazi kila mtu atakubaliana namimi kuwa serikali chini ya Hayati Magufuli imechangia kuharibu miradi hii ya NHC ni wazi pengine Nehemia mchechu alionewa na kinachotakiwa hapa ni serikali chinin ya Mama Samia kurekebisha na kuhakikisha miradi hii inakwisha.

Wasalaam
Mwendazake hakupenda kuona mtu mwingine anasifiwa wakati yeye yupo na ameharibu mashirika mengi sana ya umma kwa ubinafsi wake.
 
I am not against serikali kumalizia hiyo miradi, it does make economic sense walau wapate chochote. Lakini huyo Nehemia usimpe sifa ambazo hastaili.

Kama ni hasara tayari washapata commonsense says watakuwa wana top up kila mwezi kwenye madeni ya NHC maana J.K aliiwekea mikopo yao guarantee ya serikali.

Sasa kwanini awaimalizii Dr Mpango na Dotto James watakuwa na majibu mazuri au waliopo sasa kwenye nafasi zao za awali ndani ya wizara ya fedha.

Last I know serikali iliweka kipaumbele kumalizia mradi wa NSSF kigamboni watu waamie, sina uhakika kama kumalizia miradi ya NHC plans zake na zenyewe zipo kwenye pipeline.
hakika
 
Nehemiah Mchechu alikuwa mmoja wa vijana wa Mkwere katika kupiga hela kupitia mikopo toka benki za China!! Jiwe aliliona hilo ndio maana alimuondoa na akaweka uchunguzi ambao sijui uliishia wapi!!! Mkwere akipata nafasi anaweza akamrudisha mchechu pale ili wamalizie miradi yao!!

Lukuvi sasa hivi anapumua hata confidence yake kidogo imerudi kwani kwa Jiwe alikuwa amekalia kuti kavu; sidhani kama mwendazake angekuwepo angekuwa bado Waziri , ishara za kumchoka zilionekana wazi wazi!!!
lakini pamoja na yote alilifanya shirika likawa na nguvu sana
 
Nehemiah Mchechu alikuwa mmoja wa vijana wa Mkwere katika kupiga hela kupitia mikopo toka benki za China!! Jiwe aliliona hilo ndio maana alimuondoa na akaweka uchunguzi ambao sijui uliishia wapi!!! Mkwere akipata nafasi anaweza akamrudisha mchechu pale ili wamalizie miradi yao!!

Lukuvi sasa hivi anapumua hata confidence yake kidogo imerudi kwani kwa Jiwe alikuwa amekalia kuti kavu; sidhani kama mwendazake angekuwepo angekuwa bado Waziri , ishara za kumchoka zilionekana wazi wazi!!!
Haya, baada ya kumuondoa mpiga dili, Magufuli alivyomuweka jamaa yake asiyempiga dili, maendeleo yako wapi hata nusu ya yale aliyokuwa anafanya msechu?
 
Real estate sasa iv ime fulia sanaaa mfano tu kuna jengo pale la pembeni moroco sijui lina floor kama 7 iv hamna wapangaji ...maofisi yana fungwa
Ofisi za nini kwenye zama za teknohama..
Watu wafungua ofisi kwenye laptop na waajiriwa wote wana laptop kwisha mchezo....
Wazungu wenyewe ulaya wanalia na magorofa yao hamna watu wanapanga kufungua ofisi....
 
Miradi alishaikopea hela kwa dhamana ya serikali, expenditure control measures zake za ovyo, matumizi mabaya ya mikopo, watu wanapeana tender za ajabu hela za mkopo zikaishia kati.

Bado tena anarudi serikalini impe dhamana ya kukopa yeye mwenyewe mabank hawana imani nae, na kulipa hayo madeni badala ya kujenga nyumba zinazouzika anaweka bei ya nyumba ya vyumba viwili Mkinga Tanga na Lindi kwa 45 million (yule mtu akili zake azikuwa sawa), don’t forget he had economies of scale too. Alipoona nyumba aziuziki kuweza kulipa madeni mzigo akauamishia kwa wapangaji wa NHC walipe madeni yake, hizo kodi alivyokuwa anawaongezea mungu anajua.

Hakujawahi tokea M.D wa ovyo Tanzania kama Nehemia, hao watu walichekewa sana ku abuse wananchi chini ya JK. Deni la taifa 2 trillion kalitengeneza yeye.

Anyway zama za kuharibu nchi zinaelekea kurudi sitoshangaa akipewa ulaji tena, either way Nehemia hana uwezo huo kama anavyosifiwa.
 
NHC ya Mchechu ilikuwa inalenga wenye hela ndefu tu. Nyumba zinauzwa Tshs. milioni 250 hadi milioni 360!

Ni vema kibiashara kujenga nyumba za bei mbaya kwa ajili ya wenye hela, lakini wangejigawa wakajenga na nyumba za sio zaidi Tshs. milioni 30 kwa ajili ya wananchi wa ngazi ya chini. Na pia Tanzania inahitaji nyumba ambazo mtu anaweza akamudu kuimiliki kwa malipo ya pesa sawa na kodi ya pango kila mwezi. Yaani mtu alipe Tshs. 100,000/- kwa mwezi, 200,000/- kwa mwezi au 300,000/- mpaka amalize bei ya nyumba. Hata akipewa miaka 20 au 30 kulipa sio mbaya.

Mkataba uwe mkali kuwa akichelewesha malipo kwa miezi kadhaa (miwili au mitatu sio mbaya) nyumba yake inawekwa sokoni kwenye mnada ambapo mnunuzi atatakiwa kulipa kwa mkupuo pesa yote ambayo mkazi huyo ameshalipa mpaka hapo aliposhindwa.
 
Back
Top Bottom