Nemesis
JF-Expert Member
- Feb 13, 2008
- 5,462
- 4,364
Uwanja wa CCM Kirumba ambao unamilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM)
Enzi za chama kimoja, majengo na maeneo yote ya umma yalikuwa chini ya Serikali. Ujenzi na uendelezaji wa maeneo hayo ulifanya na Serikali kupitia kodi za wananchi, michango, fedha za wafadhili na wahisani mbalimbali.
Kwa namna isiyoeleweka baadhi ya maeneo hayo yameporwa na CCM na kuwa mali ya chama.
Kwa uchache tu natoa mfano: Uwanja wa CCM Kirumba (Mwanza), Samora (Iringa), Sokoine (Mbeya), Shekh Amri Abed (Arusha), Majimaji (Songea), Kaitaba (Kagera) nk.
Umiliki huu ni kero siyo tu kuikosesha mapato Serikali bali kero kwa wanamichezo, wananchi wa kawaida na Halmashauri za Manispaa/Miji. Kwa mfano: fuatilia habari hiihapa chini: kero zilizojitokeza
1) CCM (M)Iringa imefunga uwanja wa Samora hali inayowanyima haki wananchi kub urudika.
2) Ligi wa Taifa ngazi ya mkoa imevurugwa kwa kukosa uwanja
3) Matamasha yaliyopangwa kufanyika yamevurugwa.
Swali: Mpaka lini viwanja hivi vitabaki mikononi mwa CCM badala ya Serikali kuu au Halmashauri husika?
Wakati mfumo wa chama kimoja haikuwa rahisi kujua miradi ya umma na ya chama. Miradi iliyoanzishwa kwa ajili ya chama ilikuwa na dhumuni moja: kuhamasisha sera ya chama kimoja. Ndio maana ulikuwa ukichaguliwa mwenyekiti wa chama mkoa, ukuu wa mkoa unakuja automatic.
Tulipobadili mfumo na kuingia mfumo wa vyama vingi miradi iliyojengwa kwa ajili ya chama lakini kimsingi ni ya umma ilibaki kuwa ya chama.
Mfano viwanja vya mpira na ofisi za uongozi kama mkuu wa mkoa. Kulikuwa hakuna haja ya kujenga viwanja viwili sehemu moja yani cha chama na serikali, kulikuwa hakuna haja ya kujenga ofisi ya mkuu wa mkoa na mwenyekiti wa mkoa wa chama: ilikuwa ni kitu kimoja.
Wazo langu ni kwamba miradi mikubwa kama viwanja virudishwe viwe mali ya umma, haiwezekani mikoa yote viwanja viwe vya CCM, viwanja viwe mali ya umma chini ya halmashauri za mikoa.
Ofisi wanaweza kuchukua lakini si viwanja. Wengi mtakuwa mnafahamu baada ya mfumo wa vyama vingi katibu wa CCM wilaya alikuwa na ofisi kuliko mkuu wa mkoa.
Tuige KENYA: baada ya kibaki kuingia madarakani aliuchukua ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta toka KANU. Alisema ni mali ya wakenya, ni jasho la wakenya chini ya mfumo wa lazima wa chama kimoja
KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI YANENA
KAMBI rasmi ya upinzani bungeni, imeitaka serikali kuvichukua viwanja vyote hapa nchini vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho hakivihudumii inavyostahili.
Ushauri huo ulitolewa jana na Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Joseph Mbilinyi 'Sugu' ambapo alisema baada ya serikali kuvichukua viwanja hivyo, ianzishe Mamlaka ya Viwanja vya Michezo.
Sugu alisema mamlaka hiyo ipewe jukumu la kuviboresha viwanja hivyo ili vitumike kwa maslahi ya Watanzania wote, badala ya utaratibu wa sasa ambapo CCM ndiyo yenye kuvimiliki.
Alivitaja viwanja hivyo kuwa ni Majimaji Songea, Sheikh Amri Abeid Arusha, Viwanja vya Jamhuri Morogoro na Dodoma, ule unaoitwa Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza na vingine vyote vilivyomilikishwa kwa CCM.
"Viwanja hivi nilivyovitaja na vinginevyo vilijengwa na wananchi wote wakati wa utawala wa chama kimoja na hivyo CCM haipaswi kuvimiliki bali serikali ambayo ni ya wananchi wote inatakiwa ivimiliki.
Mbali na sababu hiyo, viwanja hivyo havihudumiwi kwa kiwango, tunaitaka serikali ivirejeshe mikononi mwake na kuanzisha mamlaka itakayovihudumia," alisema.
Aliongeza kuwa mamlaka hiyo kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya serikali, ipewe jukumu la kuhakikisha kila mwaka inajenga vituo vya kisasa vya mazoezi na hosteli kwa ajili ya wanamichezo na angalau kiwanja kimoja kikubwa chenye hadhi ya kimataifa inayolingana na Uwanja mpya wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Sugu alisema, inasikitisha kuona miaka 50 baada ya Uhuru, Tanzania ina uwanja mmoja tu wenye hadhi ya kimataifa ambao ni Uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam, uliojengwa kwa msaada wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu.
Aliongeza kuwa kiwanja hicho kimekuwa hakiendeshwi vizuri hata kulitia aibu taifa kwa huduma mbovu, ikiwemo ya kukatika kwa umeme kama ilivyotokea hivi karibuni wakati wa fainali za michuano ya Kombe la Kagame ambalo Tanzania ilikuwa mwenyeji.
Wakati huohuo, Mbilinyi alisema Tanzania imeshindwa kuzalisha walimu wa kutosha wa michezo mbalimbali na mbaya zaidi, hata wachache wazalendo hususan wa soka, wenye ujuzi na umahiri wa kuridhisha, wamekuwa hawapewi motisha, pindi wanapoteuliwa kufundisha timu za taifa.
Alisema, serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa kuwapa ajira walimu wa kigeni, ambao wanakuja hapa nchini kuzifundisha timu za taifa.