Kukutana na wale Mliosoma wote zamani, kuna umuhimu gani?

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,182
3,547
habari wadau zenu wadau natumai mko powa.

Jamani mimi nimemaliza darasa la saba mwaka 2001 ila tangu juzi kuna marafiki zangu
tuliokuwa tunasoma darasa moja shule ya msingi. Walinitumia meseji kwamba .

Katika watu tuliosoma pamoja wameandaa sherehe ya flani ya watu tuliosoma pamoja kuweza kuonana. Sehemu flani ivi tukutane huku tukipata vinywaji na kubadilishana mawazo.....na kukumbushana mengi ya zamani.

Swali je, School reunion zina umuhimu gani Maana ukiangalia baada ya watu kumaliza shule muda mrefu mkionana watu mtakuwa mnatofautiana kuna wengine wameowa, kuna wengine wako sehemu nzuli serikalini, kuna wengine mambo yao mazuli ,

Kuna wengine hali yao ya kimaisha ngumu.

Ni nzuri na mbaya kwa upande wa Pili
Faida zake ni nyingi
-Ni kwamba inavuta hisia za mbali za maisha ya shule,kwahiyo ni rahisi saana kujua kwamba kila mmoja ndoto zake alizokuwanazo zimetimia au la
-Husaidia saana kimaisha katika kila mmoja,maisha ya sasa lazima uwe na link,sasa hii itafanya kila mmoja ajue mwenzie anafanya nini,kama ni mfanyabiashara basi anaweza kutanua biashara kwa upande ambao mwenzie yupo kama kuna fursa.
Kama ni muajiriwa basi ni muda wa kupeana hamasa za kazi.
-Kubwa zaidi ni kusaidiana pale mmoja wenu anapokuwa hana ajira,na itakuwa rahisi kumsaidia either kumuunganisha sehem yenye ajira,hapo kuna direct na indirect,unaweza kukuta mnasaidiana nyie au ndugu zenu on backside.
Kwa ufupi ni nzuri kupita maelezo,ila kwa wenye akili,ni sehem kubwa saana ya fursa kimaisha hasa kwa sie watu wa biashara.

Ubaya wake:-
Kama mkeo ndio anakuambia anaenda kwenye Makutano hayo kwamba anaenda kukutana na aliosomanao.
Basi hapo lazima ujue kwamba asilimia kubwa ya mtu aliemgegeda Shuleni watakutananae.Na asikudanganye mtu,Mtu hata kama ameolewa,akikutana na Classmate mwenzie alimuanzisha basi ni rahisi saaana kushawishika tena.Unaweza kuchezwa mchezo hata kama wewe upo.
Maana wewe unakuwa ni mualikwa tu,ila wao ndio wenye shughuli na maongezi yao si lazima na wewe uwe muongeaji na yapo maongezi ya one to one,na pia kubadilishana number za sim.Hapo ndio kazi inaanza.
Ila sio wote wanaweza kufanya hivyo,ila asilimia kubwa hali hii inakuwapo.
 
Inasaidia pia kama ulikuwa na mtu unampenda kipinde kile lakini hukuwa na uwezo wa kumpata, sasa ndiyo muda muafaka wa kukonga roho yako. Ingawa haitakuwa kama zama zile lakini umempata.
 
Sijui niseme nimeshangaa. Nilipoisoma hiyo heading tu nilidhani umesoma na mh. Magufuli au Lowasa kumbe ni jana tuu unaiita zamani?? Sawa boss nenda kakutane mjazane udogooo wenyu
 
Inaelekea umesoma shule ya kimasikini sana na hao uliomaliza nao wameishia kuwa watu walio chini ya level yako. Ndo maana unaona hata ukienda hawatakusaidia kitu.
Reunion ni kitu kizuri sana kwasababu mmeshare the same history for years, its a place to re-establish the lost connection.
Mashule makubwa yana re-union hadi wanaamua kujenga charities au wanaunda taasisi za kuisaidia shule yao. Wengine wanakuwa madaktari, maengineer, walimu etc. utawahitaji siku moja and through wao utakutana na wengine zaidi.
Through your older friends utakutana na wengine wa muhimu zaidi. Wao wana act kama daraja la kwenda mbele zaidi cause it is easier kukusaidia.
How long will you try to make new friends and drop the old ones? Usiwadharau kwasababu hujui ni lini na wapi watakusaidia.
Old is gold.
I'm talking from experience.
 
Umeongea vzur sana mkuu!
 
"The most valuable ANTIQUES are dear old FRIENDS"- H. Jackson Brown Jr
 
Wewe utakuwa umesoma Mnazi Mmoja shule ya msingi.
Na umemaliza darasa moja na mimi.
Simple usije wenzako tutaenda unajidai sana na kujiona great thinker.
Nishakujua
 
Wewe utakuwa umesoma Mnazi Mmoja shule ya msingi.
Na umemaliza darasa moja na mimi.
Simple usije wenzako tutaenda unajidai sana na kujiona great thinker.
Nishakujua

Heee,haya sasa mapya yanaibuka hapa.
Werrrrrrrrrrrrraaaaaaaaaa,AMU mwaga sssseraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,kumbe jamaa anazuga humu sio
 
Wewe utakuwa umesoma Mnazi Mmoja shule ya msingi.
Na umemaliza darasa moja na mimi.
Simple usije wenzako tutaenda unajidai sana na kujiona great thinker.
Nishakujua

una ugomvi wewe.!! huyu jamaa hataki kwenda kukumbushia mgegedo wake
 
watu siku hizi wamatumia mitandao ya kijamii kuunda kamati za harusi na send off.
ukiwaambia kuna mwenzenu ana shida anahitaji msaada wanakaa kimya.
mkikaa kimya kwenye hiyo michango ya send offs na harusi wanaanza kulalamika.
oooh! tunahitaji kusaidiana na upuuzi mwingine mwiiiingi.

hivi mgonjwa na anayefunga harusi ya kifahari nani anahitaji kusaidiwa?
kwani send off/harusi lazima uweke sherehe kubwa?
yaani mi mtu akinitafuta tumesoma wote ananikumbuka kwenye michango ya send off/harusi ndio kabisaaa sitoi.
 
Ni nzuri na mbaya kwa upande wa Pili
Faida zake ni nyingi
-Ni kwamba inavuta hisia za mbali za maisha ya shule,kwahiyo ni rahisi saana kujua kwamba kila mmoja ndoto zake alizokuwanazo zimetimia au la
-Husaidia saana kimaisha katika kila mmoja,maisha ya sasa lazima uwe na link,sasa hii itafanya kila mmoja ajue mwenzie anafanya nini,kama ni mfanyabiashara basi anaweza kutanua biashara kwa upande ambao mwenzie yupo kama kuna fursa.
Kama ni muajiriwa basi ni muda wa kupeana hamasa za kazi.
-Kubwa zaidi ni kusaidiana pale mmoja wenu anapokuwa hana ajira,na itakuwa rahisi kumsaidia either kumuunganisha sehem yenye ajira,hapo kuna direct na indirect,unaweza kukuta mnasaidiana nyie au ndugu zenu on backside.
Kwa ufupi ni nzuri kupita maelezo,ila kwa wenye akili,ni sehem kubwa saana ya fursa kimaisha hasa kwa sie watu wa biashara.

Ubaya wake:-
Kama mkeo ndio anakuambia anaenda kwenye Makutano hayo kwamba anaenda kukutana na aliosomanao.
Basi hapo lazima ujue kwamba asilimia kubwa ya mtu aliemgegeda Shuleni watakutananae.Na asikudanganye mtu,Mtu hata kama ameolewa,akikutana na Classmate mwenzie alimuanzisha basi ni rahisi saaana kushawishika tena.Unaweza kuchezwa mchezo hata kama wewe upo.
Maana wewe unakuwa ni mualikwa tu,ila wao ndio wenye shughuli na maongezi yao si lazima na wewe uwe muongeaji na yapo maongezi ya one to one,na pia kubadilishana number za sim.Hapo ndio kazi inaanza.
Ila sio wote wanaweza kufanya hivyo,ila asilimia kubwa hali hii inakuwapo.

aiseee mkuuu nimeipenda hiyoo analysis......nadhani hapa nimeanza kujifunza kituu
 
Nilijaribu kuattend nikaambulia umbea na kuchonganishana. Hata wale friends niliokuwa na amini ni genuine wakapotezwa. For real hakuna kitu kinawauma kama kuona waliokuwa wanadoji nao class wako wamewazidi kwa kila kitu...lazima wakupige majungu na kukuharibia hata old network uliyokuwa nayo inayorelate nao kwa namna moja.
Binfsi nimesaidiwa sana na new friends (some were even not friends) kuliko old ones. We meet we link up..
Sasa subiria hao old friends mmoja aoe au kuolewa wanavyoomba mchango....haha harusi sichangii hata kwa dawa. Yangu ntachangiwa na familia kitakachopatikana hichohicho kitatumika. Mayatima wamejaa nikanunulie watu pombe???
 
kuweka link
kufahamu swoc zako
kusaidia na kusaidiwa
kupata uliowapoteza
kiukweli its a good thing
 
We jamaa sanasana utakuwa unasumbuliwa na inferiority complex tu,kwamba uko nyumba kimaendeleo kuliganisha na hao ex classmates wako na ulikuwa mzuri tu class ama utakuwa teacher wewe maana ndo huwa wako very inferior kukutana na watu wa kada zingine hasa waliosoma nao.

Faida unazijua sana sema unazuga tu.

No offense!!
 
Back
Top Bottom