Kukumbushana ni Muhimu, kama wewe ni Mzazi soma hapa Tafadhali.

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
42,167
2,000
Shule jamani shule,

Tuko ndani ya mwezi December xmass hiyo around the corner, kwa wale Wazazi wenzangu tuliogoma kusomesha watoto zetu kwenye shule za Umma tunajukumu mbele yetu.

Kinachonisikitisha Watanzania japo si wote tunaishi kiholela holela bila mipango wala bajeti, utadhani mwezi December haupo kwenye kalenda na January huwa inasubili kama mwandamo wa mwezi.

Madhumuni ya thread hii ni kukumbushana kama mfuko umekaa vizuri ni jambo la heri kabisa kuwahi benki na kulipa school fees ya mtoto/watoto na ubaki na pay in slip yako kwa ajili ya kuifikisha shuleni siku ya kwanza shule itakapofunguliwa.

Msisubili January hiyo muanze maandalizi ya zima moto tuanze kupigana mizinga na kujiingiza kwenye mikopo ya riba ambayo haina maana yoyote, wote tumechoka lakini kidogo tunachopata tunajitahidi kuishi kwa bajeti na malengo.

Na wale Wazee wa nyumba ndogo nawaomba kama unasomesha mwezi huu ziambie zikukalie mbali kabisa umebanwa na familia muonane after January.

Ni hayo tu mtaikumbuka thread hii siku si nyingi.......
 
PetCash

JF-Expert Member
Mar 20, 2012
1,993
2,000
Hehe!
Waambie mkuu....wasisahau na kununua ving'amuzi mwisho wa analogia ndo huu
 
Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
42,167
2,000
reminder bora kabisa hii!!!
Ni kweli kabisa maana kuna wengine nawaona wako bize kujiandaa na xmass wakati 6 January shule zinafunguliwa unaishia kwenda kukopa mikopo ya kijinga yenye riba za juu.
 
SnowBall

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
3,054
1,750
Watu tunapenda sana 'mambo yanayotupa starehe ya muda mfupi'...xmass na idd will never end!!
Ndo maana ukitwambia tuchangie harusi utatupata wengi tu..twambie sasa tuchangie kujenga shule..lol
ila ubarikiwe kwa kutukumbusha!!
 
Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
14,527
2,000
Asante mkuu kwa kutukumbusha. Kabla ya nguo ya sikuku na mapochopocho tufunguke kwa ada kwanza!!! Aibu mtoto anaanza muhula mzazi unasuasua ada wakati krismas na mwaka mpya watu walilala kwako kwa kuvimbiwa na ulevi!!! Na nyumba ndogo mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh!!!
 
Kaunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
12,546
2,000
Duh mimi nimrtokamo na Ada imeniacha penniless, mpaka April ndio nachimbua tena!
Ila Asante for reminding us.
 
Mr Rocky

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
15,188
2,000
Dah mkuu Matola asante sana kwa taarifa hii muhimu sana
Maana unaweza shangaa mwezi januari unaaibika kabisa aise
Bora kujiepusha na starehe za mwisho wa mwaka tumalize masuala ya ada kwanza
Mkuu SnowBall heshima yako mkuu
 
Last edited by a moderator:

Nimeshapitia Maisha ya kukopa kwa ajili ya kuendekeza starehe za kijinga, Mtoto kurudishwa shule kwa sababu ya Ada ni aibu kwa sisi hasa Baba zao, hata kama hatuna kitu kujipanga mapema ni muhimu.
 
Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
14,527
2,000
Duh mimi nimrtokamo na Ada imeniacha penniless, mpaka April ndio nachimbua tena!
Ila Asante for reminding us.

Jambo zuri sana mkuu Kaunga. Naongezea kuwa kama mtu una uwezo ukilipa ya mwaka mzima unabaki stress free kabisa na mtoto unamjengea confidence na kuonyesha you a responsible parent!! Watoto nao wanajifunza kwetu kuona kuwa ada is very compulsory na wakikua watafuata nyayo zenu.
 
zhi you nhi

Member
Dec 16, 2012
60
0
Shule jamani shule,

Tuko ndani ya mwezi December xmass hiyo around the corner, kwa wale
Wazazi wenzangu tuliogoma kusomesha watoto zetu kwenye shule za Umma
tunajukumu mbele yetu.

Kinachonisikitisha Watanzania japo si wote tunaishi kiholela holela bila
mipango wala bajeti, utadhani mwezi December haupo kwenye kalenda na
January huwa inasubili kama mwandamo wa mwezi.

Madhumuni ya thread hii ni kukumbushana kama mfuko umekaa vizuri ni
jambo la heri kabisa kuwahi benki na kulipa school fees ya mtoto/watoto
na ubaki na pay in slip yako kwa ajili ya kuifikisha shuleni siku ya
kwanza shule itakapofunguliwa.

Msisubili January hiyo muanze maandalizi ya zima moto tuanze kupigana
mizinga na kujiingiza kwenye mikopo ya riba ambayo haina maana yoyote,
wote tumechoka lakini kidogo tunachopata tunajitahidi kuishi kwa bajeti
na malengo.

Na wale Wazee wa nyumba ndogo nawaomba kama unasomesha mwezi huu ziambie
zikukalie mbali kabisa umebanwa na familia muonane after January.

Ni hayo tu mtaikumbuka thread hii siku si nyingi.......

Da we noma,una akili coz unaona mbali...
 
Mr Rocky

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
15,188
2,000
Nimeshapitia Maisha ya kukopa kwa ajili ya kuendekeza starehe za kijinga, Mtoto kurudishwa shule kwa sababu ya Ada ni aibu kwa sisi hasa Baba zao, hata kama hatuna kitu kujipanga mapema ni muhimu.

Ni aibu tena aibu kubwa sana mkuu kwenda kukopa kwa ajili ya kulipia ada ya mtoto wakati kwa sikukuu nzima ulikuwa unaonekana viti virefu
 
SnowBall

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
3,054
1,750
Mr Rocky nipo bro...sema mambo mengi ndio maana tunapishana!
Usisahau bwana kumalizia ada za wanetu...maana nyie wazee wa arachuga 'kwenu kila siku sherehe'
Nikipata NAULI ntakuja one time kuwasalimia pande hizo za Ar JF wing......

Dah mkuu Matola asante sana kwa taarifa hii muhimu sana
Maana unaweza shangaa mwezi januari unaaibika kabisa aise
Bora kujiepusha na starehe za mwisho wa mwaka tumalize masuala ya ada kwanza
Mkuu SnowBall heshima yako mkuu
 
Last edited by a moderator:

Suprise

JF-Expert Member
Nov 2, 2012
2,697
2,000
Shule jamani shule,

Tuko ndani ya mwezi December xmass hiyo around the corner, kwa wale Wazazi wenzangu tuliogoma kusomesha watoto zetu kwenye shule za Umma tunajukumu mbele yetu.

Kinachonisikitisha Watanzania japo si wote tunaishi kiholela holela bila mipango wala bajeti, utadhani mwezi December haupo kwenye kalenda na January huwa inasubili kama mwandamo wa mwezi.

Madhumuni ya thread hii ni kukumbushana kama mfuko umekaa vizuri ni jambo la heri kabisa kuwahi benki na kulipa school fees ya mtoto/watoto na ubaki na pay in slip yako kwa ajili ya kuifikisha shuleni siku ya kwanza shule itakapofunguliwa.

Msisubili January hiyo muanze maandalizi ya zima moto tuanze kupigana mizinga na kujiingiza kwenye mikopo ya riba ambayo haina maana yoyote, wote tumechoka lakini kidogo tunachopata tunajitahidi kuishi kwa bajeti na malengo.

Na wale Wazee wa nyumba ndogo nawaomba kama unasomesha mwezi huu ziambie zikukalie mbali kabisa umebanwa na familia muonane after January.

Ni hayo tu mtaikumbuka thread hii siku si nyingi.......

asante mtoa mada ingawa umetunyanyapaa tusio wazazi ingawa nasi tuwalezi na hizo ada tunazifeel ileile
 
Mr Rocky

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
15,188
2,000
Mr Rocky nipo bro...sema mambo mengi ndio maana tunapishana!
Usisahau bwana kumalizia ada za wanetu...maana nyie wazee wa arachuga 'kwenu kila siku sherehe'
Nikipata NAULI ntakuja one time kuwasalimia pande hizo za Ar JF wing......

hakuna mbaya mkuu SnowBall
karibu sana mji wetu huu na utatukuta wenyeji tuko mkuu
Nishamaliza mapema sana mkuu na anasubiri tuu kwenda shule hapo mwakani kaka
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom